Kwamba MSAMAHA WA RAIS KWA WAFUNGWA ndio chanzo cha matukio makubwa ya UJAMBAZI ulioanza tena kwa kasi ya ajabu.
Hali hii inasababishwa na wakuu wa MAGEREZA KUACHIA WAFUNGWA AMBAO HAWASTAHILI MSAMAHA.
Pia kuna kasoro kubwa ktk msamaha huo kwani ni wa jumla,kiasi inakuwa ngumu kujua nani ni nani.
Inashauriwa msamaha usiwe wa jumla na badala yake wakuu wa magereza wawe waadilifu katika kuorodhesha wanao stahili msamaha kwa kushirikisha taarifa ya KIPOLISI NA MWENENDO WA MFUNGWA GEREZANI.
Mfumo wa sheria uwe mzuri/usiwe na upendeleo na kwamba anayefungwa gerezani,asipewe msamaha bali ktk mazingira maalum kama ugonjwa ambapo uhakika upo hana nguvu za kufanya kazi tena.
Mfumo wa sheria ukiwa mzuri na polisi wakifanya kazi zao kwa makini matatizo haya MSAMAHA HAYATOKUWEPO.Mfano kuna tetesi kuwa ktk GEREZA LA KILIMWANGA LILILO MKOANI ARUSHA ni kituo cha wafungwa wa ujambazi kukutana na kupanga mikakati ya ujambazi,kivip?KUNA JAMBAZI MOJA SUGU AMBALO NI "planner"(ambaye ni mfungwa,)hivyo majambazi ambayo hayajakamatwa na kufungwa kwa ujambazi yanajaribu au yanafanya uhalifu mwingine ambao adhabu yake ni ndogo na kesi inaenda haraka haraka na kuhukumiwa kutumikia kifungo labda miezi sita au mwaka ktk GEREZA HILO.WAKISHA PELEKWA HAPO HUKUTANA NA PLANA NA KUMPA MPANGO WA KWENDA KUPORA SEHEMU FLANI,HIVYO YEYE ANATOA USHAURI WA NAMNA YA KUKAMILISHA ZOEZI LAO HILO.
Ikumbukwe kuwa hawa wanaotafuta adhabu ndogo ili kupanga mikakati yao,hufanya hivyo karibu na kipindi cha msamaha wa RAIS kwani wanajua 9.12 na/au 26.4 kunakuwa na msamaha na hivyo hata adhabu ya miezi sita au mwaka hawaitumikii yote.