Msaada wenu tena nipo njia panda

Msaada wenu tena nipo njia panda

unajishughulisha na nini .....unaonekana goal kipa wewe
 
habar zenu wakuu
Ni jumapili nyingine tulivu nikiwa nimejilaza ghafla nimeshtuka naanza kumuwazia kijana mmoja ambaye alinitokea kama mwaka mmoja na nusu uliopita ni mfanyakazi katka wizara moja nyeti jirani na ofisini kwetu

kipindi nakutana nae alikuwa na matatizo na mke wake akaniaproch nikamwambia nina mtu.basi tukawa kama marafiki mawasiliano yakaendelea japo haikuwa kivile mara chache akinieleza matatizo na mkewe na bla bla me nikawa namshauri asiachane na mkewe avumilie yatapita.

mwishoni mwa dec.mwaka jana akanitext wametalikiana. nikamwambia its fine ni maisha yenu. ikaishia hapo.

Nikiwa katika wakati huu ambao nimeachana na mwanaume wangu km two weeks ago nilikutana nae sehemu hatukuwa tumepanga tukasalimiana na stor mbili tatu akaniomba tuonane tuongee
( of course nilikuwa bored siku hiyo tukatoka ilikuwa jioni) tukakaa sehem tukaongeaaa the guy anadai ananipenda sana anataka tuwe wote nikamwambia nitamjibu.

Ukweli ni kwamba yuko so lovely,mtanashati educated yani ni mwanaume ambaye kila mwanamke akimuona atatamani kuwa nae mo than my x lakini kitu kimoja tu tukiwasilia
na kwenye simu hana maneno mengi, yan ni salam asubuhi, jioni na usiku mwema

(sijui ndivyo alivyo au ni kutokana na mazingra ya kaz yake au ni nini)Ila tukionana ataongea yote the way ananifil na nini na nini anafunguka.

sijampa jibu lakini nawaza sana huu ukimya wake ntawezana nae, nini kilisababisha waachane na mke ndani ya ndoa ya miezi 6?

kukaa more that 10hrs bila kuwasiliana na mtu nayempenda nitaweza?
Ama nakurupuka?

Matusi Hayatanijenga
kama unao ushauri nisaidie nipo njia panda natamani niwe na mtu kuwa alon kunaumiza sana,

HIVI NYIE FORM THREE MBONA MNAPODOJI SHULENI MNAPENDA KUCHAT BADALA YA KUJIANDAA NA MITIHANI??
 
Hujamkubali ndio maana hana mengi ya kuongea na ww maana hawez hata kukuita yale majina matamu km darling, Sweetheart, Honey/baby! n.k mkubali hizo issue ndogo mtafundishana.
 
Me nafikiri ukishamzoea mtu hakupi shida kbsa. We kama unaona sio mtu wa kuchat chat muache ndivyo alivyo husimbadilishe mtu akawa unavyotaka ww. Kama unampenda jitahidi kumzoea na ndipo mtakapoelewana, ukimmiss unampigia Unaongea nae unaridhika.
 
Mkubali mtajenga kitu kizur mwanaume hakosi majukum na anaweza akawa anakupenda ila wewe ukafikiri akupendi mvumilie ni mambo tu yake ya meenda kombo labda ndio inamuweka ivyo
 
Dah hiyo ratiba ya kuwasiliana kila mara mara na si chini ya masaa 10hrs ingenishinda hata mimi kusema kweli.... la muhimu muulize kwa nini waliachana mkewe na wewe mueleze kwa nini umeachana na mme wako...namba zikisomana basi ingieni Eden....
 
Kila jambo linawakati na mungu anamakusudi yake tena huenda huyu akawa mzuri kwako coz hakubani wala kukusumbua cku nzima anakupigia cm ami was ana jambo la msingi na kama anakusalimia bac we jua uko akilini mwake. Fanya uamuzi kabla hajafanya maamuzi mengine.
 
Anajali muda na ameupangilia, mara nyingi mtu anayetumia nguvu kubwa kufanya jambo fulani huwa nia yake si nzuri sana. Kama mkikutana anaongea mambo mengi ya msingi hamna tatizo cha muhimu ni kujua chanzo cha yeye kuachana na mkewe na ukiona sababu haina athari kwako basi kubali na myajenge vyema.
 
Mwambie unaomba umtembelee KWAKE........as ipi ingia mitini komaaaa nayee
 
Uzuri NI KWAMBA MAVETERAN wa X Relationship wakikutana hawatashidwani maana kila kitu kwao ni KIPORO. So go ahead mama
 
Huyo mtu unampenda? Ama ndio unatamani kuwa naye sababu he's lovely&mtanashati?

Ila mi nakushauri kama utaweza kujitahidi jitahidi tu kuwa alone hawa divorced wa kibongo bongo utajitafutia matatizo mengine makubwa tu

Naamini soon utapata ambaye hajawahi kuoa

Pambana
Mkuu wote n ma divorced huyu mleta Uzi na braza mtanashat & HB
Naweza kufananisha na kwny chemistry japo sipo deep sana
Ukichukua concentrated sulphuric acid then uka react na concentrated NaOH
Nathan kitakachotokea majibu unayo mheshimiwa
So achaa waoaneeeeeeee
 
Back
Top Bottom