Msaada wa ushauri kwa mtoto aliyefeli form two

WA MAMNDENII

JF-Expert Member
Joined
Jun 5, 2010
Posts
344
Reaction score
58
Wanabodi chaliii wangu ananiumiza kichwa kinyama, May mwaka huu anatimiza 18 yrs. Uwezo wake kimasomo tangia primary kiukweli ulikuwa mdogo sana hivyo nilimkaririsha mara nyingi nikadhani ange improve uwezo wake kimasomo mwishowe mtihani wa std 7 matokeo yalikuwa mabaya kiukweli,

Hivyo wakati alipomaliza std 7 nilimwanzishia tuition kwenye shule moja ya secondary ambapo mwaka uliofuata walimsajili form one ingawa hakufanya vizuri mtihani wao wa kujiunga na hiyo shule hivyo walimchukua kwa kuwa walikuwa naye kwenye hiyo tuition na pia walishauri wataendelea kuwa naye karibu wamcheki maendeleo yake.

Sasa matokeo ya form two yametoka na kapata flat F masomo yote.
Nimejaribu kukaa naye private kiurafiki sana kutaka kujua ana mpango gani,

Majibu yake hataki tena kukariri darasa bali anataka kujifunza udereva, japo simwoni saaana ana interest na magari.

Na kabla ya hapo nilikuwa namfuatilia sana ili kujua interest yake kama ana fani anayoipenda lakini alionekana yupo yupo tu.

Nilifikiri swala la chuo cha ufundi lakini veta wanachukua only form 4 kwa fani nyingi na hawachukui vichwa bongo lala

Swala la driving school kwa sasa bado hajafikisha 18. Nafikiri ningepata mahali pa shule ya ufundi ya kumfanya awe busy ili asishinde home kuanzia sasa hapo ndo kichwa kinanigonga wajameni.

Kwa yeyote kwenye hili jukwaa mwenye kaushauri tafaadhali aidha kwa ambao walishakumbana na changamoto kama hii yangu.
 
usimlazimishe aseme, mpeleke chuo cha ufundi + driving
 
Kama amesema anapenda udereva hata kama haonyeshi jitahidi umsaidie huko huko aende ila mpeleke gereji za magari, ongea na fundi mkuu mkabidhi atajifunza na atabadilika.
Nilikuwa na kijana kama huyo huyo wako nikampeleka gereji Fulani alibadilika sana baada ya kujifunza kwa miaka minne, sasa hivi amefungua ofisi wanashirikiana na wenzake wanapiga pesa .
 
Asante kwa ushauri kiongozi,
 
Ilo ndo tatizo la watanzania.
Kulazimisha watoto wakae darasani wasome kwa nadharia.
Wakati vichwa vya watoto wao vinashika mambo ya vitendo.
Huyo mtoto peleka gereji,peleka akasomee umeme.au ufundi seremala.na kama anataka udereva mpeleke.mwache afanye anachotaka.
Nimekusoma vyema mkuu
 
Kwa ushauri wangu ni vizuri kwa sasa arudie darasa. Kuna msingi wa elimu ambao anatakiwa kuwa nao ndipo aendane na ndoto zake. Watu wanaosema watanzania tunapenda kuwalazimisha watoto wasome bila kujali wao wanataka nini ni sahihi ila mwandalie japo njia ya yeye kupita kwanza. Hata hao wazungu ndio haswaa wapo makini kwenye hilo. Mara nyingi wao wana elimu sana ila katika kuamua kazi ndo huwa wanapenda kufanya wakipendacho, Hivyo basi kumpa msingi hata huo wa form4 utamusaidia sana kupata huo udereva wake anaohitaji na umweke katika mazingira mazuri. Hapa wewe kama mzaz tumia njia zote na ongea nae mpe faida ya hicho cheti kitakavomsaidia akiwa dereva na jarbu kumwahidi kama wewe pia utahakikisha upo nyuma yake ila baada ya kufanya nini unachotaka wewe mzaz wake, Mweleze matamanio yako kwake yalikuwa kwanza amalize form4 ndipo asome anachotaka.
Kama ukishindwa kwa hilo pia basi hakuna namna mpeleke, japo naelewa tuendako lazima atakuja kukumbuka na kurudi shule japo apate 4 ya mwisho.
 
