POLISI TUNAOMBA USHIRIKIANOA CHADEMA TUMEWAGUNDUA. STRATEGY HIZI MLIZIANZA SIKU NYINGI SANA, BAADA YA KUONA KALENGA MNAFELI. MMEANZISHA ILE STRATEGY YENU, valisha vijana nguo za ccm endeleza vurugu mtindo mmoja.
Ndugu Wananchi,
Taifa letu la Tanzania linapitia katika wakati wa upevukaji wa uhuru wa kusema kwa uwazi, pia Taifa letu linapitia katika harakati za demokrasia na maozezi ya deomkrasia.
Katika kipindi hiki tumeshuhudia mambo mengi yakitokea ikiwa ni pamoja na baadhi ya watu na taasisi zao kuutumia uhuru huu wa kusema vibaya kwa lengo la kutimiza malengo yao binafsi au kutimiza wajibu wa uhuru wao wa kusema.
Pia tumeshuhudia baadhi ya watanzania wakiitumia vibaya demokrasia na wengine wakiitumia vizuri kwa manufaa ya umma na wengine kwa manufaa yao wenyewe.
Baada ya utangulizi huo sasa nianze makala hii kwa kina na kwa kusema kila kitu ninachokifahamu kuhusu mada hii.
Ndugu Wananchi,
Mimi nimekuwa mtumishi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) toka 2003 nikiwa mwanachama wa kujitolea na baadae 2004/8 nikiwa kiongozi wa chama makao makuu,
Mwaka 2006 secretariat ya makao makuu ilipanga mikakati ya namna ya kukifanya chama kiwe maarufu na namna ya kuwafanya wananchi wakichukie chama tawala ili watafute mbadala wake ambao tulilenga uwe ni chadema.
Katika mikakati ile tuliazimia mambo mawili makubwa yatakayoleta matokeo yote mawili kwa wakati mmoja yaani kukifanya chama kiwe maarufu na wakati huo huo wanachi wakichukie chama tawala ili wajiunge na CHADEMA.
Mkakati namba moja ulikuwa kuandaa timu ya red brigade ya watu wenye weledi wa kijeshi wenye uwezo wa kucheza karete au kong fou ili tuwaandae wawateke viongozi wa taifa wa chama (CHADEMA),
Mkakati ule uliwalenga wabunge maarufu Dr Slaa na Zitto Kabwe, lakini pia ulilenga kumteka Mwenyeikiti wa Taifa Mbowe Alkaeli Freeman. (Lakini haya ya kutekwa viongozi yalipangwa nyuma ya uficho bila dr slaa kuhusishwa kwa sababu maalum nitaeleza baadae)
Ili kulifanya tukio lile lihusishwe na Chama tawala tulipanga yatolewe matamko makali dhidi ya serikali na chama tawala kwa lugha kali itakayosababisha serikali ijibu na ikibidi ijikanganye kutoa kauli ili red brigade watakapotuteka iwe sababu ya moja kwa moja kuwahusisha.
Katika mkakati ule mbinu na namna ya kuwateka viongozi hawa uliandaliwa vyema vijana wakiwa chini ya uangalizi wa mlinzi wa Mbowe aliyetolewa tarime (kwa jina la Chacha suguta) wakipewa mafunzo namna ya kutokomea baada ya kuwateka viongozi wetu na kuwapora computa na simu zao bila kuwadhuru.
SIKU YA TUKIO
Tukiwa makao makuu mida ya saa 3 asubuhi tukingojea muda wa matamko kutolewa na viongozi wa chama, alikuja Marehemu Chacha Wangwe akiongozana na kijana aliyekuwa mahili sana kwa siasa za tarime Chacha Okongo aliyeshinda kura za maoni kugombea Ubunge jimbo la Nyamagana lakini akaondolewa na wenje akapewa nafasi yake kwa misingi ya Mbowe kuogopa damu ya marehemu chacha wangwe ingeweza kumrudia mapema sana endapo Okongo angepata nafasi ya uongozi.
