msaada

marveljt

JF-Expert Member
Jan 11, 2017
1,503
1,479
Wakuu kwema?
Naomba kuelimishwa kidogo. Katika gari unaweza kubadilisha mfumo wa umeme kama betri ilikuwa n50 unaweza kutumia n90 na katika diff au engine unaweza kubadilisha,hat katika computer ram,processor, hdd pia zinabadilishwa
1. Je,kwenye simu unaweza kubadili ram?
2. Je kwenye simu unaweza kubadili storage yake
3. Je kwenye simu unaweza kubadili betri? Mfn. Kutoka 2000mah hadi 5000mah
4. Je unaweza kubadili body simu kutoka iPhone kwenya huawei
 
Storage sawa, ivo vngne ngoja waje...
 
battery unaweza kubadili, zipo extended battery kwa simu maarufu ambazo battery zake zinatoka.

cpu, ram storage na vitu vingi tu kama modem na radio za bluetooth vinakaa pamoja kwenye soc na havibadilishiki.

kubadili body huwezi, labda kwenye simu za kichina ambazo zinakuwa ni simu moja kasoro majina tu, sababu design za simu ni tofauti hazifanani baina ya manufacture mmoja na mwengine.
 
Sawa kivipi inamaana unaweza kutoa 4gb hadi 32 gb?
kwenye simu za android 6 kupanda kuna kitu kinaitwa adoptable storage ambapo unaeka memory card inaflashiwa na kuwa internal storage. mfano simu ina 8gb unaweza eka memory card ya 32gb ukachagua 16gb iwe internal na 16gb iwe external hivyo simu yako itakuwa na internal memory ya 24gb na memory card ya 16gb.

sema changamoto iliopo ni kwamba memory card nyingi zipo slow sana hivyo inaweza ikaifanya simu iwe slow nayo, na memory card zenye speed kubwa nazo ni gharama inaweza cost 50,000 hadi 100,000
 
Asante kaka, ila nina swali lingine, vipi kuhusu display inafaa kubadilishwa? Je, mikanda ya betri inaweza kuingiliana? Kuhusu circuit kutokuongiliana je sababu ua buton kupishana au nini
 
Asante kaka, ila nina swali lingine, vipi kuhusu display inafaa kubadilishwa? Je, mikanda ya betri inaweza kuingiliana? Kuhusu circuit kutokuongiliana je sababu ua buton kupishana au nini
display zinabadilishika ila mara nyingi inayokuja na simu ndio best za kubadilisha nyingi quality ni ndogo unless ununue inayotoka kiwandani.

hivyo vilivyobakia vinaingiliana kama design iliotumika ni moja, sana unakuta simu za kichina, ila kwa simu za manufacture wakubwa huwa mara nyingi haviingiliani.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom