Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa acha Kula Bata Ikulu wakati Timu ya Kwenu Songea Maji Maji FC inateseka huko Temeke

MINOCYCLINE

JF-Expert Member
Apr 2, 2015
8,011
16,748
Huku ikitarajia Kucheza katika Ligi ya Championship Kesho ( Ijumaa ) dhidi ya Dar City FC Klabu Kongwe na ya Kihistoria ya Maji Maji FC kutoka Mkoani Ruvuma ( Songea ) alikoishi muda mrefu Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa imefukuzwa katika Hoteli waliyoifikia huko Temeke Bulyaga huku Wachezaji wao ( wake ) wakiwa hawajala Chakula mpaka muda hali iliyopa Unafuu wasafisha Vyoo wa hiyo Hoteli kwani Njemba hazijaenda Choo kwa muda sasa Kushusha Magogo yao.

Watani zangu Wangoni mmejazana mno hapa Mkoani Dar es Salaam mkiongozwa na Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa na Wengi Wenu mna Hela ( japo nyingi huwa mnazihongea Wanawake na Kunywea Pombe ) hebu jikusanyeni na mjichangishe Fedha na muwapelekee Ndugu zenu na Wachezaji wa Timu ya Maji Maji FC kutoka Mkoani Kwenu Ruvuma ( Songea ) ili Wale kwa Usiku huu na wapate Gesti / Loji ya Kulala kwani kuna kila dalili Usiku huu wakakosa sehemu ya Kulala na wakaishia kuwa Walinzi Shirikishi wa muda huko Temeke Bulyaga waliko na Kuwahakikishia Usalama wa Ulinzi Wananchi / Wakazi wa maeneo hayo kwa Usiku huu wa leo.

Kwa Mtanzania yoyote ( pamoja na Wangoni na wana Mkoa wa Ruvuma ) Wote mlioko hapa Mkoani Dar es Salaam na Mikoa mingine ukitaka Kutuma chochote Kitu ( Pesa ) kuisaidia Klabu ya Maji Maji FC tuma kwenda Namba hii ya Dada Catherine Philip 0652 005 109 na itafika huku ukipata sana Baraka nyingi kutoka kwa Mwenyezi Mungu.

Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa juzi nilikuona ukiwa na Kiherehere kuwapa Yanga SC Fedha zao za Ahadi ya Mama ( Rais Samia ) Shilingi Milioni 15 hivyo nakuomba hapo hapo ulipo Ikulu hebu muombe Boss wako ( Rais Samia ) msaada wa chochote Kitu ili uwasaidie Nduguzo wana Lizombe ( Ruvuma ) Klabu ya Maji Maji ambayo ina Historia Kubwa na ya Kipekee hapa Tanzania hasa ilipofanya vyema ikiwa chini ya Mkuu wa Mkoa Mchapakazi na Mwanamichezo Marehemu Lawrence Gama.

ONYO

Namba ya huyo Dada Catherine Philip itumike tu kwa Lengo la Kutuma Pesa na Kusaidia Klabu ya Maji Maji inayotaabika sasa huko Temeke Bulyaga iliko na siyo kwa mengine ( Kumtongoza ) kwani Mumewe ana Siku Mbili tu karudi kutoka Kumaliza Kozi ya Pili ( Kubwa ) ya Ukomandoo nchini Cuba baada ya ile ya awali kule 92KJ Morogoro Tanzania na pia huko nyuma ndiyo alikuwa Mkufunzi wa Combat Karate wa akina Bolo Yung, Van Dame na Rais wa Urusi Vladmir Putin hivyo Usithubutu na mwishowe ghafla tukaanza Kukuita Marehemu fulani.
 
  • Thanks
Reactions: K11
Naitwa Mino na siyo Genta sawa? Utanikera sasa hivi...!!!!!
🤣🤣🤣🤣.... Huna Baya Mkuu Genta, ishi sana!

Mimi ni Alumn wako, So nakujua vizuri kaka.. hata usitumie nguvu! Hapo ulipojibu tu ktk sentensi ya mwisho pametosha ku'conclude! Hivi enzi za Fawasco unazikumbuka?
 
Sasa ishu za Tisa mbili zinakujaje hapo? Alafu karate combat haipo kama ulivyosema wewe habari za kina van Damme
 
Kwa chuki zako na msemaji ukichangia wewe unatosha

Na kwa utapeli huo hantoboi nawambiaaaaa
 
Back
Top Bottom