Marehemu Wangwe alipoingia na kuambia juu ya tamko lililoandaliwa kutolewa kuisema serikali kuwa imepanga mbinu ya kuwaua Mbowe, Zitto na Dr Slaa, Marehemu alipinga issue hiyo na kuonya kuwa itaweza kukidhuru chama chenyewe kama haikupimwa kabla ya kuitoa,
Wangwe akaonya kuwa sio kila umaarufu huwa na tija,
Mbowe aliwakaripia sana Mnyika na Zitto kwa kumshirikisha Wangwe ambaye yeye alimwita ni mvuta bangi tena akisisitiza kuwa kama ni bangi wengi tunavuta lakini zake ni za wehu.
Kwa misimamo ya wangwe aliyekuwa mbunge wakati huo hajawa Makamu Mwenyekiti wa chama taifa, Mbowe alizuia tamko lile, waandishi waliokuwa wamealikwa walipofika waliambiwa kuwa kikao kilihairishwa.
MIPANGO YA KUTEKWA YAKAMILIKA.
Mbowe aliwaita vijana wake wa red brigade akiwa na vijana wake wa mipango Mnyika na Zitto(zitto wakati huo akiwa miongoni mwa wanaompinga wangwe kwa nguvu zote bila kujua afanyalo akiwa mkono wa kazi wa Mbowe akiamini kuwa anapambana na wahujumu wa chama kumbe anapambana na demokrasia) ikumbukwe kuwa Zitto aliamua kujitoa kwa mbowe baada ya mbowe kushagilia kifo cha wangwe wakiwa musoma wakitoka msibani, wakiwa hotelini Mbowe alianza kumsema marehemu vibaya akiamini kuwa aliokaa nao wote ni vijana wake, hapo zitto aliinuka na kusema kwa uchungu sana kuwa sikujua kama mwenyekiti unaroho mbaya kiasi hiki, alipomaliza hayo aliondoka na ndio ukawa mwanzo wa mwisho wa uhusiano mzuri wa mbowe na Zitto.
Sasa tuendelee namipango ya kujiteka,
Mbowe akiwa na Zitto na Mnyika ndani ya ofisi yao makao makuu mitaa ya ufipa, walipanga mikakati ya kuwaita vijana wao walioandaliwa kufanya utekeji bila kumtaarifu katibu mkuu wao wakihofia ataogopa na pengine atatoroka, lakini waliamua kumficha pia ili atakapotekwa na kuporwa computa yake ya mkononi na simu zake kisha mwenyekiti atamwamuru katibu atoe tamko huku akiamini ni ccm wametuma watekaji ilia toe tamko lenye lugha kali kwani walijua akipaniki huwa na hasira na kumwaga maneno mengi ya hovyo kama tunavyomuona akifanya leo.
Ndugu Wananchi,
Ikiwa ni saa 7 mchana mpango ukiwa umepangwa siku ya jumapili siku waliyoipanga na kuiona ni siku muafaka ya kutekwa, mwenyekiti alimwambia Dr slaa kuwa siku hiyo usiku watakuwa na kikao pale ofsini kwao makao makuu Ufipa kuanzia saa 4 usiku akamuomba ajiandae tu lakini ajenda atakuja nazo yeye, dr slaa alikubali bila kujua kuna nini nyuma ya pazia,
Baadaye Mbowe alimwagiza Mnyika kuwataarifu watekaji kuwa wajiweke tayari,
Mnyika alitekeleza agizo hilo lakini kama kawaida yake alitoa uzuru wa kutokuwepo kwenye tukio kwa kusingizia jukumu la kifamilia,
Ikumbukwe hii imekua tabia yake kwa mlolongo ufuatao;-
Wakati kambi ya upinzani bungeni iliazimia kuondoka bungeni kupinga kumtambua Rais Kikwete, Mnyika yeye aliomba ruksa kuwa anaumwa na hakuingia bungeni kwa uoga wake na kwa kumuonea aibu kikwete kwani kikwete alimchangia Mnyika Tsh 5,500,000/= wakati wa kampeni kwa sababu ya kutompenda hawa ngumbi ambaye aliingia kwa nguvu za lowassa na ndio maana jk alimteua Nape kuwa mkuu wa wilaya masasi wakati wa kampeni,
Kikao cha kumshughulikia Zitto kilichokaliwa kwa Mbowe kilipoiva Mnyika aliomba ruksa na kuondoka,
Kadhalika na kwenye mpango ule wa kutekwa Mnyika alifanya hivyo (alidanganya kuwa mjomba wake ametoka Botswana na hakuna mtu wa kumpokea bali yeye anategemewakumpokea)
Zitto na Mbowe waliwasili makao makuu wakamkuta Dr Slaa amekaeti akiwangojea,
Mkakati ulikuwa watekwe wote ikibidi wapigwe japo sio kwa kiwango kikubwa cha kuumizwa, wakati wakizugazuga kuisubiri saa6 usiku ifike Zitto alipigiwa simu na mkuu wa kikosi cha watekaji na kuomba pesa za mafuta kwa kuwa gari lao moja limebuma, wakati huo hakukuwa na M-Pesa wala kitu kama hicho,
Mbowe alitoa tsh 200,000/= zitto akapewa apelike msasani walipokuwa, zitto alifikisha pesa kasha akaacha maagizo kuwa wasubiri atakapofika makao makuu atawapa alerting sign.
