God bell
JF-Expert Member
- May 13, 2011
- 590
- 211
Ndugu wana MMU nawasalimuni wote, poleni kwa majukumu. Nakuja na ujumbe huu jioni hii. Nawaombeni msamaha wale wote nilowakosea aidha kuwaudhi au kwa kukwaruzana katika nyuzi mbalimbali nilipokuwa nachangia au Kupeana ahadi katika PM ambazo baadae hazikuzaa mafanikio. Kuna kipindi nilimjibu mtu hapa baada ya kuniudhi nikamjibu vibaya akanisababishia BAN. Wote hao nawaomba msamaha. Ni hayo tu ili niweze kutua mzigo kwenye roho yangu níishi kiroho safi. Asanteni. Mwenye maoni anakaribishwa.