Sildenafil Citrate
JF-Expert Member
- Jan 29, 2021
- 573
- 2,553
Haushauriwi kujifungia chumbani ukiwa unalala au wakati wa kupika chakula wakati unatumia jiko la mkaa.
Aina hii ya jiko huzalisha gesi yenye sumu inayoitwa Carbon monoxide (CO) ambayo huufanya mwili usipate kiasi cha kutosha cha hewa safi ya Oxygen inayohitajika kwenye upumuaji.
Ikiwa changamoto hii itatokea, mhusika anaweza kupatwa na maumivu makali ya kichwa, kizunguzungu, uchovu mkubwa, kuongezeka kwa mapigo ya moyo, kukata kwa pumzi na hatimaye kupoteza fahamu.
Sumu ya carbon monoxide (CO) inaweza pia kusababisha uharibifu wa kudumu kwenye seli muhimu za ubongo pamoja na kusababisha kifo ikiwa msaada wa haraka hautatolewa.
Kwa watu wanaotumia aina hii ya jiko kwenye kupika chakula wanapaswa kufungua madirisha ya nyumba pamoja na kuruhusu upatikanaji wa hewa ya kutosha. Aidha, kwa wale wanaolala na jiko la mkaa wakati wa baridi kali wanashauriwa kuacha tabia hii inayoweza kugharimu maisha yao.
Chanzo: Mayo Clinic