Msaada wako unahitajika

Oct 29, 2015
59
31
Helen Keller alishapata kusema "Alone we can do so little; together we can do so much", na bwana Henry Ford yeye alisema "If everyone is moving forward together, then success takes care of itself". Waswahili nao wakasema "penye wengi hapaharibiki neno", kwa kutambua hayo yote, na kwa kujua kuwa "hakuna mtu anayeweza kufanikisha jambo lolote pasipo mikono ya binadamu wengine", ninakuja mbele yenu nikiwa nimekwama. Lakini mahali nilipokwama, natambua kuna raia wenzangu wako vizuri sehemu hiyo. Kiufupi, mimi ni mbunifu ambaye nimeamua kufanya kazi zangu za ubunifu kwa kuelimisha watanzania wenzangu. Na kwa kuanza, nilitengeneza video katika mfumo wa uhuishaji(animation). Nilipeleka video hizo katika baadhi ya vituo vya TV hapa nchini, na katika kituo kimoja nikashauriwa hivi, "mfumo wa animation unaonekana kama mfumo maalumu kwa vipindi vya watoto", hivyo nikashauriwa nitengeneze video katika mfumo uliozoeleka hapa Tanzania. Na hapo ndipo, ninacholeta mbele yako kikajitokeza. Kwa kuwa mimi nilikita akili yangu katika utengeneza video za animation pekee, software ambazo nilikuwa nazo ni zile za kutengenezea animation, na pia sikuwa nimenunua kamera kwa ajili ya video shooting. baada ya kukumbana na changamoto hiyo, niliamua kwenda kwenye baadhi ya benki kuulizia hatua za uchukuaji mkopo, kikwazo kikawa sina ajira. Hivyo, ninaomba kwa mtu ambaye yupo tayari kunidhamini katika project yangu, au pia kama unamfahamu mtu au taasisi inayoweza kunidhamini ili kufanikisha project hii, unijulishe.
Eneo ninakopatikana ni Dar Es Salaam. Na kiasi ninachohitaji ili nifanikishe hatua ya awali ya project hii ni Tshs 3,000,000. Ninaamini, nitapata msaada hata wa kiushauri.
 
Wazo zuri,na inakenaka vijana baada ya IT kufanya yake wengi saana mmeibuka na mawazo,sio mbaya.
Ila lazima ujielezewe kwanza pesa hizo ni mkopo au msaada,na zinakulipaje utazilipaje.

Maana haya kwenye vipindi vya watoto kwenye TV zote almost zinaandaliwa na wafanyakazi wa TV na sio kama mtu kanunua kipindi.
 
tuwekee animations zako tuzicheki. unaweza pata angel investors ukawa kama disney.
 
Back
Top Bottom