Mseto na mchuzi wa nazi wa samaki

gorgeousmimi

JF-Expert Member
Jun 21, 2010
8,853
1,500
Mahitaji ya mseto
 • Mchele vikombe viwili
 • Choroko vikombe vitatu
 • Tui bubu kikombe kimoja
Jinsi ya kutayarisha
Chemsha choroko mpaka ziive,punguza kiasi weka kando.Weka mchele ulooshwa kwenye choroko zilikwisha iva,ongeza maji ili vitote na punguza moto ili viive taratibu,Funika.Koroga mara kwa mara ili vivurugike.Dhumuni ni kuchanganya choroko na mchele viwe tepetepe.Vikishaiva na kuchanganyika weka tui bubu na chumvi kiasi hakikisha mchanganyiko wako umekazana,utakuwa unaongezea tui taratibu kidogodogo.Mwishoni mwagilia zile choroko ulizozitenga na usonge mseto kabla ya kuuepua

Mchuzi wa nazi
Mahitaji
 • Samaki mmoja(changu)
 • Kitunguu swaumu kijiko kimoja cha supu
 • limau
 • kitunguu kimoja
 • nyanya mbili
 • Mabamia madogomadogo kama 7
 • Tui la nazi vikombe viwili tui maji na kikombe kimoja tui bubu
 • Chumvi
 • Mafuta
 • Pilipili
 • Binzari

Jinsi ya kutayarisha samaki
Mtayarishe samaki na mkate vipande vitatu au vinne.Muweke kitunguu swaumu,chumvi,pilipili ukipendelea na limau.Muache akolee viungo kama kwa lisaa limoja.
Mkaange kwenye mafuta kama kawaida.

Jinsi ya kutayarisha mchuzi wa nazi
Kata kitunguu na ukikaange kwenye vijiko vitatu vya supu vya mafuta,kikianza kubadili rangi weka nyanya ilomenywa na kukatwa vipande na chumvi kiasi,binzari kijiko kimoja cha chai na ukaange mpaka nyanya zilainike na zipondeke.Weka tui maji la nazi na ukoroge mpaka mchuzi ukazane.Weka mabamia yalokatwa ncha na uache yaive.Yakikaribia kuiva weka tui bubu na mwisho samaki.Uache utokote dakika kadhaa nazi iive.
20140219_195558-1.jpg

Karibuni,msosi huu unasababisha watu kuvimbiwa taratibu ukiula :dance:
 

gorgeousmimi

JF-Expert Member
Jun 21, 2010
8,853
1,500
Heeee huu mseto unanikumbusha mbali shost

Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums
Mseto ukila unaona hushibi subiri kama robo saa usikilize ngoma na ukishashushia na maji sijui choroko zinavimba chumboni maana kukaa pia unaweza uone karaha inabidi ulale ili chakula kisawajike vizuri ha ha ha
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom