Msafara wa Kikwete jioni hii wazuia ambulance maeneo ya Mbezi Luis | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Msafara wa Kikwete jioni hii wazuia ambulance maeneo ya Mbezi Luis

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by regam, Jun 26, 2011.

 1. regam

  regam JF-Expert Member

  #1
  Jun 26, 2011
  Joined: Jan 4, 2011
  Messages: 268
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Niko maeneo ya mbezi magari saba kuna gari ya wagonjwa inamuwahisha mgonjwa toka tumbi. Mara msafara wa kikwete ukatokea na kuamuru ambulance hiyo ipaki pembeni.
  Jambo hili limetusikitisha sana kwa kitendo hiki ukichukulia gari inawahi kunusuru uhai wa mgonjwa.
  Kwa hiyo ina maana kwamba bora mgonjwa afia zake mbali. Inasikitisha sana!
   
 2. Rejao

  Rejao JF-Expert Member

  #2
  Jun 26, 2011
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 9,239
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Raisi anapewa first priority!
   
 3. Mzalendo80

  Mzalendo80 JF-Expert Member

  #3
  Jun 26, 2011
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 2,385
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  Huyu ni bora awe nje ya nchi kuliko akiwa humu nchini kuna kuwa na matatizo mengi tu, uhai wa mtanzania kwake sio muhimu kuliko safari yake sio. Huu ni upuuzi kabisa watu kama hao ndio wakupiga risasi na kuondokana nao kabisa wakiwepo ndio wanaliongezea taifa letu matatizo
   
 4. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #4
  Jun 26, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,011
  Likes Received: 1,816
  Trophy Points: 280
  Mkuu tuangalie mambo kwa macho mawili. Hivi hapa Rais ana matatizo gani? Rais angejuaje kama kuna ambulance inampeleka mtu hospitali? Yeye anapita kuna watu wanasafisha njia na hao watu ndio wameizuia ambulance ili Rais apite na si Rais amesema zuia hiyo ambulance nipite. Lawama hizi zinatakiwa zielekezwe kwa traffic Police. Hizi ni chuki tu kwa Rais
   
 5. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #5
  Jun 26, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Hapo ndipo ambapo naona bora kumtetea shetani hata kama malaika watanipinga. Hivi kwenye msafara ule Kikwete anajua nini kinachoendelea mbele yake? Kwani hao polisi siwanaweza kuwasiliana na muongoza msafara ili usubiri ambulance ipite? Kwa hapa Kikwete tunamwonea, tuwalaumu polisi waliosimamisha gari la wagonjwa ili kumuwahisha Rais ambaye ni mzima.
   
 6. I

  IPECACUANHA JF-Expert Member

  #6
  Jun 26, 2011
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 2,125
  Likes Received: 290
  Trophy Points: 180
  Ni wazi kwamba uwezo wa utendaji kazi wa polisi wetu ni wa Kama robot. Lakini tusilaumu sana wakati ni ukweli ulio wazi kwamba polisi wengi ni Kati ya wale walioshindwa shuleni kwa hiyo wanaendeleza "nguvu badala ya akili". Yaliotokea ni uthibitsho.
   
 7. Kichwa Ngumu

  Kichwa Ngumu JF-Expert Member

  #7
  Jun 26, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 1,726
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Heshima itarudi tuu ngoja
   
 8. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #8
  Jun 26, 2011
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  Police wa Tz ni heri ukumbane na robot !
   
 9. Mzee wa Rula

  Mzee wa Rula JF-Expert Member

  #9
  Jun 26, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 8,177
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  avatar30990_5.gif.jpg
  Kichwa ngumu vipi mkuu na hiyo avator yako, back to the topic ingebidi hiyo ambulance ibwebwe kwa kuwekwa nyuma ya msafara wa JK ili ipewe tafu kufika haraka huko iendako. Pia kuna kasumba ya madereva wa ambulance wakiona foleni basi huwasha king'ora kwa ninajili ya kukwepa foleni tofauti na matumizi ya hicho king'ora.
   
 10. I

  Ismaily JF-Expert Member

  #10
  Jun 26, 2011
  Joined: Jun 19, 2011
  Messages: 357
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Bora awe anakaa hukohuko nje ya nchi,akishakuwa humu ndani Tanzania kero tupu,TANZANIA haina RAIS,KIKWETE MABANGONI,DR SLAA MIOYONI MWETU.
   
 11. pascaldaudi

  pascaldaudi JF-Expert Member

  #11
  Jun 26, 2011
  Joined: Mar 25, 2009
  Messages: 534
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Tatizo hapa ni traffic kufanya kazi kwakuogopa, nani yupo tayari kufukuzwa kazi? maana ukiruhusu tu ambulance na wakuu wakaona basi ujue utajitetea ukiwa umefukuzwa kazi kwanza. Kwa ufupi sheria zetu ni mbovu, nchi zilizoendelea kuna njia maalumu za taxi, bus na ambulance.
   
