Msemo huu unakufanya ubweteke na usichukue hatua kusonga mbele kimaisha haraka

Infinite_Kiumeni

JF-Expert Member
Jan 23, 2023
382
661
Utapata/ itakuja kadri muda unavyozidi kwenda.

Utapata busara kadri muda unavyozidi kwenda.

Yote ina maana moja kwamba we usijali, muda upo. Endelea kusubiri mambo yatakua vizuri yenyewe.
.
Huo msemo ukuzuia kuchukua hatua pale unapoacha kutafuta uzoefu wa kitu fulani.
Ukiamini kuwa utakipata tu ukikua.
.
Hapana, utapata kutokana na uzoefu katika icho kitu.
.
Kama ni muoga, utaendelea hivyo hadi uamue kubadilika kutafuta uzoefu.

Kama ni mvivu, utaendelea hivyo hadi uamue kupata uzoefu wa kushughulika.

Kama ni jasiri, utaendelea hivyo na utapata uzoefu zaidi.
.
Kinachohitajika ni maamuzi yako, aitha uutumue huu muda kujenga uzoefu au utulie ukiamini uzoefu utakuja tu kadri mvi zinavyoongezeka.
.
Hii inasababisha watu wengine kuwaamini watu wakubwa kuliko wao wakati hawana uzoefu wowote. Kuwaona wao ndo kungwi sababu tu wamaeishi muda mrefu.
.
Umri sio kielelezo cha ujuzi, bali waheshimu. Wametangulia kuliona jua.
.
Chukua hatua sasa ya kile kitu unachotaka kufanya/ kukijua/ kukipata.

Bila kuhofia utaharibu, sababu kuharibu maana yake ni kupata uzoefu sasa umejua nini usifanye/ ukwepe/ wapi usiende.

Kuliko ungekaa ukisubiri kujua icho kitu kimiujiza wa muda.

“Ni muhimu kujipa muda lakini usiseme nina muda”.

Namaanisha usijiruhusu kubweteka ukiamini una muda mbeleni.
Bali jiruhusu kufanya juhudi na kusubiri matokeo kwa kujipa muda.

Uwe Na Amani Unapotafuta Uzoefu.
 
Nimeacha kupanga mipango badala yake ninafanya sipangi Tena,maana ukipanga Kuna uwezekano usifanye.
 
Back
Top Bottom