Msaidie Mdogo wetu Tafadhari | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Msaidie Mdogo wetu Tafadhari

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by lumange, Jul 6, 2011.

 1. l

  lumange Member

  #1
  Jul 6, 2011
  Joined: Jul 6, 2011
  Messages: 14
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  [FONT=&quot]Habari zenu wana jamii forum,[/FONT]
  [FONT=&quot]Mimi nimetumwa kwa niaba ya familia yetu nijiunge humu ili kunusuru ndugu yetu aliye katika hatari ya kupoteza maisha.[/FONT]
  [FONT=&quot]Mkasa wenyewe uko hivi;[/FONT]
  [FONT=&quot]Tuna mdogo wetu aliyevushwa na Dada mmoja kwenda Kenya kumfanyia kazi za ndani. Baada ya kufika huko wakakorofishana na huyo Dada akamfukuza huyo ndugu yetu bila kumpa nauli ya kurudi huku Tanzania.[/FONT]
  [FONT=&quot]Sisi kama ndugu tumejaribu kufuatiria kwa jamaa yake na huyu Dada anayeishi hapa Dar es salaam, lakini akatukatisha tamaa kwa kutuambia kuwa huyo Dada anamdharau sana hawezi kumwambia kitu akafanya, hivyo tutafute namna nyingine ya kumsaidia mdogo wetu. [/FONT]
  [FONT=&quot]Tukaona kupitia hapa pengine tunaweza kupata msaada, kwa kuomba mwenye uwezo wa kutuelekeza tunaweza kuchukua hatua gani ukizingatia kuwa sisi hatuna uwezo wa kufika Kenya kutokana na hali ya kiuchumi kuwa si nzuri. Je kuna hatua gani za kisheria zinaweza kutusaidia?[/FONT]
  [FONT=&quot]Ahsante kwa kusoma ombi letu.[/FONT]
   
 2. Smatta

  Smatta JF-Expert Member

  #2
  Jul 6, 2011
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 2,343
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Naomba unipe namba za huyo dada yako ili niweze kuwasiliana naye. unaweza kuni PM ili nimwongeleshe nijue ntamsaidia aje, nipo Kenya na najua naweza kumtoa alipo na kumrudisha nyumbani salama
   
 3. l

  lumange Member

  #3
  Jul 6, 2011
  Joined: Jul 6, 2011
  Messages: 14
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ahsante kwa kujitokeza kutusaidia

  Mdogo wetu hana simu ila huyo Dada aliyempeleka huko anazo simu ngoja nikamuombe huyu jamaa yake wa Dar akinipa nitaziweka hapa kwenye maelezo yangu.
  Ahsante tena sana kwa moyo wako mwema.
   
 4. Mulama

  Mulama JF-Expert Member

  #4
  Jul 21, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 2,458
  Likes Received: 710
  Trophy Points: 280


  Vipi jamani huyo mdogo wenu alipatikana au mmekosa msaada? tuwasiliane nitaangalia cha kufanya
   
 5. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #5
  Jul 22, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,096
  Likes Received: 6,559
  Trophy Points: 280
  Unakuja na hoja then unapotea jumla, jitahidi uwe na majibu bana.
   
 6. Mulama

  Mulama JF-Expert Member

  #6
  Jul 22, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 2,458
  Likes Received: 710
  Trophy Points: 280
  Yawezekana keshampata ndugu yake lakini inabidia ajulishe jf basi
   
 7. l

  lumange Member

  #7
  Jul 27, 2011
  Joined: Jul 6, 2011
  Messages: 14
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jamani sijampata ndugu yetu na wala sio kwamba nimeleta mada nikakimbia tatizo sina uwezo wa kuingia kwenye net cafe kila mara, pesa sina. Nilifuatilia kwa yule Baba kumuomba simu ya mwanamke wake akakataa kunipa ila nilipomwambia kuwa nimepata ushauri kupitia jamii forum akasema hata huyo mkewe ni mwanachama wa jamii forum tena mzuri sana!

  Kama ananisoma humu na yuko huko kenya tunamuomba aturudishie mdogo wetu kwa wema tu, wala sisi hatuna nguvu ya kifedha kupambana naye ni masikini sisi vinginevyo mdogo wetu asingekuwa mfanyakazi wake wa ndani kama tungalikuwa na uwezo.
   
 8. Aloysius

  Aloysius Member

  #8
  Jul 27, 2011
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 83
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Naomba siku nyingine usipitie hapa. Nenda polisi maramoja, hiyo inaanza kuchukua taswira ya jinai. Mshitakini huyo anayejiita ndugu yake wa hapa. NARUDIA: NENDA POLISI NI SWALA KUBWA!
   
 9. Mulama

  Mulama JF-Expert Member

  #9
  Jul 28, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 2,458
  Likes Received: 710
  Trophy Points: 280
  Mbona unamkatisha tamaa, nadhani huko Polisi atakuwa amekosa msaada ndio maana kaja jf, si unajua Polisi wetu bila pesa mambo hayaendi?! hasa pale unayeshindana naye kama anakuzidi mshiko!

  Cha msingi kama anasema huyo mhusika anasoma hii jf amsikilize kilio chake awarudishie huyo ndugu yao na au atutajie humu jina la huyo dada tusaidie kumueleza humu jamvini.
   
Loading...