Msanii Joseph Haule (Prof. Jay) ajiunga CHADEMA

Assignment ya kwanza: tunga nyimbo za uhamasishaji tena ziwe nzuri zipiku zile za analojia za Komba na TOT yake!
 
karibu sana PROJ JAY! Karibu kwenye mapambano mazee!

Pipooooooz!

kila mwenye akili safi anajiunga CDMA .Watakuja wengi tu.Hongera ndg Haule kwa kutafuta ukweli.
 
Hiyo imekaa vizuri sana na ukiona kijana yeyote anashabikia MACCM ama akili zake hazina akili au anafaidi ufisadi kwa namna moja au nyingine. Wengine hatuna uwezo wa nje wa kisiasa lakini uwezo wa ndani wa mipango, support ya hela na mawazo tutayatoa na yatasaida sana kuleta mageuzi tutakayo
 
Nchimbi au Jenista Mhagama tumbo joto mzigo utakuwa unagonga kyupi nakurudi 2015 bye bye mjengoni waanze kuaga mapema
 
Big up big dadiiii, leo umehit headlines za blogs bongo nzima.Tukio lako la kujiunga chadema ni mshtuko kwa ccm,na wahafidhina wote.Tukio hili ni kama mshtuko walioupata watu pindi waliposikia fergusion kajiuzuru kufundisha mpira, mwambie team ANACONDA tunamsubiri na yeye
 
Mi nilijua tu kwamba upo huku siku nyingi ila ukawa bado hujajitokeza hadharani. Karibu sana. Wapo wasanii wengi, wafanyabiashara wengi, wasomi wengi na Viongozi kibao tu wa CCM ambao bado hawajaweka wazi kuwa wako CHADEMA, it is matter of time.
 
 
CHADEMA mnazidi kuongeza majanga; Joseph Haule hana tofauti na Joseph Mbilinyi kwa mipasho isiyokuwa na hekima
Kati ya watu walioleta mapinduzi ya Hip hip na kukubalika na wazee mpaka watoto ni Joseph Haule kama huja wahi kusikiliza nyimbo zake kazi tafute mama...
 

Kuna kipindi alitangaza kugombea ubunge lakini ghafla akabadili mawazo yake.
 
hongera J wa mitulinga a.k.a mti mkavu.
pande zote utakwenda lakini bongo ndio home.!!!

namsubiri Jide a.k.a komando au binti machozi.!!
 
Kutumbuiza ccm harakati CDM. naona kama Jide yuko njiani vile!!?
 
'wanasema mi nakunywa weee nalala kwenye baa, wanasema mi ni bingwa la ngono kwenye mitaa, . . . . ! Karibu sana
 
kwani chadema ni chama cha wasanii? lakini kama kijana anauhuru wa kufanya hivyo na bado jd naye ataenda kesho au kesho kutwa wote wanafahamika kwa hiyo chadema sasa hivi ni miziki tu hamna kazi tena.
 
Kama unajua jinsi ya kutafuta hela bila kuitegemea CCM karibu sana CHADEMA,ila kama wewe ni kilaza na huwezi kujituma kaa huko huko CCM!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…