Msako dhidi ya Boko haram, 35 wauawa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Msako dhidi ya Boko haram, 35 wauawa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mzito Kabwela, Sep 25, 2012.

 1. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #1
  Sep 25, 2012
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,520
  Likes Received: 1,691
  Trophy Points: 280
  Takriban wapiganaji 35 wa kundi la kiisilamu la Boko Haram, wameuawa katika msako mkali dhidi ya kundi hilo Kaskazini Mashariki mwa Nigeria.
  Kwa mujibu wa jeshi la Nigeria, wapiganaji wengine sitini walikamatwa wakati wa msako huo kwenye majimbo ya Adamawa na Yobe.

  Kundi hilo la kiisilamu, linapinga mifumo ya kimagharibi na athari zake nchini Nigeria na wamekuwa wakifanya mashambulizi yanayolenga maslahi ya nchi za Magharibi pamoja na makanisa.

  Mnamo siku ya Jumapili, kulitokea shambulizi dhidi ya kanisa moja katoliki na ambalo lilisababisha mauaji ya watu wawili. Boko Haram ndilo limelaumiwa kwa kufanya shambulizi hilo.
  Msemaji wa jeshi nchini humo, alifahamisha shirika la habari la AFP kuwa msako huo ulifanyika usiku kucha kati ya siku ya Jumapili na Jumatatu.
  Wanajeshi walifanya msako wa nyumba hadi nyumba, katika mitaa mitatu na wakati mwingine kufyatuliana risasi na wapiganaji hao, usiku kucha.
  Wanajeshi wawili walijeruhiwa katika makabiliano hayo.
  Bunduki na mabomu vilipatikana katika maficho ya wanamgambo hao pamoja na silaha zengine ikiwemo mishale 32 na panga.
  Mji huo umekuwa mojawapo ya miji iliyoathirika sana kutokana na harakati za Boko Harama ambalo linataka kutumika kwa sheria za kiisilamu kote nchini humo.

  Source: BBC Swahili - Habari - Msako dhidi ya Boko haram, 35 wauawa

   
 2. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #2
  Sep 25, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 549
  Trophy Points: 280
  safi kabisa.Naigeria kamata ibilisi hao
   
 3. B

  Bangoo JF-Expert Member

  #3
  Sep 25, 2012
  Joined: Nov 3, 2011
  Messages: 5,594
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Wanajilipua na kuuwa wanadamu wasio na hatia ili wao waende mbinguni!, eti hawataki elimu ya magharibi!

  Hivi dunia hii unaweza kuendesha bila elimu ya magharibi!

  Hata nchi za kiislamu wanasoma elimu za magharibi! Sasa wao wanataka kusoma nini?


  Ama kweli watu hawa duniani wanaleta janga!!!.

  Ee mungu tunusuru na huyu ibilisi anaezidi kupata nguvu
  hakika nguvu zako zitamshinda.
   
 4. Remote

  Remote JF-Expert Member

  #4
  Sep 25, 2012
  Joined: May 20, 2011
  Messages: 14,875
  Likes Received: 1,561
  Trophy Points: 280
  Wamekuwa ni janga la kidunia sasa
   
 5. N

  Nyakipambo JF-Expert Member

  #5
  Sep 25, 2012
  Joined: Nov 10, 2011
  Messages: 435
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Wewe Sangarara hao maibilisi wakija watakutoa macho!
   
 6. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #6
  Sep 25, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 549
  Trophy Points: 280
  kwani Boko haramu wapo hapa JF?
   
 7. Ally Kombo

  Ally Kombo Verified User

  #7
  Sep 25, 2012
  Joined: Nov 11, 2010
  Messages: 11,440
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 145
  ..........haya Wagalatia ukumbi wenu !
   
 8. T

  Taso JF-Expert Member

  #8
  Sep 25, 2012
  Joined: Jun 12, 2010
  Messages: 1,649
  Likes Received: 458
  Trophy Points: 180
  Nigeria ni sawa na mgonjwa aliyekunywa vidonge lakini hakumaliza dose nzima, ugonjwa unarudi kwa kasi.

  Walipokua wanatafuta tatuzi la udini waliamua kugawana maeneo, yale yaliyokuwa na mrengo wa kidini ikakubalika yatawaliwe na sheria za kidini wanayotaka. Lakini bado wanatokea watu wengine wanataka nchi nzima nayo iwe kama wao walivyo. Kukata mzizi wa fitini, kupata suluhisho la kudumu, ilibidi Nigeria ikatwe panga katikati ziwe nchi mbili au tatu tofauti, kila dini na upande wake.

  Wakati mwingine si busara kung'ang'ania miungano ambayo haina tija, ndio maana hata kwenye ndoa kuna divorce.
   
Loading...