Kwanza nashukuru kwa ushauri mkuu.

Ni kweli mkuu nilikuwa natamani sana japo afike f4 potelea mbali hata akifeli atakuwa ameongeza maarifa na ukomavu wa akili plus leaving certificate. Ila ndo hivyo nimejitahidi sana kumweleza umuhimu wa f4 tatizo ni ugumu ninaouona hata akirudia f2 uwezekano wa kuvuka ndio pagumu.
 
Wanabodi chaliii wangu ananiumiza kichwa kinyama, May mwaka huu anatimiza 18 yrs. Uwezo wake kimasomo tangia primary kiukweli ulikuwa mdogo sana hivyo nilimkaririsha mara nyingi nikadhani ange improve uwezo wake kimasomo mwishowe mtihani wa std 7 matokeo yalikuwa mabaya kiukweli,

Hivyo wakati alipomaliza std 7 nilimwanzishia tuition kwenye shule moja ya secondary ambapo mwaka uliofuata walimsajili form one ingawa hakufanya vizuri mtihani wao wa kujiunga na hiyo shule hivyo walimchukua kwa kuwa walikuwa naye kwenye hiyo tuition na pia walishauri wataendelea kuwa naye karibu wamcheki maendeleo yake.

Sasa matokeo ya form two yametoka na kapata flat F masomo yote.
Nimejaribu kukaa naye private kiurafiki sana kutaka kujua ana mpango gani,

Majibu yake hataki tena kukariri darasa bali anataka kujifunza udereva, japo simwoni saaana ana interest na magari.

Na kabla ya hapo nilikuwa namfuatilia sana ili kujua interest yake kama ana fani anayoipenda lakini alionekana yupo yupo tu.

Nilifikiri swala la chuo cha ufundi lakini veta wanachukua only form 4 kwa fani nyingi na hawachukui vichwa bongo lala

Swala la driving school kwa sasa bado hajafikisha 18. Nafikiri ningepata mahali pa shule ya ufundi ya kumfanya awe busy ili asishinde home kuanzia sasa hapo ndo kichwa kinanigonga wajameni.

Kwa yeyote kwenye hili jukwaa mwenye kaushauri tafaadhali aidha kwa ambao walishakumbana na changamoto kama hii yangu.

Mruhusu afanya kitu kingine anachopenda, hakujaliwa huko, and yet anaweza kufika mbali kama walioenda shule!
 
Mpeleke tena shule plan kubwa iwe akafute ujinga kijana bado mdogo.
 
akarriri tu Darasa hata huo udereva ataharibu magari ya watu
f flat khaaaaaaaaa
 
Msogeze sogeze amalize tu form four, unaweza kumtafutia tuition afanye mitihani kama private candidate labda mazingira ya shule hayamfai kusoma
Wakati uko nae chungu za kipaji chake, Mungu hakunyimi kila kitu, anaweza kuwa mzuri kwa kazi za mikono kama kupika, kushona au mechanics. Unaweza kumwendeleza huko.
 
Kwanza nashukuru kwa ushauri mkuu.

Ni kweli mkuu nilikuwa natamani sana japo afike f4 potelea mbali hata akifeli atakuwa ameongeza maarifa na ukomavu wa akili plus leaving certificate. Ila ndo hivyo nimejitahidi sana kumweleza umuhimu wa f4 tatizo ni ugumu ninaouona hata akirudia f2 uwezekano wa kuvuka ndio pagumu.
Hayo ndiyo mawazo magumu tunayohitaji sisi kama wazazi. Unaweza shangaa hili tu la kurudia shule anaipenda balaa na hatimaye analeta matokeo chanya hadi unashangaa.ila siyo kukata tamaa.
 
Back
Top Bottom