Msaada wa Ujenzi wa Nyumba | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Msaada wa Ujenzi wa Nyumba

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Sina pa kwenda, Aug 2, 2011.

 1. S

  Sina pa kwenda Senior Member

  #1
  Aug 2, 2011
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 116
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Habari zenu wanajamvini, kwanza kabisa nimezunguka kutafuta viwanja kila sehemu bei juu yaani kila kitu siku hizi kimepanda, msadaa wa kwanza nataka kununua kiwanja nielekezeni ni mitaa ya wapi nitapata kiwanja ambacho bei yake iko pouwa kwa hali ya mtanzania kama tujuanavyo halafu pili nikitaka kujenga nyumba ya kawaida yaani, vyumba vitatu vya kulala, sitting rum, dinning, jiko na choo inaweza ikacost howmuch?
   
 2. Dr wa ukweli

  Dr wa ukweli JF-Expert Member

  #2
  Aug 2, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 892
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  viwanja vipo vingi sana unataka wapi na unakiasi gani? kama uko Dar masaky, knyama, mbezi beach viwanja vizuri vinaanzia 50M ila maeneo kama mbagala mwisho, chanika, kongowe, mvumoni, goba kuanzia 2M unapata. ujenzi wa nyumba inategemea na mateial na quality ya nyumba kama fance nk ukiwa na 25M waweza jenga kigumu.
   
 3. Who Cares?

  Who Cares? JF-Expert Member

  #3
  Aug 2, 2011
  Joined: Jul 11, 2008
  Messages: 3,465
  Likes Received: 1,951
  Trophy Points: 280
  haya maeneo niliyo ya-bold yana-utata tosha
  1- masaki, knyama mbezi beach etc... hakuna viwanja vya bei hizo... bei inaanzia 100m kwa maeneo ya mbezi na knyama ila masaki inaanzia usd 300,000- usd 3,000,000. kama huamini soma matangazo kwenye magazeti utakubali mwenyewe
  2- kiwanja cha 2m hupati mitaa ya goba na mivumoni labda mbagala
  3- nyumba ya 25m 3-bedrooms sio kweli labda ajenge asiweke milango, madirisha, umeme, maji etc...iwe amejenga banda na kulivunika bati..tena bati zenyewe ziwe zileee za kizamani..kitaalamu zinaitwa corrugated iron sheets na sio hizi mnazoita za south afrika au migongo mipana kitaalamu Industrial trough sheets... ni mtazamo wangu wa kitaalamu na kijamii zaidi.
   
 4. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #4
  Aug 2, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Kuwa mwangalifu sana unapotafuta kiwanja na wapi kunafaa.
  Mosi wakijua kwamba unatafuta kiwanja kwa nguvu zote kila mmoja atapandisha dau utashtukia mtaji wako unaishia kununua kiwanja.
  Yalinipata hayo yanayokupata leo nilitaka kuingia kichwa kichwa wakati bongo nilikuwa nimeaiacha mika kadhaa kumbe kumebadilika sana, nikaamua kutuliza kichwa kwanza na kujifanya kama mdadisi na mwenye kutaka kujua biashara ya viwanja inavyoenda, nakuambia sikuchukua hata wiki nikapata nyumba ya kununua iliyo kuukuu kwa bei chini ya kiwanja na kuharakisha kubadilisha hati miliki wizara ya ardhi hadi le, nikaibomoma na kujenga yangu upya, namshukuru Mungu.

  • Mambo ya msingi unapotafuta kiwanja cha kujenga kama ni nyumba ya kuishi na familia yako, kwanza angalia mambo ya msingi katika maisha kama usafiri, umeme na maji hayo kwangu ni kipaumbele kwanza.
  • Isije kuwa taabu kwako kuvuta umeme toka maili tano ikakuingizia hasara isiyozibika haraka.
  • Usafiri nao ni muhimu kwani haitaingia akilini uwe unaliacha gani kwa jirani akutunzie kwa vile barabara ya kufikia uishika haipitiki hata kwa mkokoteni.
  • Kama eneo unalotaka kujenga linauwezekano wa kuchimba (drill) kisima kwa ajili ya kujitegemea maji maana tunajua wazi huduma ya maji toka huduma za kijamii ni kitendawili tega.
  Ukishajiridhisha yaho kati ya viwanja kadhaa ulivyopata, unaweza chagua kimoja ambacho unaona kinakidhi mahitaji yako, ndo maana usiende papara kupata kiwanja fanya uchunguzi wa kutosha na hati miliki kabla hujagawa madafu.
  Kisha fanya tadhmini ya ujenzi wa nyumba yako kutokana na ramani yako ambayo na hakika mchoraji atakuwa ameshakufanyia makadirio yake, na kama hujafanya hayo soma paragraph ifuatayo.

