Msaada wa namna ya kuondoa kiwalaza

XII Tz

JF-Expert Member
Aug 16, 2020
4,293
6,957
Habari wakuu

Mdogo wenu hapa nimekuja nahitaji msaada wenu, nimeanza kuota kiwalaza na hii inanipa stress sana ukizingatia na umri pia bado hauni ruhusu kumiliki vitu vya ajabu ajabu.

Najaribu kujiuliza kwanini kimeniota haraka haraka namna hii ukizingatia pia hatuna historia ya viwalaza kwenye familia yetu, mzee wangu yupo kwenye 60s na ana nywele zote timilifu.

Bro wangu mkubwa yupo early 30s na yeye hana kiwalaza, sasa najiuliza nimekipata wapi na ndio kwanza nimetimiza miaka 20 juzi hapo ??.

Yani upande wa mbele wa kichwa changu nywele zimeacha kuota pembeni mwa komwe ( receding hairline) na pia nyuma kidogo ya kichwa nywele zimeacha pia kuota.

Wakuu sikuwahi kujua kama hii kitu Ina stress namna hii, na ninavyopenda kunyoa viduku basi daah!
 
Basi wew si wa huyo mzee nenda kwa upole muulize mama ako akuonyeshe baba ako mwenye kipara mpaka kisogoni.
Ungepata bahati ya kuniona na ikatokea siku umekutana na mzee wangu akiwa peke yake, hutohitaji hata kuuliza kama ni baba yangu, tumefanana hadi unyayo.
 
pole sana ndugu at 20s kuota uwalaza ni stress tupu. Na rafiki yangu alikuwa anapenda kufuga nyewele but now ni mwendo wa kunyoa kipara
 
Mpk plastic surgery
64FFB877-38D8-45EC-AB49-EF33943587BC.png

Hakuna ulazima mkuu, kuna Hair growth products nyingi tu. XII Tz
 
Back
Top Bottom