Msajili wa vyama vya siasa nchini Jaji Francis Mutungi ametua mkoani Iringa na kulaani vikali kitendo cha kupigwa vibaya kwa Padre wa Kanisa la Orthodox Parokia ya Basil Mkuu Baba Costantine Mbilinyi.
Akizungumza na waandishi wa habari msajili huyo amelaani vikali unyama huo usio na hata chembe ya ubinadamu na kusema tayari ofisi yake imeanza uchunguzi rasmi wa tukio hilo.
Jaji Mutungi amesema anatarajia kukutana na Padre Mbilinyi ili amweleze mkasa mzima ulivyotokea na baada ya hapo ofisi yake itachukua hatua kali bila kumpendelea wala kumuogopa mtu yeyote.
Padre huyo mwenye ushawishi mkubwa jimboni Kalenga alipigwa vibaya na wafuasi wa CCM kisha kumfunga kamba mikononi na miguuni na kuburutwa mithilili ya mwizi na kwenda kumtupa kizuizini katika ofisi ya kijiji.Kosa la Padre huyo inadaiwa ni kuonekana akiwa anazungumza na wafuasi wa Chadema.
Kanisa la Orthodox lina jumla ya makanisa 19 Jimboni Kalenga huku makanisa hayo yakiwa na waumini wengi.
Source:Tanzania Daima.