Msaidieni mdogo wangu

Msaidieni mdogo wangu

pole sana
sie tuna mdogo wetu ameshindikana kabisa baada ya kuchelewa kugundua jutahidi kumpatia msaada mapema vinginevyo ni janga la familia
 
Polen sana,
Nijuavyo mimi bila yeye kuamua kuacha kutumia ni ngumu kumzuia asitumie
Oongeeni nae mpeni side effect ya hayo madawa then
akionekana anajutia ndo mumpeleke rehab
 
Anatumia madawa gan huyo dogo?

kuna hospital special kwa ajil ya victims wa drugs au rehabs.

but kabla hamjafikiria kumpeleka kwenye matibabu ingefaa mkae nae na muongee nae kwa kirefu. Kujua ni kwanin alianza kutumia madawa pia mjue kama anajutia kuacha shule na kupoteza future yake.

pia mumpe mifano ya marafik zake wa utotoni wenye mafanikio mazuri shuleni. Cha msingi mnatakiwa muongeenae kwa upole na upendo huku mukimtengenezea mazingira ya ku regret tabia yake ya kutumia madawa.

akisha regret atakuwa tayar kuacha na hapo ndo mumpeleke rehabs au hospital kwa matibabu,uangalizi na ushauri zaid.

Mkuu hakuna mvuta unga aliekolea ambae aliacha kwa kuambiwa tu aangalie wenziwe au kutengenezewa mazingira ya ku-regret.. In case kama hufahamu Mkuu.. starehe ya utumiaji wa madawa ya kulevya na haswa cocaine na heroin unakuwa mwanzo tu wakati unapoanza kutumia.. Unakuwa unajisikia hali fulani ya ecstasy hivi.. Ila baadae sasa inabadilika na kuwa kama tiba.. Anapoyakosa madawa mtumiaji anakuwa na maumivu mwilini ambayo mwisho wa siku anashindwa kuyavumilia.. Hali hiyo inapelekea mpaka kuwa wagonjwa kabisa wenyewe wanaita alosto.. Wanapokuwa kwenye hali hiyo wanaweza kufanya lolote (hata kuliwa tigo) mradi wapate dawa ili wadevele..

Ushauri wangu kwa happiness win ni kutafuta rehab clinics ambazo wataweza kumsaidia mdogo wake..
 
Last edited by a moderator:

Asante sana. Ziko wapi hizo rehab?. Unaweza kujua gharama zake?
 
Polen sana,
Nijuavyo mimi bila yeye kuamua kuacha kutumia ni ngumu kumzuia asitumie
Oongeeni nae mpeni side effect ya hayo madawa then
akionekana anajutia ndo mumpeleke rehab

Kwa kweli hadi sasa haoneshi kujutia ila yuko tu kama zoba fulani, yaani kazubaa. Hata ukiongea naye anakuangalia tu na kuishia kulala.
 
Asante kwa ushauri wako. Huyu Bwana mdogo amekuwa zoba kabisaaa, yaani tumeshakaa naye hana la maana analoongea zaidi ya kusinzia na kutoa udenda. Yaani unaweza kuongea naye mwenzio anainamaaa tu hadi analala, ila anadai yeye hajala madawa zaidi ya bangi. muonekano wake ni madawa tu yamemjaa akilini, na ameanza kuiba vitu na pesa nyumbani, kwa ndugu na majirani. Sijui nimpeleke hospitali gani?

Kuna hosp. Tanga inaitwa rutindi ni nzuri au rehab kwa hapa bongo sijui ipi nzuri.

ila hutaweza kumsaidia bila yeye kuwa tayari kuacha kutumia hayo madawa! Mkilazimisha treatment atatulia then atarudia tena! Ni vizur mkampa couselling had akubal kuacha ndio apate treatment.

kumpeleka shule mbali anaweza akasababisha matatizo mengne..kama ameshaanza udokoz ataibia wenzake akasake unga popote na hyo inaweza leta matatzo kwenu.

counselling ni muhimu, mnaweza kum encourage like kumwambia anaweza kuwa beta than condition aliyo nayo.
 
Kabanga! pole tu! huna neno jingine la kunisaidia kuhusu hili? Asante

ndugu hili ni tatizo, samahani wacha nichukue nafasi yangu ya ualimu.
Mko mbali na mdogo wenu, hii ndio sababu kubwa sana, mwapasa kuwa nae karibu hata aikiwa huko shule ya bwalo.
tatizo lenu wazazi na walezi mnatuachia sana walimu kazi za malezi yote, kwa maana wewe ukishalipa ada eti umemaliza wajibu wako, lah, hapana kabisa kupitia kwa mwalimu waweza kuwa karibu sana na mdogo/mtoto wako, nasiku hizi mashule mengi yameweka siku za kuwatembelea watoto/wanafunzi tumia nafasi hiyo mzazi/mlezi, waweza jua mengi ya kijana wako kimaendeleo kiafya, kitaaluma n.k
Natumaini utakuwa umenielewa, vinginevyo uliza nitakusaidia...
 
