BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,789
- 288,014
Kutoka Gazeti la MwanaHALISI la August 26, 2009
Kutoka Gazeti la Mwananchi la Sept 15, 2009Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, John Chiligati aliwaambia waandishi wa habari baada ya kikao cha NEC, "Tumesema inatosha. Hapa tulipofika tusiendelee mbele. Wanaoropoka ovyo ni walevi na tumeona kuna kundi dogo ambalo linajiona kama ni wateule wa kuzungumzia ufisadi."
Kauli hii ya CCM ililenga wabunge jasiri ambao wamekuwa wakiikosoa serikali, miswada yake na kutaka watuhumiwa wa ufisadi kuchukuliwa hatua.
Tutaona na kusikia mengi sana yaliyojaa usanii wa hali ya juu katika safari hii ya kuelekea October, 2010 kutoka kwa viongozi mbali mbali ndani ya Chama Cha Mafisadi ili kuomba KULA (isomeke Kura) kutoka kwa Watanzania.Jana, Chiligati alikuwa ni mtu mwenye kuunga mkono kikundi hicho wakati Mwananchi ilipotaka maoni yake kuhusu wabunge hao ambao wanaonekana kukaidi maazimio ya Nec, huku wakitamba kuwa hakuna anayeweza kuwafunga mdomo.
"CCM haina ugomvi na wabunge wake wala mtu yeyote anayejitoa mhanga kupinga ama kupambana na mafisadi," alisema Chiligati ambaye pia ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
"Msimamo wa chama chetu ni kwamba rushwa ni adui wa haki, usichukue, kuomba wala kutoa rushwa, huo ndio wimbo wa kila mwana-CCM.
"Hatuna ugomvi wala uadui na mtu yeyote anayepambana na rushwa, ufisadi, uporaji, wizi na ujambazi. Huo ndio msimamo wa CCM."
Last edited: