Msamiati wa Nyakati na Saa

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,986
Msamiati wa Nyakati na Saa
Siku za Juma
Juma au wiki moja huwa na siku saba. Yafuatayo ni majina ya siku za juma. Kwa kuwa asili yake ni Kiarabu na Kiislamu, Jumamosi ndiyo siku ya kwanza ya wiki; nayo Ijumaa ndiyo siku ya saba.
SIKU YA JUMAKIINGEREZA
JumatatuMonday
JumanneTuesday
JumatanoWednesday
AlhamisiThursday
IjumaaFriday
JumamosiSaturday
JumapiliSunday
Siku Zikilinganishwa na Leo
Haya ni majina tunayotumia kurejelea siku zinazokaribiana na leo.
SIKUMAELEZOMFANO
juzisiku iliyotangulia janaikiwa leo ni Jumatano, juzi ilikuwa Jumatatu.
janasiku iliyotangulia leoikiwa leo ni Jumatano, jana ilikuwa Jumanne.
leosiku ambayo tuko sasa hivi
keshosiku inayofuataIkiwa leo ni Jumatano, kesho itakuwa Alhamisi.
kesho kutwasiku itakayokuja baada ya keshoikiwa leo ni Jumatano, kesho kutwa itakuwa Ijumaa.
mtondogoosiku itakayokuja baada ya kesho kesho kutwa. siku tatu kutoka leoikiwa leo ni Jumatano, kesho kutwa itakuwa Jumamosi.
Miezi ya Mwaka
Jedwali lifuatalo linaonyesha majina ya miezi katika mwaka, na idadi ya siku katika kila mwezi.
#JINAMWEZI WA:SIKU
1Januarikwanza31
2Februaripili28
3Machitatu31
4Aprilinne30
5Meitano31
6Junisita30
7Julaisaba31
8Agostinane31
9Septembatisa30
10Oktobakumi31
11Novembakumi na moja30
12Disembakumi na mbili31
Masaa ya Siku
Yafuatayo ni mafungu ya masaa au nyakati mbalimbali za siku.
WAKATIMAELEZOMASAA
mchanawakati wa siku wenye jua. kutoka saa kumi na mbili asubuhi hadi saa moja jioni hivi6am - 7pm
usikuwakati wa siku usiokuwa na jua. kutoka saa moja jioni hadi saa kumi na mbili siku inayofuatia7pm - 6am
alfajirikati ya saa tisa na saa kumi na moja asubuhi3am - 5am
macheosaa kumi na moja hadi saa kumi na mbili hivi jua linapochomoza3am - 5am
asubuhikutoka saa kumi na mbili hadi saa sita za mchana6am - 12pm
adhuhurisaa sita za mchana hadi saa nane12pm - 2pm
alasirisaa nane hadi saa kumi na moja hivi2pm - 5pm
jionisaa kumi na moja hadi saa moja jioni5pm - 6pm
machweo/magharibisaa kumi na mbili hadi saa moja jioni; jua linapotua6pm - 7pm
usiku mchangakati ya saa moja jioni na saa sita za usiku7pm - 12am
usiku wa mananekutoka saa sita za usiku hadi alfajiri12am - 3am
Kusoma Saa
Tunaweza kusoma saa tukitumia:
Mfumo wa Kiswahili
katika mfumo wa Kiswahili/Kibantu, siku huanza saa kumi na mbili asubuhi. Kwa hivyo, saa moja ya asubuhi inakuwa ndiyo saa ya kwanza(1) ya siku.
Mfano:
  1. 5:00 asubuhi ⇒ saa tano kamili asubuhi
  2. 9:15 usiku ⇒ saa tisa na robo usiku.
  3. 11:30 jioni ⇒ saa kumi na moja unusu jioni
  4. 2:45 alasiri ⇒ saa tatu kasorobo au saa mbili na dakika arubaini na tano alasiri
  5. 10:23 alfajiri ⇒ saa kumi na dakika ishirini na tatu alfajiri
Mfumo wa Kimataifa/Kiingereza
Huu ndio mfumo unaokubalika kirasmi katika mataifa na lugha mbalimbali. Kulingana na mfumo huu, siku huanza saa sita za usiku. Hivyo basi, saa saba ya usiku inakuwa saa ya kwanza(1) ya siku.
Mfano:
  1. 6:00 macheo ⇒ saa kumi na mbili asubuhi kamili macheo
  2. 12:15 adhuhuri ⇒ saa sita na robo adhuhuri.
  3. 3:30 alasiri ⇒ saa tisa na nusu alasiri
  4. 6:45 jioni ⇒ saa moja kasorobo au saa kumi na mbili na dakika arubaini na tano jioni
  5. 11:08 usiku ⇒ saa tano na dakika nane usiku

 
Back
Top Bottom