Msaada wa ushauri kwenu wanajamvi

Jifunafu

Senior Member
May 25, 2020
182
598
Kichwa cha habari chajieleza, mimi ni Mtanzania nipo wilaya ya Kasulu huku vijiji vya ndani kabisa.

Ninahitaji kufungua ofisi ya kuchaji simu, kurusha nyimbo kwenye simu na kubarn cd kwa kutumia computer desktop na pia kuonyesha mpira pia.

Ninaomba ushauri kwenu ni aina gani ya nishati ya umeme mzuri kutumia maana huku nilipo hakuna umeme wa Tanesco.

Je kuna solar inayoweza kuendesha vifaa hivi kwa wakati mmoja ili kupunguza gharama za kununua mafuta na kutumia generator.

Asante,
Nawasilisha.
 
Kama Tanesco wako mbali na hapo, waone Mobisol watakupa solar yenye uwezo tena kwa mkopo .
 
Back
Top Bottom