Salaam jf
Nimeshangazwa na style iliyotumika kufungia nyimbo ya Snura inayofahamika kama snail(video na audio), ambapo kabla ya kufungiwa kwake nyimbo hiyo ilikuwa sio maarufu sana katika mitandao na hata katika jamii lakini baada ya kufungiwa kwake na mamlaka husika nchini, sasa nyimbo hiyo imekuwa maarufu na inafuatiliwa na watu wengi kuliko ufuatiliaji wa vitu vingene. Utafiti mdogo nilioufanya katika jamii inaonyesha kuwa watu wengi wenye simu za mikononi zenye uwezo wa kucheza mafaili ya video, basi lazima utakuta faili la video la msanii huyo limo hii uhusisha wanafunzi wa vyuo vikuu, walimu, wanajeshi, maaskari, waingiza nyimbo katika simu, wanafunzi wa sekondari hasa shule za kata, huku ikiwaacha watu wa dini kunusurika na swala hilo. Na haya yote ushaidi upo. Licha ya serikali kutoa onyo kali dhidi ya mtu atakaekiuka maagizo yaliyotolewa na serikali kuhusu uchezwaji wa nyimbo hiyo.
kulikuwa hakuna sababu kwa serikali kuliweka katika jamii kwa mtindo wa media badala yake kufikisha kwa watu husika na kuliwacha na mwishowe kupotea lenyewe kulingana na mazingira. Lakini mambo yamekuwa ni kinyume yaani sasa hivi Nyimbo hii inaimbwa darasani laivu na imekuwa ni ajenda iliyobebwa na wanafunzi wote wa shule za sekondari za kata na wanafunzi kukata mauno. Natarajia haya hayatakiwi kutokea tena katika idara husika iliyohusika kutoa tamko la kuzuiwa kwa nyimbo sampuli hizi.