Asante sana. Ziko wapi hizo rehab?. Unaweza kujua gharama zake?

Ngoja nikuangalizie then nitakupa na contacts zao.. Kuacha inawezekana sana.. Wako wengi ambao wameacha japo bado kuna wengine wali-relapse.. But inategemea na familia iliyokuzunguka..
 
ndugu hili ni tatizo, samahani wacha nichukue nafasi yangu ya ualimu.
Mko mbali na mdogo wenu, hii ndio sababu kubwa sana, mwapasa kuwa nae karibu hata aikiwa huko shule ya bwalo.
tatizo lenu wazazi na walezi mnatuachia sana walimu kazi za malezi yote, kwa maana wewe ukishalipa ada eti umemaliza wajibu wako, lah, hapana kabisa kupitia kwa mwalimu waweza kuwa karibu sana na mdogo/mtoto wako, nasiku hizi mashule mengi yameweka siku za kuwatembelea watoto/wanafunzi tumia nafasi hiyo mzazi/mlezi, waweza jua mengi ya kijana wako kimaendeleo kiafya, kitaaluma n.k
Natumaini utakuwa umenielewa, vinginevyo uliza nitakusaidia...

Ni kweli uko sahihi kabisa. Ila sasa nini kifanyike ili arudi normal? endelea kusaidia mwalimu usiwe na hasira ya kuachiwa mzigo wa kulea.
 
Kuna hosp. Tanga inaitwa rutindi ni nzuri au rehab kwa hapa bongo sijui ipi nzuri.

ila hutaweza kumsaidia bila yeye kuwa tayari kuacha kutumia hayo madawa! Mkilazimisha treatment atatulia then atarudia tena! Ni vizur mkampa couselling had akubal kuacha ndio apate treatment.

kumpeleka shule mbali anaweza akasababisha matatizo mengne..kama ameshaanza udokoz ataibia wenzake akasake unga popote na hyo inaweza leta matatzo kwenu.

counselling ni muhimu, mnaweza kum encourage like kumwambia anaweza kuwa beta than condition aliyo nayo.

Asante. umesema Lutindi iko Tanga? ni nitaitafuta. Nashukuru.
 
Mkuu hakuna mvuta unga aliekolea ambae aliacha kwa kuambiwa tu aangalie wenziwe au kutengenezewa mazingira ya ku-regret.. In case kama hufahamu Mkuu.. starehe ya utumiaji wa madawa ya kulevya na haswa cocaine na heroin unakuwa mwanzo tu wakati unapoanza kutumia.. Unakuwa unajisikia hali fulani ya ecstasy hivi.. Ila baadae sasa inabadilika na kuwa kama tiba.. Anapoyakosa madawa mtumiaji anakuwa na maumivu mwilini ambayo mwisho wa siku anashindwa kuyavumilia.. Hali hiyo inapelekea mpaka kuwa wagonjwa kabisa wenyewe wanaita alosto.. Wanapokuwa kwenye hali hiyo wanaweza kufanya lolote (hata kuliwa tigo) mradi wapate dawa ili wadevele..

Ushauri wangu kwa happiness win ni kutafuta rehab clinics ambazo wataweza kumsaidia mdogo wake..

Mkuu naijua arosto na side effects zake kama kuumwa mwili mzima,kutapika,kuhara et al

ila tambua hata rehab watu wanatibiwa kwa hayo hayo madawa sema kwa kipimo maalum..na arosto unaweza kunywa kahawa au kuna special chewing gum unaweza kutuliza na kama c mteta mzoefu unaweza kumaliza tatzo mwenyewe tu bila rehab.

ila kwa teja mzoefu kama hana nia ya kuacha hawez acha kwa kumlazimisha kwenda rehab, atapimiwa unga rehab kwa interval na atakuwa fresh ila akirudi uraian ataendelea kuji boost to the maximum.

kikubwa ni mtu kuwa tayari kwanza kuacha uteja ndio asaidiwe kupata treatment.
 
Last edited by a moderator:
pole sana mkuu,dawa ya madawa ni kumpeleka kwenye REHABILITATION CENTERS ndio kuna tiba huko tena ASAP maana namna utavyomchelewesha kupata tiba ndio atakavyokua nguli wa madawa,ATAPONA NA KUACHA TU.
 
Matibabu yake hata kama ataenda rehab inabidi kuwa nae karibu sana na kumpa upendo wa karibu kama ndugu yenu.
Tatizo kubwa la watumiaj wa unga ni kukosa support hasa baada ya wao kuwa wameacha shughuli zote zihusianazo na madawa.
Society haiwapi tena second chance ndo maana mwisho wake wanaishia kurudi kutumia tena because of frustrations wanazokutana nazo katika day to day life. hili ndo hasa tatizo lililomkuta Langa hata umauti.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom