D Metakelfin
JF-Expert Member
- Mar 23, 2017
- 3,197
- 3,333
Nina mama yangu mdogo anafanya biashara ya samaki huchukua bwawa la mtera na kwenda kuuza makambako lakini hivi karibuni amekumbwa na mikasa ya kukamatwa na askari wa Doria(sio maliasili).
Jana kwa mara ya pili walikamata gari aliyopanda(fuso) na kukagua mzigo tena hukagua kwa kuchana ovyo mzigo hivyo hupelekea uharibifu wa samaki wengi na walipokuta samaki hao wamewekwa pamoja na samaki wadogo(wasioruhusiwa) walikamata gari na kusema ielekee polisi na kudai samaki watapelekewa wafungwa(samaki wenyewe ni kama tenga mbili tu ukijumlisha wakubwa na wadogo) mpaka walipopewa laki mbili ndipo waliachia.
NAAMINI JAMII FORUMS KUNA WANASHERIA WENGI MACHACHARI NA NITASAIDIWA KADRI YA UWEZO WENU NA UTAALAMU WENU KISHERIA msaada nnaohitaji
==>Ninaweza kujitetea vipi nikikamatwa ili kuulinda mzigo wangu ikiwezekana samaki wakubwa waachwe wachukuliwe wadogo tu au waachwe wote
==>pdf inayohusu sheria ya samaki.
NB:kubwa zaidi ni jinsi ya kujitetea
Nawasilisha kwenu wakuu