Msekwa sikubaliani na wewe. Tunaweza kuwa na katiba inayozuia kuwa na viongozi wabovu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Msekwa sikubaliani na wewe. Tunaweza kuwa na katiba inayozuia kuwa na viongozi wabovu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Gosbertgoodluck, Jan 29, 2011.

 1. Gosbertgoodluck

  Gosbertgoodluck JF-Expert Member

  #1
  Jan 29, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,866
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  WanaJF,
  Kwa wale walifuatilia mdahalo wa Jmosi uliomhusisha Mzee Pius Msekwa watakumbuka hoja mojawapo ya mzee huyo ilikuwa ni kutenganisha kati ya katiba na utendaji. Mzee Msekwa anataka kutuaminisha kuwa kazi ya katiba ni kuwezesha vyombo kuundwa, basi. Kinachofuata baada ya hapo, siyo kazi ya katiba. Eti ni mambo ya utekelezaji ambayo ufanisi wake unategemea uadirifu wa wanaongoza vyombo hivyo. Kwa hiyo, kwa mtazamo wangu, angekuwa mzee huyu ana uwezo angekataa katakata kubadili katiba iliyo kwa imani kwamba vipengele vyake vingi bado ni relevant. Alitolea mfano wa tume ya maadili kwamba nayo imeundwa kwa mujibu wa katiba lakini maadili yapo palepale.

  Mimi binafsi naona huo ni mojawapo ya udhaifu wa katiba yetu ya sasa. Katiba lazima iende mbele zaidi. Isiishie kujenga mazingira ya chombo kuundwa (serikali, bunge na mahakama, n.k). Lazima iingie kwenye utendaji na ku-address masuala yanayotokana na utendaji. Na zaidi ya yote ianishe mfumo mzuri usiotiliwa shaka wa kupata viongozi wa ngazi zote kuanzia chini hadi juu. Ninachotaka kusema hapa ni kuwa, chini ya katiba mpya, wananchi wasiofaa kuwa viongozi wasiote hata ndoto ya kugombe uongozi.
   
 2. Dumelambegu

  Dumelambegu JF-Expert Member

  #2
  Jan 29, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 1,052
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Mkuu nakuunga mkono. Msekwa is misleading the public.
   
 3. M

  Mzee wa Usafi JF-Expert Member

  #3
  Jan 29, 2011
  Joined: Apr 16, 2008
  Messages: 634
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 45
  sasa wadau mlitarajia nini kutoka kwa makamu mwenyekkiti wa ccm Tanzania Bara? Yeye ni mmoja wapo wa wale watu 10 walioitunga hii katiba ambayo inampa ulaji yeye,chama chake na marafiki zao.......angekuwa hayupo madarakani angepigia upatu katiba mpya ila sasa ataendelea kutetea tu....wapo wengi mno katika ccm wenye mawazo kama yake
   
 4. Gurudumu

  Gurudumu JF-Expert Member

  #4
  Jan 29, 2011
  Joined: Feb 5, 2008
  Messages: 2,350
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Gosbert, heshima yako mkuu,

  niliufuatilia mdahalo wote. Kimsingi nilijifunza mambo kadhaa. Kwanza, nilimuonea mzee msekwa huruma kwa kitendo cha kukubali kuwa mzungumzaji mkuu kwenye ule mdahalo. Siyo tu hajui upana wa tatizo bali alithibitisha kwamba ccm imeparaganyika.

  Msekwa mwanzo alikataa katiba mpya katika staili ambayo nilitafsiri kwamba ni msimamo wa ccm. Alipobanwa akataka ajivue umakamu mwenyekiti kisha baadaye akakubali katiba mpya.

  Mwanzoni alikuwa na msimamo kwamba tume ya rais ni msimamo wa CC lakini baadaye akapanua wigo na hata kukaribisha mapendekezo kutoka kwa wadau.

  Mwanzoni alionekana kujaribu kuongea kwa authority kwamba yeye anajua vema muktadha na hitoria ya katiba yetu, baadaye alipobanwa na washiriki akapanic na kuwa mdogo

  mwanzoni aliongea kama vile anataka kutoa msimamo wa chama na serikali lakini alipoanza kupwaya na Zitto kumuokoa, akaonesha kwamba inawezekana ccm wala serikali hawajakuwa na msimamo thabiti

  kubwa kuliko yote nililojifunza ni kwamba mzee yusufu makamba alifanya vizuri sana kukataza wagombea wa ccm kushiriki midahalo wakati wa kampeni za Uchaguzi mkuu. Kimsingi, tangu baada ya Uchaguzi mkuu, sijamuona mwana ccm ambaye ameonesha ufahamu na uwezo wa kujibu hoja za wadau kwenye mdahalo. Fikra za ccm zimebaki karne iliyopita wakati wao wamevuka kuja karne hii
   
 5. Madela Wa- Madilu

  Madela Wa- Madilu JF-Expert Member

  #5
  Jan 29, 2011
  Joined: Mar 24, 2007
  Messages: 3,074
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  Mzee Msekwa ni Ganda la muwa la jana... ni chungu pekee ndiye hufanya karamu.
  Apumzike tu nimemsamehe.
   
