Msafara wa magufuli waacha gumzo

Msafara wa magufuli waacha gumzo

jjimmy.jjose

Member
Joined
Dec 12, 2012
Posts
35
Reaction score
4
Wajameni ndo kusema watu wa kanda ya ziwa wanamthamini mtu huyu kwa nafasi ya juu kabisa (Urais) hata kabla ya uchaguzi 2015 ?

Story nzima hapa chini, kazi twende!

MSAFARA wa Waziri wa Ujenzi, John Mgaufuli umeacha maswali jijini Mwanza baada ya kuwa na magari 26,viongozi mbalimbali wa mkoa na kusindikizwa na kuongozwa na pikipiki inayoongoza msafara wa viongozi wa kitaifa akiwa Rais.

Magufuli ambaye alikuwa katika ziara ya kikazi mkoani Mwanza kwa ajili ya kuangalia barabara ya kutoka uwanja wa Ndege kwenda Igombe ambayo inapaswa kufungwa kupisha ujenzi wa upanuzi wa uwanja wa ndege wa Mwanza, mbali na kusindikizwa na gari la kamanda wa polisi wa mkoa, pia kila alipopita kulikuwa na askari wa usalama barabarani ambao walikuwa wakizuia magari kuruhusu msafara wake kupita.

Msafara huo ulianzia ofisi ya mkuu wa Mkoa wa Mwanza na kuelekea Igogo saa 3:14 asubuhi kwa ajili ya kukagua ujenzi wa barabara zilizojengwa kwa mawe, kwanza ulitanguliwa na pikipiki ya Jeshi la Polisi iliyokuwa ikisafisha njia na kufuatiwa na gari la Kamanda wa Polisi ambalo lilikuwa limewasha taa na kufuatiwa na gari la Mkuu wa Mkoa wa Mwanza na nyuma yake gari la Waziri Magufuli na kisha magari mengine ambayo idadi yake ilikuwa zaidi ya 26.

Mbali na kutanguliwa na magari, pikipiki hiyo ya king’ora pia katika makutano ya Barabara ya Nyerere na Bungando walikuwa wameandaliwa askari wa usalama barabarani kuzuia magari ili msafara huo kupita pamoja na njia nyingine zinazoingia katika barabara hiyo.

Source : Mwananchi, 12 January 2013
 
  • Thanks
Reactions: RR
Namfagilia sana huyo bro na kama anataka upresidaa anastahili mpeni.
 
Arudishe kwanza nyumba za SERIKALI alizogawa kama Pipi kwa wenzake na yeye akajigawia.

we unafikiri alifanya kwa uwezo wake ndugu yangu. nyumba za wenyewe zile na hawez fanya chochote coz washika dau wakubwa wapo tuu kimyaa. yan hapa kama ikiwezekana kumpata kiongozi wa upinzani huenda zikarudi hizo nyumba
 
Jamani tukiacha majungu huyu Bwana anastahili kuchukua Urais wa nchi hii kama tunahitaji Tanzania ipone. Kwa Upande wa CCM hana Mpinzani. Wengine porojo tuu. Tunahitaji mtu kama Magufuli awe rais wa nchi hii. Ni Magufuli pekee ambaye anaweza kupambana na Dr Slaa. CCM wasipomteua Magufuli, Slaa hana Mpinzani. Heko Magufuli.
 
Hata Chekechea ukiwaambia eti hiyo ndiyo SABABU basi watakucheka.
we unafikiri alifanya kwa uwezo wake ndugu yangu. nyumba za wenyewe zile na hawez fanya chochote coz washika dau wakubwa wapo tuu kimyaa. yan hapa kama ikiwezekana kumpata kiongozi wa upinzani huenda zikarudi hizo nyumba
 
Wajameni ndo kusema watu wa kanda ya ziwa wanamthamini mtu huyu kwa nafasi ya juu kabisa (Urais) hata kabla ya uchaguzi 2015 ?

Story nzima hapa chini, kazi twende!

MSAFARA wa Waziri wa Ujenzi, John Mgaufuli umeacha maswali jijini Mwanza baada ya kuwa na magari 26,viongozi mbalimbali wa mkoa na kusindikizwa na kuongozwa na pikipiki inayoongoza msafara wa viongozi wa kitaifa akiwa Rais.

Magufuli ambaye alikuwa katika ziara ya kikazi mkoani Mwanza kwa ajili ya kuangalia barabara ya kutoka uwanja wa Ndege kwenda Igombe ambayo inapaswa kufungwa kupisha ujenzi wa upanuzi wa uwanja wa ndege wa Mwanza, mbali na kusindikizwa na gari la kamanda wa polisi wa mkoa, pia kila alipopita kulikuwa na askari wa usalama barabarani ambao walikuwa wakizuia magari kuruhusu msafara wake kupita.

