MSANII G SOLO - MUDA WA VITENDO

MSANII G SOLO - MUDA WA VITENDO

Joined
Nov 8, 2018
Posts
29
Reaction score
31
🔥 JE, HIP HOP YA ZAMANI ILIKUWA SAUTI YA JAMII?

Kuna kipindi Hip Hop haikuwa burudani pekee, bali ilikuwa pia kioo cha jamii. Wasanii walitumia kalamu zao kuzungumzia maisha ya wananchi, siasa, uchumi, rushwa, elimu, ajira na changamoto mbalimbali zilizokuwa zikiikabili Tanzania.

Leo tunakuletea lyrics hizi zenye ujumbe mzito wa kijamii. Msanii anagusa mambo mbalimbali na kuuliza maswali ambayo bado yanaweza kutufanya tutafakari mpaka leo.

G SOLO - MUDA WA VITENDO
STUDIO - KAMA KAWA RECORD
PRODUCER - GEOF MASTER...

🎤 VERSE 1

Fake Emcees wanaongea upumbavu kwenye hii jamii/
Sera zao wote kavu kujenga u-enemy/
Wanasahau matatizo yanayowakabili/
Wakidhani wameshafika, hutofika kwa kazi hii/
Huku wananchi wanatamani kuongea na President/
Wamueleze matatizo wayaonayo kwenye Government/
Cheki kodi inavyopanda na jua lachoma/
Mishahara bado hafifu wafanyakazi wanagoma/
Elimu ya juu bila mkopo ni nani atasoma/
Huku taaluma nayo inashuka muda unayoyoma/
Kuongea ni uhuru, ukweli ni nuru/
Japo unazuru mafisadi wana fedha mpaka wanakufuru/
Sio EPA, Richmond mpaka na TAKUKURU/
Mwananchi ameshachoka na mzigo wa ushuru..

🎶 CHORUS

Matatizo bado mengi/
Tofauti tofauti/
Kwetu shida, kwenu raha/
No doubt doubt/
Kwenye ulingo nawapiga knock out/
Knock out/
Huu ni muda wa vitendo/
Ku-shout si shout..

Matatizo bado mengi/
Tofauti tofauti/
Kwetu shida, kwenu raha/
No doubt doubt/
Kwenye ulingo nawapiga knock out/
Knock out/
Huu ni muda wa vitendo/
Ku-shout si shout..

🎤 VERSE 2

Fedheha kwa Taifa zima pamoja na Serikali/
Viongozi wana siri kali za kusaini mikataba japo wanajua dosari/
Hii ni hatari..!!/
Wananchi vijijini na mijini magonjwa na njaa kali/
Wastaafu wa East Africa ni nani anaowajali/
Na vipi madaktari mbona sijawahi kusikia au kuona migomo ya maaskari/
Usafiri kwa mwanafunzi bado jua la utosi/
Dhiki mikosi..!!/
Gari za fedha nyingi wanazomiliki mabosi/
Ni aibu kwa shule kufungwa kwa ukosefu wa misosi/
Hakuna kitu migodini, chembe chembe za madini/
Kizazi kitarithi nini zaidi ya dhiki, umaskini/
Bidhaa feki zinaingia kwa sera za ubabahishaji/
Na ukoloni unaendelea kwa jina la uwekezaji/
Ni rushwa itikadi, vyama vya siasa ni miradi/
Alaumiwe Rais au dalali issue ya Rada/
Hata kesi ya Balali haina utofauti na ile ya chavda/
Ufisadi unaendelea kuisha lini sijui labda/
Pale Mungu atakapoamuru viongozi wenye mioyo safi/
Mungu wao wanamshukuru, walitamani kuingia Ikulu mmoja mmoja anajiuzulu/
Pongezi kwako Jakaya kwa kuwatolea uvivu viongozi wote wabaya/
Waliohujumu nchi hii kwa tamaa zao mbaya/
*** *** ***/
Sauti ya haki/
Yo..!!

🎶 CHORUS

Matatizo bado mengi/
Tofauti tofauti/
Kwetu shida, kwenu raha/
No doubt doubt/
Kwenye ulingo nawapiga knock out/
Knock out/
Huu ni muda wa vitendo/
Ku-shout sishout.. si shout Out

Matatizo bado mengi/
Tofauti tofauti/
Kwetu shida, kwenu raha/
No doubt doubt/
Kwenye ulingo nawapiga knock out/
Knock out/
Huu ni muda wa vitendo/
Ku-shout si shout..

Mdau wa Ukwaju wa kitambo endeleeni na next verse...

🤔 TAFAKURI KWA WADAU WA HIP HOP

Kwa mtazamo wako, ujumbe mkuu wa wimbo huu ulikuwa upi?

Je, matatizo yaliyotajwa kwenye lyrics hizi bado yapo kwenye jamii ya Tanzania leo?

“Kuongea ni uhuru, ukweli ni nuru” — je, Hip Hop ya Tanzania bado ina nafasi ya kusema ukweli bila kuogopa?

Kama wimbo huu ungeandikwa mwaka 2026, ni tatizo gani ungependa msanii aliongeze kwenye lyrics?

🔥 Na mwisho, ni mstari gani kwenye wimbo huu umekugusa zaidi, na kwa nini?

#UkwajuWaKitambo #Tunakurudisha #OldSkoolHipHop #TanzaniaHipHop #BongoFleva

Ukwaju wa kitambo
0767 542 202
 
Back
Top Bottom