Msamaha na Kisasi

Mada nzuri sana ila yataka watu wenye kuwa wavumilivu katika kusoma muda mrefu(Maneno/mchango mrefu). Kwa mfano mtu amekuibia ndizi yako moja shambani. Kiuhalisia huyo ukimkamata anastahili na ni haki yake aadhibiwe.
Ukimsamehe utakuwa hujamsaidia kwani kesho atarudia tena. Ukimwadhibu i.e. ukimpa haki yake huwezi jua - adhabu inaweza kumsababishia madhara makubwa e.g. kifo au ulemavu wa kudumu. Katika scenario hiyo, mtu anaweza kutumia hekima na kumwambia mwizi wake "Ondoka hapa" (manake hajasema Nimekusamehe). Mwizi ataondoka lakini atakuwa na dukuduku moyoni mwake kwamba ni nini kitafuata? Wewe uliyemwambia ondoka hapa, hujamtendea haki i.e. hukumpa haki yake mwizi wako - Kesho ataiba tena kwa mwingine.
Sasa tufanyeje(The way forward)? Mtu apime mwenyewe gharama na madhara ya kutoa adhabu kama Haki au Kughairi kutoa hiyo haki i.e. kuacha kutoa adhabu na kubaki kimya. Lakini endapo huyo mkosaji hatimaye atajirudi na kuja kuomba msamaha, basi inafaa umtamkie "Nimekusamehe".
 
Asante sana kaka napokea pongezi zako😊🙏🙏

Ni kweli mkosewa ndio inabidi apime ni namna gani afanye asamehe au amuwajibishe alimkosea

Kwenye comment yako nimejifunza kwa mfano huo iliotoa wa mwizi kukuibia shamani kwako

Kwamba kumwambia mwizi ondoka hapa haina maana umesamehe bali mtu husamewa kwa kua ameomba kusamehewa na wewe umeridhia huo msamaha

Na pia kamba mwizi akiwajibishwa sio makosa maana unakua kama una m shape hiyo tabia ya wizi either kurudi kuiba mara ya pili au kwenda kuiba kwa mwingine

Maana yaake mwizi kuadhibiwa ni haki yake msamaha ni busara tu
 
Kisasi ni haki ya aliyetendewa ubaya haijalishi atabaki na amani au majuto.
Kisasi kama haki ya mtendewa, ni pia sawa na umerudisha Ubaya kwa Mbaya wako. i.e. +1 - 1 =0. Tukija kwenye uhalisia, hesabu hilo halifundishi kweli wa maisha katika jamii tunamoishi kwani linajikita kwenye usemi "Kula na kulipa ndo mtindo wa kisasa". Tutaendelea kupiga na kupigwa na hiyo itaitwa kupigana. Hapo haitakaa itokee Amani -kila siku ni kuviziana katika madhaifu na kukomoana kama sehemu ya ulipizaji kisasi hata kama ni kisasi kwa kosa la mwaka juzi.
 
yapi ni maoni yako kwenye hili ndugu
 
Naomba kukunukuu hapa:
"Maana yake mwizi kuadhibiwa ni haki yake msamaha ni busara tu"
Hoja kubwa hapa ni inakuwa unamwadhibuje mwizi wako?
1. Ukimpeleka kwenye vyo vinavyoitwa ni vyombo vya Sheria, utasumbuliwa sana na pengine Haki isipatikane; ukajikuta umejijengea uhasama .....
2. Utapoteza muda wako mwingi bila faida yoyote eti "ninampatia haki yake mwizi wangu"
3. Hii ndo mbaya zaidi: Unampepeleka kwenye vyombo vya sheria na anahukumiwa kifungo 5yrs. Ndani ya muda huo wa kifungo (5yrs) Familia yake ambayo sio mlengwa wako, itapitia wakati mgumu sana kwa sababu ya wewe kutaka kutoa haki. Kwa hiyo umeadhibu hata wasio husika ktk kosa hilo.
Halafu, katika harakati za kumkamata na kumfikisha kwenye vyombo vya sheria huyo mwizi, ghafla linaibuka kundi la mashabiki na kuanza kutoa kipigo kwa mwizi na kwa bahati mbaya mwizi anapoteza maisha kama tunavyowaona wengi huko mjini. Wewe utaisaidia Polisi kutoa maelezo ya tukio lilivyotokea, Familia itakulaumu ........
Kwa mantiki hiyo mtu anaamua kujinyamazia Nafsi (Karma) ifanye kazi yake
 