Msafara huo ulianzia ofisi ya mkuu wa Mkoa wa Mwanza na kuelekea Igogo saa 3:14 asubuhi kwa ajili ya kukagua ujenzi wa barabara zilizojengwa kwa mawe, kwanza ulitanguliwa na pikipiki ya Jeshi la Polisi iliyokuwa ikisafisha njia na kufuatiwa na gari la Kamanda wa Polisi ambalo lilikuwa limewasha taa na kufuatiwa na gari la Mkuu wa Mkoa wa Mwanza na nyuma yake gari la Waziri Magufuli na kisha magari mengine ambayo idadi yake ilikuwa zaidi ya 26.

Mbali na kutanguliwa na magari, pikipiki hiyo ya king'ora pia katika makutano ya Barabara ya Nyerere na Bungando walikuwa wameandaliwa askari wa usalama barabarani kuzuia magari ili msafara huo kupita pamoja na njia nyingine zinazoingia katika barabara hiyo.

Source : Mwananchi, 12 January 2013
Labda future president of Kenya alikuwepo, jamaa ni marafiki
 
Ukifika wakati wa kuchagua mgombea Urais kwa tiketi ya CCM. Mkutano mkuu wa Taifa utashangaza wengi hasa wale wanaofikilia itakuwa ni EL au Membe

.Kuna uwezekano huyu jamaa akawa ndiye mtu wao na kama itakuwa sivyo, basi atakuwa kwenye upande wa mwakyembe.

.kila kukicha inaonekana hivyo kutokana na mwelekeo ndani ya CCM
 
Hii safari ya kuutaka Urais 2015 ni ngumu mno ndani ya CCM nafikiri kuliko hata itakavyokuwa kwa vyama vya Upinzani.
Kuna kila namna ya vikumbo ndani ya Chama Tawala,kila mtu anautaka Urais.....Siipendi CCM kwa sababu imeshindwa ku-deliver kwa kipindi chote cha miaka 36 (tokea 1977) Ilipokuwa madarakani kama CCM.Sitaki kuamini kwamba itakuja kubadilika,imefika wakati sasa,tutafute Chama mbadala kinachokubalika na wengi tuwape kura zetu.

Kuna fununu ndani ya CCM kuwa Lowasa,Membe,Migiro,Nchimbi,Magufuri,Sita,Mwinyi,Sumaye,Mwakyembe na hata Prof.Mwandosya kama sio wao basi washabiki wao wanawaambia mnafaa kugombea Urais.Nafasi hiyo ya Juu ya madaraka nchini imeshuka thamani kwa kiwango kikubwa baada ya kuonekana hata Kikwete ameiweza.Nimeogopa kwa kiwango kikubwa baada ya kuona hata Nchimbi anaunganishwa katika kinyang'anyiro hicho cha uongozi wa juu wa Nchi.

Imefika wakati sasa wagombea wa nafasi ya Urais waangaliwe Wamefanya nini kabla ya kugombea nafasi hiyo kubwa na muhimu kwa Uongozi wa Nchi.Sifa za kuomba kazi hiyo ziwekwe bayana.Kwa mwendo huu tunaokwenda,tutakuja kupata Rais mwendawazimu au mtu asie Mtanzania asilia kutuongoza Nchini.Tujiwekee viwango vya nani wa kugombea nafasi hiyo.Kiongozi aliyekwisha kushindwa katika idara au Wizara alizoongoza asipewe nafasi ya kuomba nafasi hii ya Urais,tusitarajie kuona mtu kashindwa/kaboronga huko Fedha,Viwanda,Maliasili na Nje alikopitia atakuja kuweza akiwa Rais.
 
Namfagilia sana huyo bro na kama anataka upresidaa anastahili mpeni.

Magufuli ndo yule aliyewatukana wakazi wa Kigamboni na kukataa kuomba radhi, atawatumikia watu gani mtu mwenye kujisikia yeye ni yeye tu, katika uongozi hapo amepwaya sana. Atabaki kubahatisha nafasi za kuteuliwa lakini upresida utabaki njozi iliyopotea.
 
Aslan,abadan!Hatufai katu hata kwa uwaziri.Anajaribu kuvaa viatu lakini anapwaya,tatizo tulilo nalo kubwa ni kwamba tuna uhaba sana wa watendaji makini ndo sababu watu wanamwona huyu mbululu kama mfano wa kuigwa.********(labda awe rais wa nation housing huyu kenge)alishindwa kuondoa ufisadi hadi leo nyumba zetu zimejaa maponjoro na mabwanyenye.Ole wake nae siku yake itafika.
 
Back
Top Bottom