Chachu Ombara
JF-Expert Member
- Dec 11, 2012
- 5,897
- 10,358
Msajili wa Hazina Nehemiah Mchechu amesema kuwa kuna wimbi la watumishi ambao wanakimbilia kuomba uhamisho kutoka katika taasisi zao kwenya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Shirika la Umeme nchini (Tanesco), Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA) na Mamlaka ya Udhibiti Nishati na Maji (EWURA).
Akizungumza katika Kikao Kazi cha Wenyeviti wa Bodi na Watendaji Wakuu wa Taasisi za Umma, Mchechu amesema kumekuwa na ‘Mafuriko’ ya maombi kwenda taasisi hizo akisisitiza kuwa “watu wanataka kwenda huko kwa kuwa mapato ni mazuri.”
Amewataka Watendaji kusaidia kuboresha taasisi zao ili kuwezesha mashirika hayo kusimama.
Hata hivyo Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Charles Kichere amesema baadhi ya Taasisi zimekuwa zikipelekewa watumishi ambao hawana uwezo akishauri kufanyike uchambuzi ili watu wanaohamishwa wawe na sifa zinazohitajika katika taasisi husika.
“Unakuta kuna taasisi inaletewa watu ambao hata haiwahitaji kwa sababu tu ni watumishi wa umma, nadhani hili nalo lifanyiwe kazi,” ameshauri CAG.