Msaidieni mdogo wangu

happiness win

JF-Expert Member
Joined
Aug 30, 2011
Posts
2,461
Reaction score
1,394
Naomba msaada wenu; tumegundua mdogo wangu kabisa anatumia madawa ya kulevya. Shule ameacha kumbe toka januari mwaka huu hajakanyaga shule huku sisi tukijuwa yuko shule bording na ada tumeshalipa. Ameshakuwa mwizi anapita kwa ndugu na kuiba vitu kama simu na pia anatapeli ametumwa na kujipatia pesa.

Ninachoomba ni msaada wa mawazo tufanyeje? je tumpeleke hospitali? wapi? atatibika? tumpe dawa gani? tumfanye nini aache madawa? Tafadhali naomba mawazo yenu maana hili limenichanganya sana.
 
Anatumia madawa gan huyo dogo?

kuna hospital special kwa ajil ya victims wa drugs au rehabs.

but kabla hamjafikiria kumpeleka kwenye matibabu ingefaa mkae nae na muongee nae kwa kirefu. Kujua ni kwanin alianza kutumia madawa pia mjue kama anajutia kuacha shule na kupoteza future yake.

pia mumpe mifano ya marafik zake wa utotoni wenye mafanikio mazuri shuleni. Cha msingi mnatakiwa muongeenae kwa upole na upendo huku mukimtengenezea mazingira ya ku regret tabia yake ya kutumia madawa.

akisha regret atakuwa tayar kuacha na hapo ndo mumpeleke rehabs au hospital kwa matibabu,uangalizi na ushauri zaid.
 
Ukipata tiba mtafute na anae muuzie umkamate maana ataendelea haribu wengine
 
Pole sana
ngoja nitakupa namba
 
ana umri gani?

ana miaka 18. Yeye anadai anavuta bangi tu, lakini tunahisi sio kweli maana analegea na kuzubaa sana. Ametafuna vidole vyote vikucha vimebaki ... sijui nisemeje... inaniuma nimtazamapo
 
ana miaka 18. Yeye anadai anavuta bangi tu, lakini tunahisi sio kweli maana analegea na kuzubaa sana. Ametafuna vidole vyote vikucha vimebaki ... sijui nisemeje... inaniuma nimtazamapo

aisee pole sana, naweza imagine maumivu mnayo yapitia. Bado mdogo hivyo msichelewa hata lisaa limoja kutafuta huduma na tena kama mkiweza mpelekeni seminary ya mbali (maporini) ambapo hapajachakachuliwa na miunga.
 
anatumia sembe/unga au anavuta bange?
 
aisee pole sana, naweza imagine maumivu mnayo yapitia. Bado mdogo hivyo msichelewa hata lisaa limoja kutafuta huduma na tena kama mkiweza mpelekeni seminary ya mbali (maporini) ambapo hapajachakachuliwa na miunga.

Asante Ndugu yangu. Sio siri ananiumiza mno. Tumeshafanya kila jitihada na kashahama shule kibao lakini stage aliyofikia sasa ndio tunastuka kumbe kashakuwa teja kabisaaaa!. yaani we acha tu....
 
Hili ni janga kwa kweli.......mimi sina cha kusema hapa......kama mmegundua muwahini tu......atatibika.....sisi tuna wetu..... imekuwa mbaya.....rehab amekaa lakini akitoka ni anaanza moja......(yupo UK)......ki ukweli tumekata tamaa......
 
mmmmh kweli hili janga.... lisikie tu kwa mwenzio likija mlangoni mwako linauma sana.
 
Asante kwa ushauri wako. Huyu Bwana mdogo amekuwa zoba kabisaaa, yaani tumeshakaa naye hana la maana analoongea zaidi ya kusinzia na kutoa udenda. Yaani unaweza kuongea naye mwenzio anainamaaa tu hadi analala, ila anadai yeye hajala madawa zaidi ya bangi. muonekano wake ni madawa tu yamemjaa akilini, na ameanza kuiba vitu na pesa nyumbani, kwa ndugu na majirani. Sijui nimpeleke hospitali gani?
 
Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…