Msajili aingilie kati mgogoro huu wa TLP | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Msajili aingilie kati mgogoro huu wa TLP

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Technician, Jul 4, 2011.

 1. Technician

  Technician JF-Expert Member

  #1
  Jul 4, 2011
  Joined: Mar 30, 2010
  Messages: 843
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading, width: 100%"]Msajili aingilie kati mgogoro huu wa TLP
  [/TD]
  [TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] Send to a friend [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"] Tuesday, 28 June 2011 20:16 [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD] 0diggsdigg

  [​IMG]MGOGORO unaoendelea hivi sasa katika Chama cha Tanzania Labour Party (TLP) utakuwa umetoa somo moja kubwa kwa viongozi wa vyama vyote vya siasa nchini. Somo hilo ni kwamba, uhai wa chama cha siasa ni kufanya kazi ya siasa na kufanya kazi hiyo kama chama cha siasa. Wapo baadhi ya wanasiasa wanaojidanganya kuwa, vyama vya siasa vinaweza kufanikiwa hata kama havifanyi kazi ya siasa na kwamba, siyo lazima kufanya kazi hiyo kama vyama vya siasa.

  Kwa maneno mengine, siasa ni kama mchezo wowote unaochezwa kwa kufuata sheria na taratibu zilizowekwa. Vyama vya siasa sio tu vinacheza mchezo wa siasa kwa kufuata sheria na taratibu zilizowekwa, bali pia vinacheza mchezo huo kama vyama vya siasa. Kinachosisitizwa hapa ni kuwa, kila mchezo unazo sheria, kanuni na miiko inayousimamia. Kwa mfano, sheria na kanuni za mchezo wa kikapu haziwezi kutumika katika mchezo wa netiboli. Hivyohivyo, mpira wa miguu hauwezi kuchezeka kwa kutumia sheria na kanuni za mchezo wa mieleka, na kadhalika.

  Hivyo, mchezo wa siasa unachezwa na wanasiasa ndani ya vyama vya siasa kwa mujibu wa sheria za nchi na katiba za vyama husika. Ili kiwe na sifa za kuwa chama cha siasa na kupata mafanikio, kwa mfano, chama cha siasa lazima kiwe na wanachama ambao watakipa uhai wa kushindana na vyama vingine ili hatimaye kishinde chaguzi mbalimbali kuanzia katika kitongoji hadi taifa, kwa maana ya kupata wawakilishi wengi bungeni na kutwaa Dola.

  Kama lengo la chama cha siasa ni kutwaa Dola ili kiweze kutekeleza sera na ilani yake ya uchaguzi baada ya kuunda serikali, basi lazima kifanye kazi ya siasa katika ngazi zote, mijini na vijijini. Lakini hakuna chama kinachoweza kufanikiwa kuenea nchi nzima bila kuwa na mikakati ya kuhamasisha na kuongeza wanachama kwa kujenga mtandao katika vitongoji, vijiji, kata tarafa hadi ngazi ya taifa. Chama lazima kifungue matawi, kifanye vikao kwa mujibu wa katiba, kiandae mikutano ya hadhara kwa lengo la kuhamasisha wananchi kuhusu sera, matarajio na matamanio ya chama hicho.

  Tumetumia nafasi kubwa ya safu hii kwa makusudi kabisa ili kuelezea wajibu na kazi za chama cha siasa kwa sababu tunadhani kuwa, ingawa mgogoro uliomo katika TLP unaweza kuonekana kama ugomvi wa viongozi, ukweli ni kuwa kwa kiasi kikubwa unatokana na chama hicho kutoendeshwa kama chama cha siasa na kutofanya kazi ya siasa kwa misingi ya sheria inayoongoza vyama vya siasa na katiba ya chama hicho.

  Mgogoro wa TLP kwa kiasi kikubwa umelelewa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa ambayo kwa muda mrefu sasa imekuwa ikionekana kuegemea upande mmoja na kupuuza malalamiko ya upande wa pili. Pamoja na ukweli kwamba, kazi ya Msajili siyo kuingilia masuala ya ndani ya vyama hivyo, bado analo jukumu la kusuluhisha migogoro na kuhakikisha kuwa, vyama hivyo vinaendeshwa kwa mujibu wa katiba zao na sheria ya mwaka 1992 iliyoanzisha vyama hivyo.

  Ni vigumu kuelewa kwa nini Msajili amekaa kimya tangu mgogoro wa sasa uanze kufurukuta baada ya kumalizika kwa Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana. Vioja na vurugu zilizotokea juzi katika Ofisi za Maelezo kati ya pande mbili zinazopingana katika chama hicho, zilitoa picha halisi ya ukubwa wa tatizo ambalo kimsingi limo katika mamlaka ya Msajili. Demokrasia na uongozi wa pamoja vinapokosekana ndani ya chama ndipo migogoro, fujo na vioja hujikita na kufanya chama husika kupoteza mwelekeo kama ilivyo kwa TLP.

  Sisi tunadhani kuwa, malalamiko yaliyotolewa juzi na upande wa pili dhidi ya mwenyekiti wa chama hicho ni mazito na yanapaswa kutafutiwa ufumbuzi. Tunakishauri TLP kirudi katika misingi iliyokianzisha, kifanye kazi ya siasa na kifanye hivyo kama chama cha siasa.[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. M

  Marytina JF-Expert Member

  #2
  Jul 4, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,037
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  Mrema mwenyekiti
  mrema Katibu
  mrema mhazini
  mrema mnadhimu
  mrema kila kitu

  Mrema:ANATAMAA SANA YA MADARAKA
  MUHIMU: ana record nzuri ya kudeliver akilwa waziri
   
 3. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #3
  Jul 4, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,330
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  Mrema ni kichomi! Anaongoza chama kama familia yake.
   
 4. Idimi

  Idimi JF-Expert Member

  #4
  Jul 4, 2011
  Joined: Mar 18, 2007
  Messages: 10,215
  Likes Received: 2,077
  Trophy Points: 280
  Lakini kumbuka kwamba msajili wa vyama ni sehemu ta tatizo linavilokabili vyama vya siasa hapa nchini! Malamiko dhidi yake ni mengi kuliko malalamiko dhidi ya Mrema! Yeye ndo kamlea Mrema mpaka kufikia kuwa mwamuzi wa kila kitu katika chama chake (na si mkutano mkuu), sioni kama anaweza kutatua mgogoro wa TLP kwa hatua uliyofikia!
  I stand to be corrected!
   
 5. 2

  2nd edition Member

  #5
  Jul 4, 2011
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 33
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  aache tu hicho chama kife natural death ili kupunguza utitiri wa vyama vya siasa visivyokuwa na tija kwa taifa
   
Loading...