Ndugu huyu mtoto ukweli kabisa nimenyoosha mikono. Maana toka darasa la tano alianza Tabia ambazo ni za kutoroka nyumbani hadi wiki.Pengine zaidi na humu ndani Nina RB za kumtafuta ndani ya droo ziko karibu ishirini
Na mbaya zaidi nimekuja kugundua ameanza na kuvuta bangi Na sijui anazitoa wapi kingine kawa mwizi kiasi kwamba hadi inaperekea jirani kunichukia
Maana linapoiba huko wanakuja nyumbani ni nawaambia jamani nyie mkamateni Pelekeni polisi ili afungwe.
Hivi kwa sasa hayupo hapa nyumbani karibu wiki2 na kaondoka kaniibia betri ya gari yangu akaenda kuuza nilipomwambia kalilete ulikolipeleka ndio sikumuona Tena.
Ikanilazimu ninunue betri nyingine mpya pasipokutegemea
Maana gari hii auto muda wote lazima uwake kwa betri.
Sasa ndugu zangu kunamsomi hapo? Tuongee ule ukwelituu!
Sent using
Jamii Forums mobile app