Msanii mwingine Bongo Movie afariki

kimpe

JF-Expert Member
Jan 26, 2012
911
861
TASNIA ya filamu Bongo imepata pigo tena baada ya msanii aliyekuwa akichipukia kwa kasi, Patrick August ‘Bryton' kufariki dunia kwa ajali mbaya ya pikipiki.Akizungumza na paparazi wetu, Mwenyekiti wa Sherehe na Maafa kwa wasanii wa Wilaya ya Kinondoni, Masoud Kaftany alisema Bryton alipata ajali usiku wa kuamkia Jumapili maeneo ya Tabata - Relini wakati akirejea kwao maeneo ya Tabata - Kinyerezi."Alikuwa akiendesha mwenyewe pikipiki, akavaana uso kwa uso na gari.
Ilikuwa ni ajali mbaya sana kwani marehemu alipasuka vibaya kichwa hali iliyosababisha damu nyingi kuvuja na kusababisha kifo chake," alisema Kaftany.

Baadhi ya sinema alizoigiza enzi za uhai wake ni pamoja na Muuza Genge na Mapenzi ya Fukara iliyomshirikisha Kulwa Kikumba ‘Dude' na wasanii wengine. Mwili wa marehemu Bryton ulisafirishwa jana (Jumanne) kwenda Rombo, mkoani Kilimanjaro kwa ajili ya mazishi yaliyotarajiwa kufanyikwa leo Jumatano.
Source: GPL
attachment.php
 
Attachments

  • IMG20140803WA00021.jpg
    IMG20140803WA00021.jpg
    53.4 KB · Views: 3,161
Huyu alikuwa muendesha bodaboda pale kimanga..haya mambo ya kuwa msanii yametoka wapi?

Kumbe unamjua, hata mimi nimeshangaa sana.
Huyu jamaa alikuwa bodaboda na alikuwa na genge hapa jirani na ABC pub. Mara ya mwisho alikuwa anauza mdogo wake na tangu aondoke, hata wiki mbili hazikuisha na yeye ndio ameaga dunia.
Nyepesi za hapa kitaa zinasema hivi huyu mdodgo wake ana zaidi ya miaka nane tangu aletwe na kaka yake huyu.
Na tangu atoke Rombo hajawahi kurudi na hata alipoomba kurudi kusalimia tu, alikataliwa.
Kwa hiyo maisha yake yote tangu anafika yamekuwa ni ya hapo Gengeni huku yeye na shemeji yetu wakiwa wamepanga maeneo ya Kimanga hapahapa.
Nyepesi hazikuishia hapo, zinasema eti dogo hata nguo alikuwa hanunuliwi licha ya kukesha gengeni kwa muda wote huo. Akitaka nguo alikuwa akirushiwa tu (used pambas) alizokuwa akivaa sharo huyu ambaye muda wote alionekana bring bring full macheni nk.
Ile siku ya tukio alimwaga mkewe kwamba anaenda kuchukua mzigo wa genge kule Mabibo na kwa bahati mbaya tunaamka asubuhi tunasikia mauti yameshamkuta kabla hata ya kuchukua mzigo, kwa hiyo hapa hela ya mzigo ilipotelea pale pale alipopata ajali.
Mdogo wake kwenda Rombo ni kama alikuwa anaenda kutoa taarifa za msiba tu, kwa sababu amekaa miaka zaidi ya nane hajaenda, na anapoenda tu, braza anaaga dunia nyuma.
R.I.P
 
Well explained...kumbe wewe ni jirani yangu? Nakuwaga hapo ABC jumamosi naponyeza vitu laini
 
mnaomjua ni majirani zangu pia mie nimeshangaa kuckia mangi mwenzangu naye msanii. asee weekend nakuwaga hapa anti stress natoa stress kidogo karbuni wakuu
 
Kumbe unamjua, hata mimi nimeshangaa sana.
Huyu jamaa alikuwa bodaboda na alikuwa na genge hapa jirani na ABC pub. Mara ya mwisho alikuwa anauza mdogo wake na tangu aondoke, hata wiki mbili hazikuisha na yeye ndio ameaga dunia.
Nyepesi za hapa kitaa zinasema hivi huyu mdodgo wake ana zaidi ya miaka nane tangu aletwe na kaka yake huyu.
Na tangu atoke Rombo hajawahi kurudi na hata alipoomba kurudi kusalimia tu, alikataliwa.
Kwa hiyo maisha yake yote tangu anafika yamekuwa ni ya hapo Gengeni huku yeye na shemeji yetu wakiwa wamepanga maeneo ya Kimanga hapahapa.
Nyepesi hazikuishia hapo, zinasema eti dogo hata nguo alikuwa hanunuliwi licha ya kukesha gengeni kwa muda wote huo. Akitaka nguo alikuwa akirushiwa tu (used pambas) alizokuwa akivaa sharo huyu ambaye muda wote alionekana bring bring full macheni nk.
Ile siku ya tukio alimwaga mkewe kwamba anaenda kuchukua mzigo wa genge kule Mabibo na kwa bahati mbaya tunaamka asubuhi tunasikia mauti yameshamkuta kabla hata ya kuchukua mzigo, kwa hiyo hapa hela ya mzigo ilipotelea pale pale alipopata ajali.
Mdogo wake kwenda Rombo ni kama alikuwa anaenda kutoa taarifa za msiba tu, kwa sababu amekaa miaka zaidi ya nane hajaenda, na anapoenda tu, braza anaaga dunia nyuma.
R.I.P

This is JF! kimsingi wewe inaonesha ni jirani yake tena ni mtu wa mtaani hapo hapo alipopanga Marehemu! mwe!
 
Nitakutafuta jumapili, huwa napatikana mitaa ya hapa Antsress ila hasa mida ya saa moja usiku.
 
Huyu alikuwa muendesha bodaboda pale kimanga..haya mambo ya kuwa msanii yametoka wapi?

Rest In Peace Bryton.

Sioni mantiki ya kupingana kuwa marehemu alikuwa msaniiau la, kwa kuwa tu alikuwa muendesha bodaboda.

Haswa mikoani, asilimia tisini na tano kama sio mia ni lazima msanii awe na shughuli mbadala, na wanajishughulisha na sanaa baada ya kazi zao walizoajiriwa au kujiajiri...otherwise wataendesha vipi maisha kabla "hawajatoka" ili hiyo sanaa iweze kumuajiri full time ?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom