Msako wa wamiliki wa visima wasiovilipia ada ya matumizi waja

Wakuu tusijilaumu sana, sisi na sheria bila shuruti ni kama maji na mafuta, hatuendani kabisa, sheria kwenye kila jambo nchini zipo, hata kwenye maliasili na rasilimali zetu, ila kama mjuavyo, tumekuwa hatuzifuati sasa kwa miaka kadhaa, tulizoea kuishi maisha yetu kama wanyama wa misituni, ghafla JPM kakazia kuzifuata imekuwa issue, amini usiamini wajengaji tulikuwa tuking'oa hata mawe ya mipaka hata kuyasogeza kwa faida yetu, dola inapotujia juu hasa kwenye swala la miundo mbinu (kwa faida yetu) bado hatuelewi na kuona karaha ya ajabu...Hasira zetu at least zinakimbilia kuwa wakinzani kwa chama tawala, tukidhani eti nawo wakiingia madarakani kila kitu kitakuwa ruksa?!
Ila tutazoea, hakuna jinsi, binafsi pia naipata joto la jiwe na sheria za nchi lakini bora hivyo kuliko vinginevyo...
Hizi sheria hazojatungwa na bunge letu; zimekumbatiwa tu; ndiyo maana tunawalaumu hawa jopo la k utunga sheria kuwa wanafanya kazi chini ya kiwango. Hawana kabisa uwezo wa kuziidadavua sheria na kuona madhara yake.
Ina maana hata vijijini waenda kuwatoza kodi watu wanaotumia visima? Nakushangaa unapozitetea sheria kandamizi.
 
Sheria ya kipuuzi sijapata ona! Hivi kama serikali haija facilitate katika miundombinu yote ya kujenga kisima inaanzaje kudai kodi kama sio ubabe wa kijinga? Tuwe wabunifu tuneemeshe wananchi kimapatao kisha ndio tutoze kodi viongozi! Kwa hali ilipofikia sitashangaa kama kutawekwa kodi ya solar panel na kutundika dishi juu ya bati! Sio poa,
 
turudi kwenye mada: tanzania ya viwanda. miaka mitatu ishakatika hata cherehani 4 hatuzioni. mwakani msimu wa fitna za uchaguzi. viwanda lini?
Viwanda ni vya kwenye makaratasi tu,mwijage alisema yeye ni mpiga sound tu
 
Sheria ndogo ya huduma ya choo inakuja, mtu yeyote mwenye choo au aneyeenda choon/ kushusha mzigo inabidi alipe ada ya utathimin wa mazingira na utafiti wa ikolojia
Bado kodi ya wazinzi iko njiani
 
SERIKALI kuanza msako wa wamiliki wa visima visivyolipiwa ada ya matumizi ya maji kwa ajili ya kuwachukulia hatua za kisheria kwa kuwafikisha mahakamani. Akizungumza na wanahabari leo tarehe 19 Novemba 2018 jijini Dar es Salaam, Afisa Maji Bonde la Wami/Ruvu, Simon Ngonyani amesema watumiaji wa maji wasiofuata taratibu za kisheria, ikiwemo wamiliki wa hoteli 100, vituo vya mafuta 25 na kampuni 11 watafikishwa mahakamani.

“Hawa watu tukiwapelekea mahakamani tunacho wadai ni zaidi ya milioni 200 na kitu, ukiangalia kuna wengine wana madeni yaani mtu ana kisima miaka kumi iliyopita halipi, tuu hadi leo hizo nazo hatutamuacha nazo atalipa zote, baada ya kufanya zoezi zima tutajua tunawadai shilingi ngapi,” amesema Ngonyani.

Akielezea kuhusu ada za matumizi ya maji, Ngonyani amesema sheria inataka wamiliki wa visima kulipa ada hizo ili zisaidie kwenye masuala mbalimbali ikiwemo utafiti wa mwenendo wa maji chini ya ardhi.

“Sheria inasema hata kama umechimba mwenyewe, sheria inasema ulipe ada ya matumizi ya maji hayo ili hiyo ada itumike, kwa mfano inatakiwa kuangalia mwenendo wa maji ndani ya ardhi ikiwemo ubora wa maji. Sababu tuko karibu na bahari hivyo maji ya bahari yanaweza kupanda juu umechimba kisima leo maji mazuri, unashangaa mwaka mmoja au miaka fulani maji yana chumvi,” amesema Ngonyani.
Huyu jamaa ni Afisa Maji Bonde la Wami/Ruvu , mie wa Dar ananihusu nini?
 
Tunapoelekea ukikata roho utalipishwa na sehemu za makaburi tutalipishwa
 
Tanzania yangu naona wanatafuta mapatoo kwa hali na malii...! Hapa ndo naanza kuelewa why Jeshi linatumikaa
 
Mimi kama mlipakodi wa miaka mingi tu naomba serikali iwe na busara kidogo. Kuna maeneo mengi sana huku Dar es salaam na hata usitaje miji iliyopo nje ya Dar ambao wote hatuna maji salama. Hii ni kazi ya hii wizara kuhakikisha tuna maji salama. Ok sawa so wengi wetu tumejiongeza kwa kuchimba visima ili tukazane na uhai wetu halafu why tulipie leseni?? kwanza why tuombe leseni? Hii wizara ikiona mtu anahangaika kutafuta hiyo leseni ingekuwa inajiongeza kwa kufika eneo la mteja wake na kuchimba kisima cha watu wa eneo hilo ili na sisi tusave mamilioni tunayotumia kuchimba visima. Please this is your job as the government. Muwe na busara. Tanzania bado iko nyuma sana kimiundombinu na sisi wananchi tumejiongeza kwa kupunguza pressure ya serikali.
 
hii na kodi ya jengo ni uonevu, double taxation. kodi ya ardhi inatosha kuhalalisha matumizi ya ardhi uliopewa.
 
Kisima achimbe mwenyewe..kwa matumizi yake mwenyewe....gharama za kupandisha maji za kwake mwenyewe.......halafu kodi mchukue nyie..bila hata aibu...
Africa bado kuna sheria za kikoloni...yaleyale ya kodi ya kichwa

Hii Kodi hiiii ,sitaki hata kukumbuka.
 
Back
Top Bottom