msamaha wa kodi za magari (tax exemption)

Status
Not open for further replies.

KASRI

Member
May 2, 2009
93
22
Wasalaam wanaJF
Naomba kwa anayefahamu anisaidie kufahamu jinsi kodi inavyokokotolewa endapo nitanunua gari lililokuwa na msamaha wa kodi (Tax exemption) ambalo liliingizwa nchini TZ mwaka 2000. Mwenye nalo (raia wa kigeni) analiuza kwa USD 15,000. Ni Landcruiser Prado la 1998. Naomba msaada wa kuelimishwa.natanguliza shukrani.
 
Hiyo bei kwa gari ya mwaka 98 unalaliwa hapo. Gari hiyo ina zaidi ya miaka 13 halafu iuzwe for $ 15K??? Mkuu that's not a good deal.
 
I understand wewe huna exemption ila gari ni exempted. OK here we go.

1. Utatakiwa kulipa VAT 18%, Import duty 25% na transfer 1% na mwisho Tshs 60,000/= kwa ajili ya registration

2. All the above will be chargesd basing on current value in which you calculate depreciation of 20% per annum (Huyo bwana amesha kaa miaka mingapi?

Mfano:
Gari ni Dola 15,000 na huyo bwana amekaa miaka miwili basi una deduct 40% of $15,000 ambayo ni $6000. Then value itakayo baki uta add 25%, 18% na 1%.

Kwa faida ya wengine gari kama hii unge import ungelipa kama ifuatavyo.

1. Import duty 25%
2. VAT 20%
3. Dumping fee 20%
4. Excise duty 10%
6. Destination Inspection Fee (DI) 1.2%
7. Registration Tshs 360,000
8. Agency fee $300

Na ole wako kama document hazijakamilika ndo utajua shughuli hapo boarder kila mtu atataka kupaua nyumba yake kupitia mgongo wako
 
Kwa ufafanuzi zaidi ni kuwa:
FOB + Freight + Insurance = CIF, Ungelipa kama ifuatavyo:
1. Import duty 25% of CIF
2. VAT 20% of (CIF + 1 above)
3. Dumping fee 20% of (CIF + 1 and 2 above) if the car aged more than 10 yrs
4. Excise duty 10% of (CIF + 1, 2 and 3 above) or 5% of (CIF + 1, 2 and 3 above) if cc more than 1500, equal or less than 1500 respectively
6. Destination Inspection Fee (DI) 1.2%
7. Registration Tshs 360,000
8. Agency fee $300
 
Unammanisha TZS 15,000,000 au U$S 15,000? In either case kwa pesa hiyo unaweza kupata BWM X5!
 
Wasalaam wanaJF
Naomba kwa anayefahamu anisaidie kufahamu jinsi kodi inavyokokotolewa endapo nitanunua gari lililokuwa na msamaha wa kodi (Tax exemption) ambalo liliingizwa nchini TZ mwaka 2000. Mwenye nalo (raia wa kigeni) analiuza kwa USD 15,000. Ni Landcruiser Prado la 1998. Naomba msaada wa kuelimishwa.natanguliza shukrani.
Mkuu angalia kabla hujanunua iyo gari, mbona umeuziwa ghali sana. Shitukaaa
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom