Msaada wako unahitajika...

Boflo

JF-Expert Member
Jan 20, 2010
4,384
4,409
Utamsaidiaje huyu binti?...

NIACHANE NA HUYU MZUNGU?

Naomba wadau wanisaidie kwa ushauri,
Mimi ni msichana mwenye umri wa miaka 24, kuna mzungu alitokea kunipenda na tukawa tunawasiliana kwa internet tu kwani yupo mbali na mimi, urafiki wetu umekuwa ni wa muda mrefu, kiasi kwamba tumetokea kuzoeana sana na kuambizana kila kitu, ahadi ni nyingi alikuwa ameziweka kwangu ikiwemo ahadi ya kunioa, ni mtu wa kusafiri mara kwa mara na ikitokea amepata safari yoyote ya Africa huwa ananitumia Ticket namfuata.

Tatizo langu ni kwamba kila tunapoonana hapendi kuongelea swala lolote la ndoa na pia sijawahi kumwomba hata hela na huwa ananipa kiasi ambacho hakikidhi hata mahitaji yangu ya siku, nimekuwa naumia mwenyewerohoni nikiamini ladba ananipima ajue mimi ni mtu wa aina gani.
Niliporudi TZ last week nikapata tatizo ikabidi nimwombe some amount ili niweze kusolve tatizo langu, nilipomtumia email hakunijibu, na tangu siku hiyo hanipigii simu wala haniandikii tena email kama mwanzo.

Wadau wote naomba ushauri wenu.

Hurt me with the TRUTH...But don't comfort me with a LIE!
 
Boflo likizo imeisha, naona umerudi tena, sasa huyo anteomba ushauri ni wewe ama ni mtu mwingine?
 
Boflo likizo imeisha, naona umerudi tena, sasa huyo anteomba ushauri ni wewe ama ni mtu mwingine?
sio mimi....hujaacha tu vituko vyako....niko jamvini siku zote, siwezi kubanduka sema nilisusa tu kumwaga mtama
 
Kwanza kama mmekuwa marafiki mda mrefu haman haja ya kujua wewe unahitaji nini na kama ni suala la ndoa inabidi kwa kipindi hiki chote uwe umeshamuuliza ana mpango gani na wewe. Ikitokea kama hatakujibu tena ujue alikuwa hana nia ya maisha ya baadae kama wewe ulivyodhani-La kufanya wewe weka mda maalum wa yeye kukukumbuka na kukusaidia. Na asipokujibu tulia kwanza muombe mungu na naamini atakufungulia yule aliye wako.Lazima uwe na maamuzi mazuri,ukishaamua kuachana naye ukapata mwingine-cyo arudi tena kukuharibia relashionship yako. Kumbuka sala ni msingi wa kutatua matatizo yote. Note: Kama mtu anakupenda naamini c mpaka umuombe hela,la hasha lazima ana wajibu wa kujua unahitaji nini kama mchmba,girlfiriend au mke. Ni hayo.
 
Tatizo la hawa wadada wanaokuwa na uhusiano na wanaume wa kizungu wanadhani wote ni matajiri. Wengi wao hasa wale wanaokuja Afrika ni watu wa hali ya chini kwao na ndio maana wanakubali kuja kuumwa na mbu!! Wasichana wanadanganyana kwa kuoneshana picha za nyumba na magari ya kifahari huko waliko; hayo magari ni ya kukodisha na nyumba za kupanga sio mali zao kama wanavyotaka nyie muamini. If anything hao wenzenu walioolewa na wazungu wanatumika kama makuwadi kuwatafutia wanaume wa kizungu wanawake na wao hulipwa commission kwa kuwauza nyie!! Msione ajabu habari ndio hiyo; mnakuwa malaya lakini wa hali ya juu[ high priced prostitutes]. Huyo mwanaume hana lolote anataka kukutumia tu na usipoangalia atakupeleka kubaya; achana nae tafuta kibarua cha maana nyumbani hata kama ni kupika vitumbua utaheshimika na kuepuka maradhi.
 
Utamsaidiaje huyu binti?...
NIACHANE NA HUYU MZUNGU?

Naomba wadau wanisaidie kwa ushauri,
Mimi ni msichana mwenye umri wa miaka 24, kuna mzungu alitokea kunipenda na tukawa tunawasiliana kwa internet tu kwani yupo mbali na mimi, urafiki wetu umekuwa ni wa muda mrefu, kiasi kwamba tumetokea kuzoeana sana na kuambizana kila kitu, ahadi ni nyingi alikuwa ameziweka kwangu ikiwemo ahadi ya kunioa, ni mtu wa kusafiri mara kwa mara na ikitokea amepata safari yoyote ya Africa huwa ananitumia Ticket namfuata.

Tatizo langu ni kwamba kila tunapoonana hapendi kuongelea swala lolote la ndoa na pia sijawahi kumwomba hata hela na huwa ananipa kiasi ambacho hakikidhi hata mahitaji yangu ya siku, nimekuwa naumia mwenyewerohoni nikiamini ladba ananipima ajue mimi ni mtu wa aina gani.
Niliporudi TZ last week nikapata tatizo ikabidi nimwombe some amount ili niweze kusolve tatizo langu, nilipomtumia email hakunijibu, na tangu siku hiyo hanipigii simu wala haniandikii tena email kama mwanzo.

Wadau wote naomba ushauri wenu.

...hehehe, waingereza mchezo! wabahili kama nini hao. Funzo kwa kina dada wote wanaowashobokea wanaume wa kiingereza. Aheri ya wa Scottish au Welsh. Hawa waingereza wa England kuanzia Cab, vinywaji Pub nk kila mtu anajilipia hata kama ni mtu na g'friend wake.
Bisha sasa kama huyu mwanaume sio mdhungu wa England!
 
watawashinda wafaransa kweli?......
 
Back
Top Bottom