Mshahara kuchelewa

Nyamtala Kyono

Senior Member
Sep 23, 2010
163
34
Ndugu, naomba mchango wenu.

Hivi kwa mwajiri kuchelewesha mishahara ya wafanyakazi kwa zaidi ya siku 50 mpaka 90 akisema pesa ya kulipa mishahara haijapatikana (na ni kweli haipo,sababu kampuni inategemea mapato kutoka katika uzalishaji), je sababu hii inaweza kumwondolea lawama mwajiri? Je wafanyakazi, kama kundi au mtu mmoja mmoja wana weza fanya nini?

Naomba michango yenu. Na, samahani kwa kuposti mahala hapa sababu nimeona swali langu linaendana na jukwaa hili, lakini pia nimeona jukwaa hili linatembelewa zaidi

Asante
 
Ni utamaduni wa kitanzania tu kuto jali kwa sababu mishahara huwa na budget yake kwa mwaka mzima sasa haiingii akilini kabisa kuwa mwajiri hana pesa ya mishahara.Fuateni taratibu za kisheria kwa mjibu wa mikataba yenu ya ajira.
 
Ni kweli Dangala. Pia niliwahi kusikia kuwa ni kosa kisheria kwa mwajiri kutomlipa mshahara mwajiriwa wake wakati tayari amekwisha fanyia kazi...tayari nguvu zake zimekwishatumika, sijui hii imekaaje.nadhani wataalam zaidi watatusaidia
 
Back
Top Bottom