Idd Ninga
JF-Expert Member
- Nov 18, 2012
- 5,208
- 4,405
MSALITI NI HALUA.
1)vitoto mlikataa,tulisema baba yenu.
Nyinyi kwake ni uozo,kama karanga ya mbuzi.
Pindi mnapozubaa,huwaongoza mwenzenu.
Msaliti ni halua,vibwana nyinyi vibua.
2)yeye kwenu ndie nguzo,kuivunja hamuwezi.
Nyinyi kwake ni uozo,kama karanga za mbuzi.
Hamwezi fanya lipizo,nyinyi vifuu vya nazi.
Msaliti ni halua,vibwana nyinyi vibua.
3)yeye hakika farasi,nyinyi manyoya mkia.
Hamuwezi yake kasi,kwake mnajitambia.
Bila yeye kama fisi,mifupa mtajilia.
Msaliti ni halua,vibwana nyinyi vibua.
4)yeye kwenu ni upepo,bali nyinyi vibendera.
Alipoye nanyi mpo,bilaye hamna dira.
Mwampenda ila japo,nyinyi mwamuona swira.
Msaliti ni halua,vibwana nyinyi vibua.
5)yeye hakika ni maji,nyinyi vidogo vimeli.
Tenanyi ni wafa maji,yeye kwenu shelisheli.
Kwake mwapata ulaji,bilaye ni ajali.
Msaliti ni halua,vibwana nyinyi vibua.
6)yeye kwenu ndie jua,nyinyi viua vidogo.
Ukweli mnaujua,yeye ndie lenu pigo.
Mwacheni mtatambus,kuwa nyinyi ni visogo.
Msaliti ni halua,vibwana nyinyi vibua.
7)yeye kwenu ni bahari,ila nyinyi visamaki.
Akiwaacha hatari,mtawa bila mswaki
Mshindwe pandisha mori,yeye si ndie bunduki.
Msaliti ni halua,vibwana nyinyi vibua.
Shairi:MSALITI NI HALUA.
Mtunzi:Idd Ninga wa Tengeru Arusha.
0765382386.
0655519736.
iddyallyninga@gmail.com