Msekwa na bbc | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Msekwa na bbc

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Milindi, Mar 14, 2010.

 1. M

  Milindi JF-Expert Member

  #1
  Mar 14, 2010
  Joined: Mar 3, 2009
  Messages: 1,210
  Likes Received: 369
  Trophy Points: 180
  Nimemsikiliza Msekwa akihojiwa na BBC(JUMAMOSI) kwa kweli inatia uchungu sana,Wana jamii ustaarabu wa kiafrika uko vipi????,Labda tunahitaji elimu kiasi gani ili kuwajibika na makosa ya wazi tunayoyatenda.Msekwa anasisitiza Mambo yote ya kifisadi yanayowaandama vigogo kuwa ni tuhuma tu,Hivyo hawawezi kuwasimamisha kazi zao mpaka ibainike kuwa ni kweli waliyatenda je hii ni halali??.Na nyie vigogo mtu unatuhumiwa mpaka aliyetoa hongo anakubali kuwa nilimpa fulani halafu bado mnakataa kwa kudai kuwa ni tuhuma tu.Kama ni tuhuma tu basi kaa pembeni tuhuma ikionekana ni ya uongo basi utarudi na nguvu mpya.Wabunge wanatuhumiwa kwa ufisadi na wao wanasema maamuzi yao yalibarikiwa na ikulu bado ikulu inakaa kimya na wabunge hao wanaenda bungeni na kusimama na kuchangia hoja AJABU GANI HII TZ.

  MUNGU IBARIKI TANZANIA.
   
 2. M

  MaMkwe JF-Expert Member

  #2
  Mar 14, 2010
  Joined: Sep 5, 2007
  Messages: 284
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Hayo ni mawazo yake. Kisheria mtuhumiwa bado si muhalifu mpaka itakapothibitika ametenda kosa. Aidha si sahihi kusema kuwa tuhuma ni uwongo bila kusema ukweli ni upi. Kwa mfano ukisikiliza CNN, SkyNews, BBC nk. Osama anatajwa kuwa ni mtuhumiwa wa ugaidi tu. Atakuwa gaidi sheria itakapothibisha uovu wake.
   
 3. Injinia

  Injinia JF-Expert Member

  #3
  Mar 14, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 850
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Sawa, lakini kiongozi wa ngazi yoyote anapokuwa chini ya uchunguzi hata kama tuhuma bado hazijathibitishwa anatakiwa asimame kwanza ili kupisha uchunguzi!!

  Acheni kulindana
   
 4. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #4
  Mar 14, 2010
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,692
  Trophy Points: 280
  Nadhani tunahitaji radical desicion hapa.kipindi hiki ndicho ambacho kingekua transition period ili kujihakikishia msingi imara wa maadili ya uongozi kwamba ukituhumiwa tu,unakaa pembeni kidogo.

  Ni kwamba tumekuwa tunawapa uongozi watu wasiojali mandate intergrity!
   
 5. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #5
  Mar 14, 2010
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Mkuu kama ingekuwa enzi ya Nyerere labda ujinga kama huu tungeweza kuuamini. Bw Msekwa hawezi kutufanya wajinga au hawezi kutufanya hatuoni kinachoendelea.

  Serikali ilileta mkaguzi wa mahesabu, alieleza wazi kabisa na akaonesha ni nani aliiba hela. wezi walioiba hela wamerudisha, wamekubali wenyewe kuwa waliiba.

  SFO/BAE juzi tu wamesema kweli kulikuwa na utapeli. Ma akaunti ya watu huko majuu mpaka namba zao zinajulikana.

  Richmond kila mtu anajua....

  Sasa leo anasema ni tuhuma tu, what does he mean. Ni kwamba hakuna hela zilizoibiwa? are we all fools?? NO WE ARE NOT.
   
 6. Janjaweed

  Janjaweed JF-Expert Member

  #6
  Mar 14, 2010
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 9,528
  Likes Received: 882
  Trophy Points: 280
  Msekwa anapigana na upepo
   
 7. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #7
  Mar 14, 2010
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,220
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Unategemea nini toka kwa watu wanaotegemea posho za chama kuishi?
   
 8. m

  mmakonde JF-Expert Member

  #8
  Mar 14, 2010
  Joined: Dec 26, 2009
  Messages: 967
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Msekwa ,na wengineo akina Malecela,Salmin ,Mwinyi nia yao ni kuwa na status quo.
  Msekwa anatakiwa alipe deni la mtoto wake yapata miaka 6 iliyopita huko Ufaransa.

  Juzi alikuwa London anagawa kadi za CCM kwa wababaishaji london.
  Tusitegemee hawa watu wataokoa nchi yetu.
   
 9. Kiby

  Kiby JF-Expert Member

  #9
  Mar 14, 2010
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 5,200
  Likes Received: 1,003
  Trophy Points: 280
  Huyu babu aache kuona waTz ni mazuzu. Msekwa labda atusaidie hivi wale wote wanaopandishwa kizimbani imeshadhibitika kwamba ni wahalifu? Jawabu ni hapana. Sasa hao watuhumiwa watasibitishwa na nini ikiwa wana hatia au la kama hawapelekwi mahakamani? Ruzuku ya chama ambacho ndicho kinatuhumiwa kwa wizi wote uliofanyika nchini imempofusha huyu babu. Ni wakuonea huruma.
   
Loading...