Msaada : Wali wa jiko la gesi

music mimi

JF-Expert Member
Joined
Jun 16, 2013
Posts
500
Reaction score
888
Nimezoea kupika wali jiko la mkaa hapo zamani .. Sasa nimeanza kujipikia mwenyewe tatizo Nikipika wali kwa jiko la gesi ukianza kukaukia nikiutoa either utakuwa umeungua au mbichi hauliki.. Nipeni mbinu za timing ya kuuivisha vizuri.
 
Nimezoea kupika wali jiko la mkaa hapo zamani .. Sasa nimeanza kujipikia mwenyewe tatizo Nikipika wali kwa jiko la gesi ukianza kukaukia nikiutoa either utakuwa umeungua au mbichi hauliki.. Nipeni mbinu za timing ya kuuivisha vizuri.
Ukishachemkaa ukaona maji yanapungua zungusha kiwashio cha jiko taratiibu kama unazima... Kuna pahali utapata moto mdogoooo sasa unabkza hapo wali wako unaufunikaa unaiva taratibu na mvukee kama unafoilng pepa itakusaidia zaidi au wengine wanafunika na mfuko wa plastik hii uzuia mvuke usitoke na utengeneza joto jingii na wali wako utachambuka na kuiva vzuurii... Baada ya mfuko au foilng ndipo funiko lako lafata juu.

Kama kiuchumi uko vzr nunua race cooker
 
Ukishaweka mchele punguza moto mpk mwisho maji yakianza kauka tafuta mfuko wa nailon uoshe ufunike wali na mfuniko unaiva na mvuke
 
Cheza na kuongeza na kupunguza moto,
Mfano umeweka mchele maji yakianza kukauka unapunguza moto kisha unageuza chakula, ni mwendo huo mpk utapoona kinalika
Asante mkuu
 
Nashukuru kwa mchango wako
 
Maplastick yanaketa kansa
 
race[emoji12] cooker!...sawa hv sh.ngap?
 
1.Loweka mchele kama dk10 kabla ya kupika

2.Then andaa maji ya moto kwenye sufulia kama kawaida (hakikisha maji yanakuwa yamepita level ya mchele kama inch moja hivi)

3.Weka mchele jikoni,washa moto wa kawaida tu.

4.Funika chungu chako vizuri.

5.Ukikaribia kukauka punguza moto(uwe mdogo kabisa)

6.Subiri kama nusu saa utakuwa umeivisha vizuri.

NB.Sijawahi kuunguza.
 
Umemjibu vema lakini mfuko una madhara makubwa sana kwa afya yako.
Usitumie tafadhali nakusihi kwa neema ya Bwana.
Kama huna foiling, banika tu hvyo kwa huo moto mdogo, after some minutes ugeuze, then uendelee kubanika zaidi kwa moto uleule.

Mind this: majiko mengine ya gas yana tabia ya kujiongeza moto, hakikisha unakua makini usiunguze.
 
Nimezoea kupika wali jiko la mkaa hapo zamani .. Sasa nimeanza kujipikia mwenyewe tatizo Nikipika wali kwa jiko la gesi ukianza kukaukia nikiutoa either utakuwa umeungua au mbichi hauliki.. Nipeni mbinu za timing ya kuuivisha vizuri.
Mkuu yani wali wa gas wa mkaa hauoni ndani. Fanya hivi weka mafta ya kutosha ukaange mchele wako vizuri kwenye sufulia lenye mfuniko. Kisha weka maji yaliyo chemka yafunikemchele wako kama nusu centimetre au chini ya hapo.
hakikisha moto umefungulia kiasi ambacho ndani ya dakika 1.5-2 hayo maji yatakuwa yamepotea.
Then ukiona tu yamepotea punguza moto ubaki chini kabisa yani ubaki kidogo sasa hapo wali utaiva kwa mvuke.
Uache ukae uwe waugeuza kila baada y dakika kama 3. baada ya dakika kama 25 wali utakuwa umeiva na kuchambuka.
Usisahau kuweka hiriki pia.
Maujanja toka kwa seneour bachelor...
 
Ukishaweka mchele baada ya maji kucheka subir maji yakaribie kukauka then punguza moto uwe spidi ya mwisho kabisa then funika sufuria yako na foil paper
N.B ni bora utumie foil paper kuliko mfuko
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…