Una uhakika ukiwa na majuto utakua na furaha na kisasi chako
kwanza unapswa kuelewa kuwa kisasi hakileti furaha bali kinaleta uwiano.
Anaelipa kisasi hatarajii furaha bali analenga kuleta uwiano juu ya kile alichotendewa.

Mfano hivi visasi vya kwenye mahusiano kwamba me kacheat, ili pawepo na uwiano ke nae lazima acheat (kwa jina la kisasi). ambapo automatically kwenye kulipa kisasi kwa ke akipata magonjwa kwenye hii mode ndo majuto yanaanza.

kwahiyo furaha au majuto kwenye mustakabali huu wa kisasi inategemeana na aina ya kisasi
 
Ni kweli mkuu mi nilinukuu kutoka kwenye comment yako

Acha tuache kila mtu aamue kinachompa amani
Wa kisasi sawa
Wa msamaha sawa
Wa karma kama wewe sawa
 
Tutumie Busara na Hekima kufanya maamuzi hata kama ni maamuzi magumu.
Unafikiri ni hekima na busara ya aina gani ita override maumivu ya ndugu yako kuuliwa alafu huyo aliyemuua ndugu yako still yupo anadunda tu?

Na kitendo cha kaini kulaaniwa baada ya kumuua ndugu yake habil kwako unakitafsiri vipi? is this not amount of Revenge?
 
kwanza unapswa kuelewa kuwa kisasi hakileti furaha bali kinaleta uwiano.
Anaelipa kisasi hatarajii furaha bali analenga kuleta uwiano juu ya kile alichotendewa.
Kama hupati furaha kwa kulipa kisasi basi kinyume chake ni majuto
Mfano hivi visasi vya kwenye mahusiano kwamba me kacheat, ili pawepo na uwiano ke nae lazima acheat (kwa jina la kisasi). ambapo automatically kwenye kulipa kisasi kwa ke akipata magonjwa kwenye hii mode ndo majuto yanaanza.
Kwanini ke ndio apate majuto mwanaume yeye hawezi kupata magonjwa nakujutia?
 
Kama hupati furaha kwa kulipa kisasi basi kinyume chake ni majuto
Naomba nieleweke kwamba lengo la kisasi ni kuleta uwiano na sio kuleta furaha kwa sababu unaweza kulipa kisasi usipate furaha wala hayo majuto ila kukawa na uwiano wa matukio kwamba alifanyia hivi na mimi nimemfanyia hivi. inabaki hivyo
Kwanini ke ndio apate majuto mwanaume yeye hawezi kupata magonjwa nakujutia?
frequency ya majuto ya ke yatakuwa tofauti na me kwa sababu, huyu ke alikuwa anajaribu kuleta uwiano ambapo alikuwa na option ya kutokufanya hivyo kwahy anapofanya hivyo af ikamuathiri ndo safari ya majuto.
Upande wa huyu me sasa amecheat without any influence yaani kafanya kwa hiari yake kwahy inategemeana
 
Mtu aliyekuumiza au kujeruhi kihisia, kiakili au kimwili anaweza kufanya hivyo kwa sababu mbili. Moja kwa kujua. kwa makusudi-nia, ufundi na maarifa. Mbili kwa kutojua. Kutokuwa makini. Yote mawili hatahivyo hayakuondolei wajibu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…