GE2025 Msemaji wa Polisi: Ukiziona tena gari zenye 'plate number SSH 2530' toa taarifa

GE2025 Msemaji wa Polisi: Ukiziona tena gari zenye 'plate number SSH 2530' toa taarifa

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

informer 06

Senior Member
Joined
May 11, 2024
Posts
122
Reaction score
111
Plates.jpg

Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini, David Misime amesema kwamba tayari Jeshi hilo limechua hatua kuhusu magari yaliyokuwa na namba za usajili SSH2530 ambapo amesema kwamba kwa sasa magari hayo hayataonekana.
b8d22669-5ec4-472a-9986-52453fade84b.jpeg

Amesema kwamba baadhi ya magari yenye namba hizo yamekamatwa huku akitoa wito kwa Wananchi watakaoziona gari zenye namba hizo kutoa taarifa kwa Jeshi la Polisi ili hatua ziweze kuchukua.

Amefafanua kuwa kama 'plate number' hazipo kwenye mfumo rasmi uliohalilishwa na Serikali hizo zinakuwa sio sahihi.

Hayo ameyasema leo Agost 29, 2025, katika mdahalo wa Kitaifa kuhusu usalama wa waandishi wa Habari kuelekea uchaguzi Mkuu 2025 ambao umewakutanisha waandishi wa habari na wadau wa vyombo vya habari.

Ikumbukwe kumekuwepo na mjadala katika mitandao ya kijamii hususani JamiiForums kuhusu uhalali wa gari zinazotomia namba hizo.

Pia soma
 
Kaka yangu yupo hapa tena yake ina zile plate namba za kijani na njano kama serikali zile 😁😁😁
 
Jeshi la Polisi nchini limeeleza kuwa limeshaanza kushughulikia wamiliki wa magari walioweka usajili wa namba SSH 25 30 kwani hazitambuliki kisheria

Kauli hiyo imetolewa Agosti 29.2025 jijini Dar es Salaam na Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini DCP David Misime wakati akijibu swali la Katibu wa Klabu ya Waandishi wa Habari mkoa wa Kilimanjaro (MECKI) Devis Minja aliyetaka kujuwa uhalali wa namba hizo na usalama wa wananchi, katika mdahalo wa kitaifa wa usalama wa waandishi wa habari

Soma pia: Nani anaratibu au kusajili haya magari yenye plate number mfanano zenye maandishi ya SSH? Tunajua athari zake?

Screenshot 2025-08-29 045344.png

DCP Misime amesema kuwa tayari changamoto hiyo imeshafanyiwa kazi na haionekani tena, 'tumeshalifanyia kazi natumaini huzioni, kwasababu hazipo katika mfumo ambao umehalalishwa kwahiyo ukiziona tena tupe taarifa tutazirukia mara moja na sheria itachukua mkondo wake"

Uwepo wa namba hizo SSH 25 30 umekuwa ukizua mjadala na baadhi ya watu kuhoji uhalali wake kutokana na kuwa mmiliki wa chombo cha moto anaweza kufanya matukio ya uvunjifu wa amani au kusababisha ajali na chombo chake kisiweze kutambulika huku namba hizo zikichafua taswira ya mtu

Mjadala huo wa kitaifa kuhusu usalama wa waandishi wa habari umeandaliwa na UTPC pamoja na wadau wengine, umefunguliwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania (IGP) Camilius Wambura katika ukumbi wa Umoja wa Mataifa (UN) jijini Dar es Salaam
 
Hii inchi ya kibogas sana nilitegemea aseme wamechukulia sheria,yaani mtu anaamka anajibandikia plate namba bandia halafu hafanywi lolote
 
1. Je walifunguliwa mashtaka kama wahalifu wengine?
2. Kesi zao zilisikilizwa kwenye mahakama zipi?
3. Na huku ilikuaje?
4. Je niwakina nani hao kwa majina?
Mbona naona maswali ni mengi kuliko majibu...🤔
 
Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini, David Misime amesema kwamba tayari Jeshi hilo limechua hatua kuhusu magari yaliyokuwa na namba za usajili SSH2530 ambapo amesema kwamba kwa sasa magari hayo hayataonekana.
View attachment 3457404
Amesema kwamba baadhi ya magari yenye namba hizo yamekamatwa huku akitoa wito kwa Wananchi watakaoziona gari zenye namba hizo kutoa taarifa kwa Jeshi la Polisi ili hatua ziweze kuchukua.

Amefafanua kuwa kama 'plate number' hazipo kwenye mfumo rasmi uliohalilishwa na Serikali hizo zinakuwa sio sahihi.

Hayo ameyasema leo Agost 29, 2025, katika mdahalo wa Kitaifa kuhusu usalama wa waandishi wa Habari kuelekea uchaguzi Mkuu 2025 ambao umewakutanisha waandishi wa habari na wadau wa vyombo vya habari.

Ikumbukwe kumekuwepo na mjadala katika mitandao ya kijamii hususani JamiiForums kuhusu uhalali wa gari zinazotomia namba hizo.
Nyoka kujing'ata mkia ngumu!
 
Back
Top Bottom