Mshahara mpya kutangazwa leo

Feedback

JF-Expert Member
Mar 14, 2011
7,988
4,507
OFISI ya Rais leo itawasilisha Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2011/12 bungeni, huku wafanyakazi wa umma, wakitarajia kusikiliza kiasi kilichoongezwa katika mishahara yao.

Sekta binafsi vipi TUCTA wanasemaje.
 
Huo mshahara utakaoongezwa utaweza kweli ku 'offset' effects za mfumuko wa bei?

Uongo mtupu na uhadaa wa kiini macho.

Watu wana njaa
 
Leo ni BAJETI ya ofisi ya rais menejimenti ya utumishi wa umma na utawala bora huku kila mfanyakazi jicho na masikio yao wakielekeza BUNGENI Dodoma
kwa maslahi yao, miezi kadha iliyopita Rais Kikwete aliahidi kuwaongezea mishahara wafanyakazi wake huku akiwa amekaa na viongozi wa TUCTA
na kuwahakikishia kuwa wasahau yote yaliyopita na wagange yajayo jambo ambalo lilifanya TUCTA kumualika Rais wangu Kikwete tofauti na
mwaka jana.
SWALI NI JE WATAONGEZA KAMA WALIVYOKUBALIANA KWA KIWANGO CHA TSH 315000 KWA KIMA CHA CHINI?????
 
Huo mshahara utakaoongezwa utaweza kweli ku 'offset' effects za mfumuko wa bei?Uongo mtupu na uhadaa wa kiini macho.Watu wana njaa
Hayo ni lazima wayazingatie kama wanania ya dhati ya kuongeza mshahara vinginevyo ni usanii ule ule tulouzoea!
 
Kwa yeyote mwenye matarajio mema kwa serikali hii nampa pole, tuliahidiwa kwamba kodi mbalimbali za mafuta zitarejewa na kupunguzwa lakini huo kwa hakika ni ungo hali ya mafuta imezidi kuwa mbaya
 
Leo ni BAJETI ya ofisi ya rais menejimenti ya utumishi wa umma na utawala bora huku kila mfanyakazi jicho na masikio yao wakielekeza BUNGENI Dodoma
kwa maslahi yao, miezi kadha iliyopita Rais Kikwete aliahidi kuwaongezea mishahara wafanyakazi wake huku akiwa amekaa na viongozi wa TUCTA
na kuwahakikishia kuwa wasahau yote yaliyopita na wagange yajayo jambo ambalo lilifanya TUCTA kumualika Rais wangu Kikwete tofauti na
mwaka jana.
SWALI NI JE WATAONGEZA KAMA WALIVYOKUBALIANA KWA KIWANGO CHA TSH 315000 KWA KIMA CHA CHINI?????

Duh ngoja niwahi kazini maana maisha yamepanda sana nikipoteza ajira ni issue.kamshahara hakatoshi nyumba ya kupanga usiseme,chakula ndo kabithaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa!! Magamba wanaenjoy tu!
 
Chochote kill kitaongezwa ni bora kuliko kutoongezewa. Mimi naomba tuu waeke mipango sio wanatuongezea mshahara alafu wanachelewa kutulipa wakitafuta hizo hela na sisi tutaabikr
 
Mshahara ukipanda, bei za vitu navyo juu!! Nauli juu, haubaki na kitu. Hapo solutions ni kucontrol mfumko wa bei siyo hii brah brah za kisiasa kila sehemu. Ngojeni mtaona, ugumu wa maisha utaongezeka mara dufu.
 
Wanaweza kuongeza hata 500/=tu kama walivopunguza % ya kodi kwny mishahara ikaonesha effect ya sh. 1000 tu!/month.
 
Back
Top Bottom