 12. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #12
  Jun 26, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,011
  Likes Received: 1,816
  Trophy Points: 280
  Mkuu hapa sasa ndio umesema kitu. Tuna matatizo ya miundombinu. Hata kama si Rais kupita tumekuwa tukiona ambulance zinakwama kwenye foleni hapa Dar. Tena afadhali kama wangeiweka hiyo ambulance nyuma ya msafara wa rais hapo ambulance ingekuwa na uhakika kwa kufika ilikokuwa inaenda kama ni njia moja na msafara kuliko kuiacha ambulance ipige king'ora ikifika kwenye jam nayo ina jam. Mimi Kwangu sioni sababu ya kumlaumu Rais.
   
 13. mashikolomageni

  mashikolomageni JF-Expert Member

  #13
  Jun 26, 2011
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 1,565
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Kama walikuwa na mgonjwa kweli? Maana hiyo ni assumption tu
   
 14. Mtanzania haswa

  Mtanzania haswa JF-Expert Member

  #14
  Jun 26, 2011
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 665
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  wakati nikiwa driving school mwalimu wangu aliniambia ni ambulance pekee inayoweza kukatiza msafara wa rais, sasa hawa traffic sijui hawalitambui hili?
   
 15. P

  Popompo JF-Expert Member

  #15
  Jun 26, 2011
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 411
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  umesema yote mkuu!raisi si mtu makini hata kidogo lakini kwa hili hana pa kulaumiwa!traffic police ndo wanatakiwa kuondoa utamaduni wa akili za kushikiwa wawe na maamuzi sahi,walipaswa kukagua kwa haraka hiyo ambulance wakati huo wanawasiliana na wenzao wa upande wa pili dhen wanairuhusu na naamini raisi hatakuwa na malalamiko!TUACHE KULALAMA
   
 16. g

  gasper2 Member

  #16
  Jun 26, 2011
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 38
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Mkuu Kimbunga, kama ni kuangalia mambo kwa macho mawili, jamaa katoka bagamoyo kwenye arobaini, unaona ni sawa kwa raisi kuacha mambo ya maana na kuanza kukimbizana na arobaini??? anaweka foleni kwa shuguli ambazo hazina tija. Leo unazani Obama akitaka kwenda kenya kwenye arobaini, state ya amerika itamruhusu?? lazima tuwe na viongozi serious
   
 17. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #17
  Jun 27, 2011
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  Hivi wee vipi?si akae ikulu anatembea tembea kwenda wapi utadhani muuza maji bwana kutwa barabarani!!
   
 18. Mzizi wa Mbuyu

  Mzizi wa Mbuyu JF-Expert Member

  #18
  Jun 27, 2011
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 5,497
  Likes Received: 1,061
  Trophy Points: 280
  Ilikuwa ni makosa kuisimamisha anbulance na ninajua kwenye msafara wa rais magari yana kaa sana foleni! Maskini mgonjwa yule!
  Hii haikubaliki, utengenezwe utaratibu raisi asisumbue wagonjwa! Na huenda alikuwa anakwenda safari isiyo na maana yoyote!
   
 19. G

  Gurtu JF-Expert Member

  #19
  Jun 27, 2011
  Joined: May 15, 2010
  Messages: 1,202
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Watanzania kweli ni watu wasioeleweka. Ni kweli rais hajui kinachofanyika? Je, kuna haja gani kuwa mkuu wa nchi kama hana watu wa kumpa taarifa. Ujue rais ni taasisi, hivyo hatumwangalii yeye kama mtu mmoja yaani JK. Je, tunataka kusema wezi wa EPA hawafahamu?

  Kwa kifupi hayo yanafanyika kwa ajili yake na kwa ridhaa yake. Tusidanganyane katika hilo. Polisi hawakuwa na busara kwa sababu aliye juu hana hiyo busara na wametenda alivyotaka rais atendewe.
   
 20. Consigliere

  Consigliere JF-Expert Member

  #20
  Jun 27, 2011
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 8,040
  Likes Received: 7,483
  Trophy Points: 280
  Kuna watu ni wa kuwaangalia na kuwaacha tu kama walivyo, wenyewe kila wanapoona,kupokea au kusikia jambo huwa wanakuwa na mchakato mwingine vichwani mwao, na huu ni mchakato wa kujiandaa kulaumu.
  Sasa katika hili ni vipi rais analaumiwa kwa lipi? Pia muanzisha uzi ameongelea ambulance bila kuonglea ilikuwa katika mazingira gani.....ambulance inaruhusiwa kutembea barabarani hata kama haina mgonjwa/wagonjwa, so inawezekana kabisa ilikuwa na shughuli nyingine. Tuache uvivu wa kufikiri na pia tuwe na moyo mgumu na wa kiungwana ili tuwe kuuona ukweli na kuukubali
   
Loading...