Zitto alifika makao makuu akamkuta mbowe anajadiliana na Dr slaa kama viongozi wakipanga ajenda za vikao,
Zitto akampa alama ya dole kuonyesha amekamilisha kazi huko huku Dr slaa haju lolote,
Baada ya dakika kadhaa mbowe aliaga kuwa anaenda kutoa pesa kwenye ATM mitaa ya mwanamboka manyanya,
Lakini muda anaaga zilikuwa zimebaki dakika chache sana kabla ya kutimu saa6 muda muafaka kwa kutekwa walikojiandalia,
Mbowe aliondoka na derva wake akiwaacha wajumbe wamekaa ndani ya makao makuu ili hali mpango huu ukiwa unajulikana kwa zitto, mbowe na mimi tu, wajumbe wengine hawakujua kitu, sisi tulijiandaa kisaikolojia lakini nilishangaa kuwaona akina Mnyika na Mbowe wanaanza kutoroka, nikajiuliza je walitoa maagizo kuwa tuuwawe au walitoa maagizo kuwa tuumizwe?
Nikamvuta Zitto kando nikamngata sikio juu ya jambo hili nay eye akashituka, wakati huo wale maghaidi feki walikuwa wakipiga simu kutaka kupata ruksa ya wao kuvamia,
Zitto akampigia Mbowe lakini Mbowe hakupokea simu, bali akatuma sms kuwa waambie hao makamanda waje mie nitafika kabla hawajafika,
Nilimkataza Zitto asiwape ruksa hao maghaidi feki kwani yawezekana kuna mchezo umetegwa bila sisi kujua na tunaweza kudhurika kasha tukajuta nae akanisikiliza tukaazimia tumngojee Mbowe arudi kwanza,
Tulingojea kwa muda wa saa nzima mpaka saa 6:40 bila mbowe kufika toka umbali wa kilomita moja ambayo kwa miguu ungeweza kutumia dakika 20 tu,
Mimi niliamua kuondoka kasha zitto nae akanitxt kuwa ameondoka,
Ilipofika saa 8 usiku mbowe alipiga simu kwangu na kuniuliza kama tuko salama au la!!
Nikamjibu wewe uko wapi mwenyekiti wangu?
Akajibu nilipata mgonjwa ghafla nikampeleka hosp.
Ikumbukwe kuwa mbowe ana tabia ya kuanzisha zogo kasha kuwaachia iwatafune.
Mtakumbuka Mbowe alipowadanganya vijana na Dr slaa wakeshe wakiota moto kuitaka serikali imwachie Lema huko Arusha, lakini Mbowe alitoroka baada ya kuona zogo linawaka moto mkali akamwacha Dr Slaa akakamatwa peke yake na wapambe wao.
Tuendelee na sakata la kutekwa
Usiku ule tulimwacha dr slaa alikesha mpaka saa tisa usiku hakuna aliyepokea simu yake tena na hata anaposoma makala hii atakumbuka vizuri sana usiku ule!
Siku iliyofuata kila mmoja alikuja na sababu zake za uongo ili mradi wajumbe waliokuwa wakisubiri kikao ambao wote walikuwa watumishi wa makao makuu waamini.
Hakuna anaejua wale maghaidi feki waliishia wapi!