Msaidie huyu dada hana elimu lakini ana experience

Kabaizer

JF-Expert Member
Oct 4, 2011
504
64
Jamani wakuu habari zenu poleni na majukumu ya hapa na pale.

Kuna dada amenifuata na kuniomba msaada na namfahamu kwa muda kidogo anatafuta kazi lakini kutokana na mimi kuwa na uwezo duni nimeona sio mbaya nikilifikisha kwenu wakuu ili mumsaidie japo hata kwa mawazo.

Huyu dada kusema kweli ni mzuri mpaka roho inauma,yeye mwenyewe anasema amewah kufanya kazi ya wakala ya mpesa na tigopesa, amewah kufanya kazi kama cashier kwenye minisupermarket, pia amewah kufanya kazi kama waitress kwenye hotel ya landmark.

Pia anasema anaweza akafanya kazi za ndani kwenda na kurud kwao kila siku,ila kwa bahat mbaya kinapokuja kigezo cha elimu anaachishwa kazi kwakua ameishia form four.

Mimi naweka uzi kama nilivyoagizwa kwa kua yeye cm hana kwa sasa mwenye moyo wa kumsaidia naomba amsaidie mimi nimeshindwa kwa kua ni mfanya vibarua tu na sina kazi ya maana,nawatakia kazi njema na mchana mwema.
 
ni sababu zipi zilimsukuma labda hadi akaacha sehemu zote hizo alizokuwa anafanya ? nn labda kilitokea. watu wajue kwanza hapo
 
ni sababu zipi zilimsukuma labda hadi akaacha sehemu zote hizo alizokuwa anafanya ? nn labda kilitokea. watu wajue kwanza hapo

Jaman wakuu habar zenu poleni na majukumu ya hapa na pale
jaman ndugu zangu kuna dada amenifuata na kuniomba msaada na namfaham kwa muda kidogo anatafuta kazi lakini kutokana na mimi kuwa na uwezo duni nimeona sio mbaya nikilifikisha kwenu wakuu ili mumsaidie japo hata kwa mawazo,huyu dada kusema kweli ni mzuri mpaka roho inauma,yeye mwenyewe anasema amewah kufanya kazi ya wakala ya mpesa na tigopesa,amewah kufanya kazi kama cashier kwenye minisupermarket,pia amewah kufanya kazi kama waitress kwenye hotel ya landmark,pia anasema anaweza akafanya kazi za ndani kwenda na kurud kwao kila siku,ila kwa bahat mbaya kinapokuja kigezo cha elimu anaachishwa kazi kwakua ameishia form four,mimi naweka uzi kama nilivyoagizwa kwa kua yeye cm hana kwa sasa mwenye moyo wa kumsaidia naomba amsaidie mimi nimeshindwa kwa kua ni mfanya vibarua tu na sina kazi ya maana,nawatakia kazi njema na mchana mwema

Hukusoma hapo?
 
Jaman kama unamawazo hasi kuhusu mimi au huyo mdada unaweza kuongea lakin kusema kweli sina hata dalili za utapeli naridhika na kile mungu alichonijaalia
 
Form Four anaachishwa u housegirl na mpesa? Wanataka form ngapi? Hebu sema ukweli. Naona kama taarifa zako zina UTATA.

Umewaza kama nilivyowaza, kwa elimu ya 4m four hizo kazi zote alizotaja anafiti sasa sijui yeye anatatizo gani zaidi.
 
Kifupi kwamba elimu ndio tatizo kubwa na pili sehemu hizo zote alizofanya kazi kulikua na matatizo mbalimbali mfano,aliamua kuacha kazi ya wakala kwa kua kila mwisho wa mwezi alikua anakatwa mshahara kwa madai ya shoti ambazo mwenyewe anadai hazina ukweli,kazi ya hotel baada ya hotel kua na jina kubwa waliwapiga chini wafanyakazi wote wenye elimu ndogo na kuajiriwa wenye elimu ya fani hiyo,na kazi za ndani aliacha kwa kua bosi wake alikua akimtaka kimapenz ndio maana kwa sasa anahitaj sehemu atakayokua anaenda na kurud ili kuepusha migogoro ya familia,
 
Mkuu kuna kitu hakipo sawa mahali! Nashindwa kuelewa itakuwaje hadi mtu anaajiriwa na mwajiri anakuwa anajua kiwango cha elimu halafu anakuja kumtimua mbeleni!! Kwa vyovyote kuna tatizo ambalo labda dada mwenyewe hajijui,mvivu au jingine ambalo kakuficha hata wewe!
 
yote yanawezekana mkuu nisimkingie kifua sana inabid atakaemsaidia aongee nae kiundani zaid na aangalie utendaj wake wa kazi
 
Mkuu kuna kitu hakipo sawa mahali! Nashindwa kuelewa itakuwaje hadi mtu anaajiriwa na mwajiri anakuwa anajua kiwango cha elimu halafu anakuja kumtimua mbeleni!! Kwa vyovyote kuna tatizo ambalo labda dada mwenyewe hajijui,mvivu au jingine ambalo kakuficha hata wewe!

Lakini mtu kuachishwa kazi kwa sababu ya elimu ndogo baada ya ofisi kukua lipo.
 
ana umri gani?...
hebu kama umri unaruhuru mwambie akasome hata ufundi veta, akisomea umeme au welding si mbaya kigezo tu cha kuwa mwanamke kitamfanya akubalike
 
ana umri gani?...
hebu kama umri unaruhuru mwambie akasome hata ufundi veta, akisomea umeme au welding si mbaya kigezo tu cha kuwa mwanamke kitamfanya akubalike

sawa mkuu ujumbe wako umefika nitamshauri
 
Back
Top Bottom