Msamaha wa rais na ujambazi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Msamaha wa rais na ujambazi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Shaycas, May 9, 2009.

 1. Shaycas

  Shaycas JF-Expert Member

  #1
  May 9, 2009
  Joined: Feb 13, 2009
  Messages: 899
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  Kwamba MSAMAHA WA RAIS KWA WAFUNGWA ndio chanzo cha matukio makubwa ya UJAMBAZI ulioanza tena kwa kasi ya ajabu.
  Hali hii inasababishwa na wakuu wa MAGEREZA KUACHIA WAFUNGWA AMBAO HAWASTAHILI MSAMAHA.
  Pia kuna kasoro kubwa ktk msamaha huo kwani ni wa jumla,kiasi inakuwa ngumu kujua nani ni nani.
  Inashauriwa msamaha usiwe wa jumla na badala yake wakuu wa magereza wawe waadilifu katika kuorodhesha wanao stahili msamaha kwa kushirikisha taarifa ya KIPOLISI NA MWENENDO WA MFUNGWA GEREZANI.
  Mfumo wa sheria uwe mzuri/usiwe na upendeleo na kwamba anayefungwa gerezani,asipewe msamaha bali ktk mazingira maalum kama ugonjwa ambapo uhakika upo hana nguvu za kufanya kazi tena.
  Mfumo wa sheria ukiwa mzuri na polisi wakifanya kazi zao kwa makini matatizo haya MSAMAHA HAYATOKUWEPO.Mfano kuna tetesi kuwa ktk GEREZA LA KILIMWANGA LILILO MKOANI ARUSHA ni kituo cha wafungwa wa ujambazi kukutana na kupanga mikakati ya ujambazi,kivip?KUNA JAMBAZI MOJA SUGU AMBALO NI "planner"(ambaye ni mfungwa,)hivyo majambazi ambayo hayajakamatwa na kufungwa kwa ujambazi yanajaribu au yanafanya uhalifu mwingine ambao adhabu yake ni ndogo na kesi inaenda haraka haraka na kuhukumiwa kutumikia kifungo labda miezi sita au mwaka ktk GEREZA HILO.WAKISHA PELEKWA HAPO HUKUTANA NA PLANA NA KUMPA MPANGO WA KWENDA KUPORA SEHEMU FLANI,HIVYO YEYE ANATOA USHAURI WA NAMNA YA KUKAMILISHA ZOEZI LAO HILO.
  Ikumbukwe kuwa hawa wanaotafuta adhabu ndogo ili kupanga mikakati yao,hufanya hivyo karibu na kipindi cha msamaha wa RAIS kwani wanajua 9.12 na/au 26.4 kunakuwa na msamaha na hivyo hata adhabu ya miezi sita au mwaka hawaitumikii yote.
   
 2. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #2
  May 9, 2009
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Kwa kifupi msamaha wa rais ufutwe!
  Au kuwe na parol body? Ipo hiyo? Alafu wao ndo wanapendekeza majina ya watu wastahiliyo kusamehewa!
   
 3. Mshiiri

  Mshiiri JF-Expert Member

  #3
  May 9, 2009
  Joined: Jun 16, 2008
  Messages: 1,893
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 145
  Kila jambo lapaswa kufanywa kwa hekima huwezi amka tu na kusema wafungwa hawa na hawa inje. Nadhani mjomba ana kazi kubwa ya kufanya. Tathmini ya nani apewe msamaha isiwe tu aina ya adhabu bali mwenendo wa tabia wa mfungwa husika. Jela si mbaya ila ni serikali yetu inafanya ziwe mbaya. Jela ni mtambo wa kurekebisha tabia na akili; kama ilivyo shule, vyuo, makanisa, hospitali ya mirembe au popote wawapo watu wenye tabia mbalimbali na lengo ikiwa kuwabadilisha tabia watu wawe na tabia ambayo ni wastani kwa jamii. Kama tabia ya mtu inakuwa sugu kubaidilika basi asipewe msamaha. Na tena ingekuwa ni uamuzi wangu wa busara wafungwa wote wanaoachiwa wangepelekwa katika mazingira ambayo ni wazi kama wami nk. wakaanzisha kijiji chao na wakaendelea na kazi waliyokifunza jela na kujenga nchi badala ya kuwaachia tu holela na kurudia kubomoa nchi. Wezi hawa hawajengi nchi why sasa unawapatia msamaha. Anyway labda wezi pia wana thamani nchini kwa makundi fulani ya watu.
   
 4. Shaycas

  Shaycas JF-Expert Member

  #4
  May 10, 2009
  Joined: Feb 13, 2009
  Messages: 899
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  Kwani ni lazima MSAMAHA UWEPO?
   
Loading...