Mfumuko wa bei wapanda kwa asilimia 1.4

WilsonKaisary

JF-Expert Member
Apr 4, 2017
392
946
Kiwango cha mfumuko wa bei nchini kimepanda kwa wastani wa 1.4 kutoka asilimia 5 ilivyokuwa mwezi Februari hadi asilimia 6.4 kwa mujibu wa taarifa kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu nchini (NBS).

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, baadhi ya sababu zilizochangia ongezeko hilo ni kupanda kwa bei za bidhaa za vyakula na zisizo za vyakula ambapo vyakula vilivyopanda bei ni pamoja na mchele, sukari, unga wa mahindi, mtama, ndizi pamoja na mihogo mibichi.

Kufuatia ongezeko hilo, baadhi ya wakazi Jijini Dar es Salaam wametoa maoni yao na kutaja ukosefu wa kipato kuwa unaongeza ugumu wa maisha hasa kwa wafanyabiashara ambao wamelalamikia upungufu wa wateja sambamba na ushauri wa hatua za kuchukua kukabiliana na hali hiyo.

Chanzo: EATV
 
unga wa sembe kilo unakaribia elfu mbili..kwa hali hii maskini watapona kwel??
Wewe inaonyesha huishi Dar , nakama uko dar basi uko katika hali nzuri, huwa unanunua kiroba kizima. Unga dukani tunauza 2000 tshs @ kg.1. Mpaka wiki ijayo wanyonge wa rais wa wanyonge watanunua unga kwa 2200/=.(Veterinary/TAZARA)
Wananchi walipima maji kwa mguu, wamezama.
 
Wewe inaonyesha huishi Dar , nakama uko dar basi uko katika hali nzuri, huwa unanunua kiroba kizima. Unga dukani tunauza 20000 tshs @ kg.1. Mpaka wiki ijayo wanyonge wa rais wa wanyonge watanunua unga kwa 2200/=.
Wananchi walipima maji kwa mguu, wamezama.
sisi huku 1800@kg 1
labda huko wamewah kupandisha..
hslaf hapo elfu ishirini hiyo umekosea
 
Wewe inaonyesha huishi Dar , nakama uko dar basi uko katika hali nzuri, huwa unanunua kiroba kizima. Unga dukani tunauza 20000 tshs @ kg.1. Mpaka wiki ijayo wanyonge wa rais wa wanyonge watanunua unga kwa 2200/=.
Wananchi walipima maji kwa mguu, wamezama.
Kula ugali siku hizi ni bonge ya anasa!
 
Maisha yanazidi kuwa magumu hasa kwa wananchi wa kipato cha kati na chini...Hao wanasiasa hii taarifa wanaiangalia tu..hawana habari nayo...ikifika wakati wa kampeni utasikia "Naombeni kura zenu, nitawapunguzia ugumu wa maisha" Shabaaash
 
Huku pande za moshi unga kilo moja ni 2200, sukari kilo moja ni 3000 na mchele kilo moja ni shilling 2000 hebu tupia na wewe bei ya huko ulipo
 
Unga 1700,sugar 2800 pamoja na bei elekezi tuliyoahidiwa nadhan bora angeacha nchi iendelee kunajisiwa na majangili kwakua ilikua haiumiz hvi ila namudu kwakua tuko watu 5 ila balaa la mwaka ni gesi 54000 hii ni arusha
 
Nawasalimu ndugu wana JF,

Mimi ni mkulima nipo Kigoma vijijini nimevuna magunia yangu kumi yenye ujazo wa debe sita sasa huku nilipo bei iko chini sana yani debe in elfu 7000 nimeona itanikata sana nataka nisafirishe kamzigo kangu.

Nipeleke kati ya Dodoma au Dar

Wakuu mnaoishi katika mikoa hii naombeni mnijuze bei ya mahindi ili niwe na uhakika kabla sijajirusha.

Asanteni
 
Mdau mahindi yameshuka sana. Fanya hima uuze haraka kabla debe halijafika sh 4500
 
Wakuu main Beni mnijuze being ya mahindi gunia ujazo wa debesita huku kwetu kigoma kasulu bei ya debe no elf saba

Nimevuna gunia kumi nataka kusafirisha kwenda kati ya Dodoma au dare es salam plz niambieni bei wakuu mlio katika mikoa hii
 
Back
Top Bottom