  Kwa vile gharama za uchoraji ni ghali, jaribu kupunguza gharama kwa kuwaona maofisa wa mipango miji idara ya ujenzi wana ramani nyingi tu hivyo wanaweza kukumegea moja unayoipenda kwa gharama nafuu ukaitumia kufanya makadirio ya gharama za ujenzi wa nyumba yako. Kukuambia kwamba ujenzi wa nyumba yako ni milioni 30 tutakudanganya maana kuna mengi ambayo yanatakiwa kupitia katika kupata mahesabu sahihi kutokana na eneo, hali ya ardhi, mwinuko au tambalare, vifaa utakavyotumia kujenga, na mtindo wa nyumba utakaojenga. Ndio maana utafiti ni muhimu kufanya kabla hujafanya hayo.

  Cha msingi hangaikia kupata kiwanja kwanza na baada ya kupata utaweza saidiwa na wazoefu hapa gharama za makadirio ya ujenzi wa nyumba yako.
   
 5. u

  ureni JF-Expert Member

  #5
  Aug 2, 2011
  Joined: Jun 14, 2011
  Messages: 1,272
  Likes Received: 232
  Trophy Points: 160
  <br />
  <br />
  Ni kweli kabisa kupata kiwanja kwa milioni mbili maeneo ya goba sio rahisi na kama utapata kitakua ni kidogo sana na kitakua kipo ndani sana porini huko ambapo hata umeme na barabara hamna,mie nilipokuwa natafuta kiwanja kinachoeleweka na karibu na barabara kubwa ya lami walikua wanaanzia milioni 30,kadri unavyoingia ndani kutoka barabara ya lami bei inazidi kupungua,lakini niliweza kubahatisha cha shilingi milion 10, km 2 from barabara ya lami ilikua last year.
  Kuhusu garama ya ujenzi hata ukitumia bati za kawaida iko juu sana kwa sasa hivi,ukiwa na milioni 25 hutafika popote itaisha yote.
   
 6. Mshume Kiyate

  Mshume Kiyate JF-Expert Member

  #6
  Aug 2, 2011
  Joined: Feb 27, 2011
  Messages: 6,774
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Mkuu nenda kigamboni kuna viwanja vilivyopimwa tofauti vile vya mradi wa mji wa kigamboni, milioni 5 unapata kiwanja unajenga nyumba yako ya kawaida!
  Mwakani NSSF wanajenga daraja dakika 30 mzee umefika mjini
   
 7. newmzalendo

  newmzalendo JF-Expert Member

  #7
  Aug 3, 2011
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 145
  kigamboni 25km from ferry acre 1 = 1.6mil.
  hamna umeme,maji unachimba kwa 2mil. solar unaweka ya 1mil.
   
 8. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #8
  Aug 3, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Hii imetulia, maana kama viwanja vimepimwa natumaini umeme utaingia punde tu
   
 9. rmashauri

  rmashauri JF-Expert Member

  #9
  Aug 4, 2011
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 3,008
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Mkuu ni eneo gani hilo la Kigamboni? Maana kwa sasa nako viwanja bei iko juu mno. Kwamfano huko Tuangoma viwanja vilivyopimwa vinaaznia 10mil na kwenda juu.

  NB: Mods unganisheni hii thread na ile yenye kichwa cha habari "Gharama za kujenga nyumba Tanzania" iliyoanzishwa na Guantanamo Bay tarehe 24 Sept. 2010 ambako watu wamechangia sana, mawazo, utaalamu na uzoefu wao.
   
Loading...