msaada website hazifunguki | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

msaada website hazifunguki

Discussion in 'Tech, Gadgets & Science Forum' started by mnyamangeso, Sep 17, 2010.

 1. m

  mnyamangeso Member

  #1
  Sep 17, 2010
  Joined: Jun 27, 2010
  Messages: 33
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  naombeni msaada. siwezi kuaccess some websites kama za udsm,open university of tanzania na za baadhi ya vyuo vingine vya hapa tanzania,na leo nimejaribu kuaccess ya tra nayo nashindwa kufungua. i have tried several browsers but they failed. je tatizo linawezakuwa la my isp au kuna settings za kufanya kwenye machine yangu? other websites nafungua vizuri.
   
 2. MwanaHaki

  MwanaHaki R I P

  #2
  Sep 17, 2010
  Joined: Oct 17, 2006
  Messages: 2,403
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 145
  Ok. Hili ni swali zuri na la msingi.

  Kabla ya kuundwa kwa Tanzania Network Information Centre (TZ-NIC) ambayo sasa inasimamia Country-Top Level Domains (cTLDs), usajili na usimamizi wa cTLDs ulikuwa chini ya ndugu Bill Sangiwa, ambaye alikuwa anafanya kazi hii kwa kujitolea na kulipwa allowances na donor organisations, ili kumwezesha kutoa huduma hiyo. Sangiwa ndiye amewezesha kwa kiasi kikubwa TZ-NIC kuwa hewani, kwani alikuwapo wakati wote wa zoezi la kuhamishia usajili na usimamizi wa domain name hizi kutoka kwenye himaya yake hadi kwenye himaya ya TZ-NIC. (Hata hivyo hadi leo mchango wa Sangiwa haujatambuliwa na taasisi hiyo.)

  Kutokana na kwamba asasi nyingi za kielimu zilizoea kutolipia usimamii wa domain name zao, zilitarajia kwamba hata wakati wa TZ-NIC wangeendelea na utaratibu huo, hivyo hata pale ambapo TZ-NIC walipoanza kampeni yao ya kuwataka wamiliki wa domain name za .TZ waanze kuzilipia, wengi walizembea na hawakulipia.

  Ilipofika Julai 27, 2010, domain zote za .TZ ambazo zilikuwa hazijalipiwa zilikwisha muda wake (zili-expire), ukawekwa muda wa siku 30 za mwisho (grace period) kuzilipia. Lakini hazikulipiwa. Ndipo ilipofika Agosti 26, 2010, saa 1 jioni, domain hizo zikawa zimesitishwa kwenye himaya ya TZ-NIC. Wengi walihamaki na kwenda kulipia, lakini wengi bado hawajalipia, hivyo, bado mpaka sasa asasi nyingi hazionekani kwenye mtandao (Internet).

  Nadhani nimejibu swali lako kwa ufasaha.

  -> Mwana wa Haki
   
 3. m

  mnyamangeso Member

  #3
  Sep 17, 2010
  Joined: Jun 27, 2010
  Messages: 33
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  yap, Nashukuru
   
 4. Amoeba

  Amoeba JF-Expert Member

  #4
  Sep 17, 2010
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 3,328
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 0
  Mkuu haya maelezo kweli ni ya kina, lakn nadhani huyu jamaa yetu ana tatizo lingine kwa sababu websites alizotaja hazijafungiwa! udsm.ac.tz, out.co.tz ziko hewani mpaka sasa!
   
 5. m

  mnyamangeso Member

  #5
  Sep 17, 2010
  Joined: Jun 27, 2010
  Messages: 33
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  sasa mbona mnaanza kunichanganya?
   
 6. Chamoto

  Chamoto JF-Expert Member

  #6
  Sep 18, 2010
  Joined: Dec 7, 2007
  Messages: 2,086
  Likes Received: 1,125
  Trophy Points: 280
  Kama umeshatumia browser zaidi ya moja basi inawezekama ip yako iko banned. Unaweza kujaribu kutumia proxy kucheki kama tatizo ni ip. Tumia hii ip ya canada (174.142.104.57:3128) mimi huwa naitumia sana kudanganya mahali nilipo.

  A. Ku-Set Up Proxy Fuata Haya Maelezo

  Ili kujua kama tatizo ni ip kwanza kabisa ondoa cookies na cache zote halafu nenda hii tovuti kuona ip yako IP Address Geolocation to Identify Website Visitor's Geographical Location

  Kama unatumia Firefox 6


  1. Nenda "tools" halafu bonyeza options
  2. kiboksi kikitokea gonga "Advanced" (juu upande wa kulia)
  3. Chini kidogo utaona tabs nne (General, Network, Update na Ecryption) wewe gonnga Network.
  4. Upande wa kulia utaona setting button, bonyeza
  5. Connection settings itatokea. Natumaini "No proxy" radio button itakuwa selected. Sasa wewe bonyeza "Manual proxy configuration" Hivyo viboksi vita kuwa activated.
  6. Sasa weka 174.142.104.57 kwenye kiboksi cha kwanza kushoto na "3128" kulia kwake.


