Rais Samia azindua programu ya uchimbaji wa visima 67,800

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,817
4,568
Rais Samia Suluhu Hassan amezindua programu ya uchimbaji wa visima kwa ajili ya wakulima wadogo 67,850 kwa nchi nzima vitakavyowezesha hekari 2,7014,000 kufikiwa na mfumo wa umwagiliaji.

Akitoa maelezo kwa Rais Samia katika kilele cha maadhimisho ya sherehe ya wakulima nane nane kwenye viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya, leo Jumanne, Agosti 8, 2023, Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe amesema kila kisima kitakuwa na uwezo wa kuhudumia wakulima 16.

Amesema kisima hicho kitakuwa na tenki la lita 5,000 litakalokuwa limefungwa mfumo wa umeme jua kwa ajili ya ku-pump.
"Pia mkulima atapewa eneo la umwagiliaji la heka 2.5 na mkulima wa kwanza katika program hii anatoka wilayani Mbarali mkoani Mbeya," amesema.

Akizungumzia mradi huo, Rais Samia amempongeza Waziri Bashe kwenye eneo hilo la umwagiliaji maji kwa kufanikiwa kutumia vyanzo mbalimbali ikiwamo skimu za umwagiliaji.

Amesema upo uwezekano wa kutumia maziwa ambayo Mungu ameibariki Tanzania yakatumika pia katika kilimo cha umwagiliaji.
"Tunalo Ziwa Vicktoria, Tanganyika na Nyasa maji yako pale. Tukivuta maji machache kufanyia kilimo haitadhuru samaki waliokuwepo pale wala haitapunguza kina cha maji cha meli kuelea, ni maziwa makubwa Mungu katubariki.

"Angalieni uwezekano wa kutoa maji kumwagilia kwenye mashamba wakulima wavune mara mbili kwa mwaka," amesema.

Ametoa mfano nchi kama Misri inatumia maji ya Mto Nile kuzalisha ngano ambayo imeifanya nchi hiyo kuwa kinara wa uzalishaji wa zao hilo duniani.

"Kuwepo mikataba sijui ya kikanda wenzetu wamefumba macho na masikio. Sisi Mungu katupa maziwa matatu halafu tunatafuta vyanzo vya kumwagilia kilimo! vitumiwe watalaamu wakae ili kilimo chetu kikue zaidi," amesema.
 
Mradi huo ungekuwa na tija zaidi kama wangesaidiwa vijana na wakulima ambao wapo mashambani tayari.

Mkulima mwenye uzoefu ni rahisi sana kumsaidia kutatua changamoto zake na taifa likanufaika kuliko wale wanaolima kwenye karatasi na computer ambapo huu mradi umeegemea zaidi huko.

Kimsingi miradi ya kumwagilia kwa visima vya kutumia umeme ni ya kinadharia zaidi.

Serikali ianzishe irrigation schemes kwa kutumia mito na mabwawa kwenye maeneo ambayo yapo naturally favourable kabla ya hizi utopian plans.
 
Back
Top Bottom