 6. Madela Wa- Madilu

  Madela Wa- Madilu JF-Expert Member

  #6
  Jan 29, 2011
  Joined: Mar 24, 2007
  Messages: 3,074
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  Maelezo yako ni safi.

  Niliwahi kufuga mbwa 15 na kuwafundisha kushambulia.
  Walikuwa na nidhamu kwelikweli.
  Tatizo ni kwamba ukitoa Amri ya kushambulia uwe umejiandaa la sivyo unaweza kuleta madhara makubwa kwa mbwa wako mwenyewe kwani mashambulizi siku zote hayako synchronized.

  Uongozi wa CCM ni mithiri ya kundi la 2000 half trained dogs hawakawii kuumana mikia na kutiana ngeu wenyewe kwa wenyewe kila wakidhani wanashambulia  Labda Training yangu ilishindika kwa vile mimi ni Mbweha na wao ni mbwa???
   
 7. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #7
  Jan 29, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Kitaeleweka tu!
   
 8. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #8
  Jan 29, 2011
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  He is doing it on purpose, anajua kuwa tayari katiba yetu imefanya kazi hiyo. Tunatakiwa tumwambie Msekwa kuwa tunataka tuweke vipengele vya kuwafanya viongozi wawe accountable kwa waliopiga kura. katiba ya sasa inamruhusu mtu kuchaguliwa, kuzuga kwa miaka mitano akitaka anaondoka na akitaka anaendelea huku amejichotea kama milioni 500 hivi.

  Mimi napenda tuwe na kipengele cha kuwafanya wanaotoa ahadi wabanwe kisheria, bila kujali uwezo wao wa kutekeleza ahadi.

  Napenda tuwe na kipengele kitakachombana Rais afanye kazi asitalii tu, nje na ndani ya Tanzania, tuwe na vipengele vya kupima utendaji wake si lazima akae miaka yote mitano(mbunge na rais) halafu ndio tusubiri uchaguzi tena.

  Haya yanawezekana na Msekwa anajua wazi.
   
 9. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #9
  Jan 29, 2011
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,377
  Likes Received: 3,140
  Trophy Points: 280
  Kwa namna yoyote ile nataka katiba ambayo itaondoa kinga kwa rais..................tunataka kumshitaki kikwete kwa kukumbatia ufisadi ya yeye mwenyewe kujihusisha na ufisadi
   
 10. n

  nooresh Member

  #10
  Jan 29, 2011
  Joined: Mar 28, 2009
  Messages: 20
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Katiba mpya inahitajika zaidi ili kukidhi mahitaji ya wananchi kupata maendeleo haraka zaidi lakini pia kuwepo na mabadiliko ya tabia za viongo- waliopewa dhamana wasitumie kwa manufaa yao mfano wewe ni ceo wa tanroads halafu una approve projects zisizokuwa na tija kwa taifa bali zina manufaa kwako hapo huwezi ukalaumu katiba tu bali na tabia zibadilike
   
 11. Profesa

  Profesa JF-Expert Member

  #11
  Jan 29, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 902
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 45
  Katiba nzuri inaweka mifumo mizuri ya kiutawala na maadili husika! Mzee Msekwa was so vulnerable kiasi cha kuchakachuliwa na Zito Kabwe bila kujitambua akahama kabisa kwenye misimamo na position aliyokuwa ameanza nayo...
   
 12. c

  cray Senior Member

  #12
  Jan 29, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 172
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Msekwa amepitwa na wakati, hata ukiangalia umri wake tu, utaona kua hata akili itakua imechoka pia. Naomba umlinganishe kama babu yako alioko kijijini na mawazo yake. Yaani unamsikiliza afu unaachana nae.
   
 13. n

  nooresh Member

  #13
  Jan 29, 2011
  Joined: Mar 28, 2009
  Messages: 20
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Ndugu yangu hebu angalia kenya wamepata katiba mpya lakini wat happened politicians wamebadilika rangi hawataki kwenda icc na kitu cha pili je katiba yao mpya imebadilisha mawazo ya ukabila the answer is a big no ukiangalia ile famous triple k gathering together kamba kikuyu na kalenjin in form of kenyatta musyoka na ruto ganging up for next year election...wanasiasa wabadilike pia its a fact
   
 14. D

  Deo JF-Expert Member

  #14
  Jan 29, 2011
  Joined: Nov 10, 2008
  Messages: 1,193
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 145
  Huyu mzee msameheni bure, ndiye aliyeandika kitabu cha chama kushika hatamu "The Party Suprimacy", na baado yuko huko huko
   
Loading...