  Click OK hicho kiboksi na kile cha kwanza halafu ondoa cookies na caches, halafu jaribu kutembelea IP Address Geolocation to Identify Website Visitor's Geographical Location kuona kama ip yako imebadilika.Kama imebadilika nenda kutembelea hizo tovuti zako

  Kama unatumia Internet Explore


  1. Nenda tools halafu chagua "Internet Options"
  2. Katika tabs za juu bonyeza"connections"
  3. pale chini upande wa kulia kuana kiboksi cha "LAN Settings". Bonyeza kile.
  4. Kiboksi kikitokea chagua "use a proxy server for ypour LAN..."
  5. Weka 174.142.104.57 upande wa kushoto na 3128 upande wa kulia. Bonyeza OK viboksi vyote viwili.
  6. Jaribu kutembelea hizo tovuti

  Click OK hicho kiboksi na kile cha kwanza halafu ondoa cookies na caches, halafu jaribu kutembelea IP Address Geolocation to Identify Website Visitor's Geographical Location kuona kama ip yako imebadilika.Kama imebadilika nenda kutembelea hizo tovuti zako


  ** ONYO **
  Baada tu ya kumaliza kutembelea hizo tovuti rudisha settings za connection kama mwanzo (yaani bila proxy).
  Pia kam utatembelea google wakait umetumia proxy usishangae kukuta homepage ya google inasema "We're sorry but..." hii ni kwasababu hii proxy (IP) ni ya public na watu wengi huitumia kusend automated query google kwahiyo google huwa wanaiban mara kwa mara.  B. Kama bado unatatizo jaribu "diable firewall kama iko ON halafu tembele tovuti zako.


  C. kama hii haija saidia angalia hosts file yako kama ina block hizo sites

  location ya hosts file

  Windows 95 - C:windows
  Windows 98 - C:\windows
  Windows Me - C:\windows
  Windows 2000 - C:windows\system32\drivers\etc
  Windows XP - C:\windows\system32\drivers\etc
  Windows NT - C:\winnt\system32\drivers\etc
  Windows Vista - C:\windows\system32\drivers\etc  kama unakitu kama hiki hapa chini wakati www.domain-fulani.com ni moja ya hizo domain unazo taka kutembelea futa hako ka line, save hiyo file halafu itembelee.

  127.0.0.1 www.domain-fulani.com
   
 7. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #7
  Sep 18, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  je hizo website zinazoshindwa kufungua

  • Kuna error message or error code inatokea? kama ipo ni ipi?
  • browser inasearch page muda mrefu bila kutoa ujumbe wowote?
  • Umejaribu kuzinfungua hizo site kupitia link za google.?
  Binafsi nimefungua TRA na UDSM zote ziko bomba. kwa hiyo kama unaweza kuaacess site nyingine kama google , yahoo na jamii forums tatizo litakuwa kutoka kwa ISP wako kwenda kwenda kwenye hizo site. May be ISP DNS database haiko updated. Inashindwa kujua ni route gani ya kuzizafirsha hizo packets.

  Sasa ku confirm au kuverify kama tatizo liko kwenye routing trace route itakupa jibu.

  jaribu ku run hii command ya Dos
  >>tracert udsm.ac.tz

  Unaweza kusoma hapa kazi ya hiyo command http://www.mediacollege.com/internet/troubleshooter/traceroute.html

  Utajua kazi yake ambayo itakuonyesha packet za hizo site unazo request zinakwama wapi. ukishindwa kutafisri feedaback unayopata idondoshe hapa.
   
 8. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #8
  Sep 18, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Ebu tuelimishane hii kivipi ukitumia browser zaidi ya moja Tra na UDSM wana kuban?

  [FONT=&quot]Alafu hizo procedure za kutumia hiyo proxy kwangu zimegoma.[/FONT]
   
 9. Chamoto

  Chamoto JF-Expert Member

  #9
  Sep 18, 2010
  Joined: Dec 7, 2007
  Messages: 2,086
  Likes Received: 1,125
  Trophy Points: 280
  Pale nilimaanisha kama ni site moja lakini kwasababu site mbili tofauti zinagoma basi tatizo sio ip banned.

  Nimeitesti hii proxy sasa hivi na inafanya kazi sasa sijui kwanini kwako inagoma.

  Jinsi ya kusetup proxy


  Kwani error gani unipata kwenye browser?

  Unaweza ku download addon ya firefox Live Http headers ili uone transaction ya header inakwendaje. Itakusaidia kujua error gani unapata kutoka kwenye server ya UDSM na hiyo ya TRA. Unaweza ku-run hiyo addon halafu uka attach copy ya hiyo transaction hapa ili tuone tatizo ni nini.

  Jinsi ya kutumia live httpheader

   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 10. m

  mnyamangeso Member

  #10
  Sep 18, 2010
  Joined: Jun 27, 2010
  Messages: 33
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  browsers zinatumia muda mfupi kusearch na zinatoa error ya 'page/server can not be found'. vilevile hamna search engine inayoweza kunilink including google zaidi ya matoleo yao yenye vichwa vya habari.

  nimejaribu kutrace route udsm.ac.tz,out.co.tz zinaleta:-

  unable to resolve target system name.

  na nyingine kama ya trapad.co.tz inaleta:-

  over a maximum of 30 hops

  1. <1ms <1ms <1ms myrouter ip address
  2. isp server ip reports: destination host unreachable
  trace complete.

  conclusion: mpaka sasa siwezi kuziaccess some of these websites za hii familia ya .tz
   
 11. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #11
  Sep 19, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Tatizo nadhani ni Domain Namae Server Database ya ISP wako ina kasheshe kama vile kuwa na wrong routing information of Next hop hasa kwa kwa .tz domain.

  Lakini kwa issue hii ni wazi hata ukiwaambia wao watakueleza ni kompyuta yako na wakiwa wajanaza zaidi watawarushi mzigo kuwa ni matatizo Telephone service provider kama ni kamapuni tofauti na ISP.
   
Loading...