Msanii Sajuki Aanguka Jukwaani Arusha

Ndallo

JF-Expert Member
Oct 1, 2010
7,619
4,292
attachment.php

Mwigizaji wa filamu nchini, Sajuki alidondoka jukwaani juzi wakati akijaribu kuwasalimia mashabiki wake waliofurika kumtazama kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abedi, Arusha. Sajuki ambaye jina lake halisi ni JUMA Saidi Kilowoko alikua akisumbumbuliwa na matatizo ya kupungukiwa na damu na kulazimika kwenda kutibiwa nchini India.

Mwigizaji huyo alipanda jukwaani katika tamasha lililowahusisha wasanii wa filamu na muziki lakini ndoto yake ya kuwasalimia mashabiki wake haikuwezekana. Mara baada ya kukabidhiwa kipaza sauti Sajuki alitamka neno moja ''ahhh'' na kudondoka chini na wasanii wenzake walimsaidia kuinuka na kumuondoa jukwaani hapo.
 
Attachments

  • Sajuki.jpg
    Sajuki.jpg
    516 KB · Views: 1,824
Dah; bado afya yake haijaimarika,aupunzishe mwili wake hadi apone kabisa...,Nampa pole sana
 
du haya misha siyo kabisa, bora angepona kwanza ndio aanze mihangaiko.!
 
lile tamasha la arusha lilikua kwa ajili ya kukusanya pesa za kumpeleka india. anatakiwa apate m 28. so wasanii wenzake wa bongo movie wakakubali wawe wanazunguka naye mikoani ili apate hela.
Cha ajabu arusha wasanii wa bongo movie walimgeuka. yeye alipanga kufanya show jumapili lakini wasanii wa bongo movie wakaenda kufanya show jmos bila yeye kujua kitu kilicho mchanganya. uzuri wasanii wa mziki wa arusha waliamua kumpa kampani jumapili na hela yote kumpa yeye. so alipanda jukwaani akiwa amezidiwa. mia
 
lile tamasha la arusha lilikua kwa ajili ya kukusanya pesa za kumpeleka india. anatakiwa apate m 28. so wasanii wenzake wa bongo movie wakakubali wawe wanazunguka naye mikoani ili apate hela. Cha ajabu arusha wasanii wa bongo movie walimgeuka. yeye alipanga kufanya show jumapili lakini wasanii wa bongo movie wakaenda kufanya show jmos bila yeye kujua kitu kilicho mchanganya. uzuri wasanii wa mziki wa arusha waliamua kumpa kampani jumapili na hela yote kumpa yeye. so alipanda jukwaani akiwa amezidiwa. mia
watu wasaliti sana
 
lile tamasha la arusha lilikua kwa ajili ya kukusanya pesa za kumpeleka india. anatakiwa apate m 28. so wasanii wenzake wa bongo movie wakakubali wawe wanazunguka naye mikoani ili apate hela.
Cha ajabu arusha wasanii wa bongo movie walimgeuka. yeye alipanga kufanya show jumapili lakini wasanii wa bongo movie wakaenda kufanya show jmos bila yeye kujua kitu kilicho mchanganya. uzuri wasanii wa mziki wa arusha waliamua kumpa kampani jumapili na hela yote kumpa yeye. so alipanda jukwaani akiwa amezidiwa. mia

Wachana na mambo ya Mbon'go!
 
Wadau kwa maombi na sala zetu mbele za Mungu tuendelee kumuombea Sajuki Mungu ampe afya njema juzi alianguka jukwaani Arusha akijiandaa kuburudisha mashabiki wake Uwanja wa Sheikh Amri Abeid

attachment.php
 
Attachments

  • DSC03246[1].JPG
    DSC03246[1].JPG
    40.3 KB · Views: 1,001
  • DSC03245[1].JPG
    DSC03245[1].JPG
    47.8 KB · Views: 623
Ilitakiwa apumzike kidogo si ndo ametokea India tu juzi juzi hatakiwi kufanya kazi za kujichosha, pia nadhani akafanyiwe na maombi maana India tu haitoshi
 
mkuu wa kaya hamuoni huyu, huyu ndo anahitaji msaada zaidi kuliko yule teja wa kujitakia ray c, Mungu akupe nguvu sajuki.
 
Si waende kumuona JK kuliko kuzunguka nae mikoani wakati bado hajapona
 
lile tamasha la arusha lilikua kwa ajili ya kukusanya pesa za kumpeleka india. anatakiwa apate m 28. so wasanii wenzake wa bongo movie wakakubali wawe wanazunguka naye mikoani ili apate hela.
Cha ajabu arusha wasanii wa bongo movie walimgeuka. yeye alipanga kufanya show jumapili lakini wasanii wa bongo movie wakaenda kufanya show jmos bila yeye kujua kitu kilicho mchanganya. uzuri wasanii wa mziki wa arusha waliamua kumpa kampani jumapili na hela yote kumpa yeye. so alipanda jukwaani akiwa amezidiwa. mia

Akiripoti kutoka kusikojulikana, huyu ni figganigga wa Jamiiiiiiiiiiiiiiiiiiii Foraaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaam.

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
  • Thanks
Reactions: PhD
Wadau wa tasnia ya filamu nchini ni nini kimemkuta Sajuki tena? Je ni mizunguko anayoifanya mikoani ndo imepelekea kuanguka ghafla au lipi jingine?
 
Tamasha la bongo movie Arusha ndyo limemfanya adondoke maana na yy alipanga kufanya tamasha halafu bongo movie wakamwambia Sajuki ahairimishe maana na wao wanatamasha.
 
Sajuki kwa sasa kalazwa Hospitali ya Muhimbili Mwaisela 1,
hali yake ni mbaya sana na anapumulia mashine...
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom