Msaada wa namna ya kuandika barua ya kuomba kurudishwa katika ajira ya ualimu baada utoro wa miaka minne

Samsuka

Member
Apr 22, 2011
8
15
Wadau Samahani Naomba msaada wa namna ya kuandika barua ya kurudi katika Utumishi baada ya kuondoka kazini bila kuaga na kupewa barua ya kufukuzwa kazi.

Nilikua mtumishi katika wizara ya Elimu (Mwalimu). Niliondoka kazini bila kuaga tangu mwaka 2018 na kwenda kufanya mambo binafsi ambayo kidogo yalionesha manufaa kwa wakati ule lakini saivi mambo yameenda vibaya na ninatamani kurudi katika utumishi serikalini.

Naomba msaada sana kwa hilo wadau
 
When you listen too much from motivational speakers,they feed and implant your brain with some trashes .

Sasa umerudi we wa kuchapa kabisa.
1669013282261.jpg
 
Ndugu mwandishi tafuta mtu wa halmashauri akusaidie kesi yako umu ndani watakutibua ny'ongo na Maneno yao.

Halmashauri hizo kesi ni nyingi sana so watajua njia gani rahisi kuitumia. Lakin from what I know kunahitajika kuwepo ushahidi wa viongozi wa dini japo sijui wanahusikaje
 
Wadau Samahani Naomba msaada wa namna ya kuandika barua ya kurudi katika Utumishi baada ya kuondoka kazini bila kuaga na kupewa barua ya kufukuzwa kazi.

Nilikua mtumishi katika wizara ya Elimu (Mwalimu). Niliondoka kazini bila kuaga tangu mwaka 2018 na kwenda kufanya mambo binafsi ambayo kidogo yalionesha manufaa kwa wakati ule lakini saivi mambo yameenda vibaya na ninatamani kurudi katika utumishi serikalini.

Naomba msaada sana kwa hilo wadau
Mkuu; Mbona unawatega wenzako? Taratibu na Kanuni za kiutumishi hususan kwa mtumishi wa umma/serikalini si unazifahamu? Ulipoajiriwa kwa mara ya kwanza ulipewa barua JD na ndani yake waliambatanisha kanuni. Hukuisoma vizuri mkuu?
Umekaa nje ya kituo chako cha kazi bila ruhusa au Taarifa kwa mkuu wako wa kazi kwa muda wa miaka minne(4)!!! Halafu unajisumbua kurudi katika Utumishi Serikalini. Huo ni muda mrefu sana -si unaona hata namna ya kuandika barua ya kikazi umesahau. Strictly ni siku tatu(3)tu - wakikuhurumia unapewa barua ya Onyo. Wakikusimamia kooni wanakusimamisha kazi (Utaambiwa na kosa lako) halafu unapewa barua ya kukutaka Ujieleze ni kwa nini Hatua kali za kiutumishi zisichukuliwe dhidi yako ikiwa ni pamoja na kukufukuza kazi mara moja; na unatakiwa uijibu barua hiyo ndani ya siku 14. Inavyoonekana wewe hujafanya hata kimojawapo - labda usubiri Ajira mpya na ikibainika ulishaajiriwa halafu ukawa mtoro kazini............cjui(malizia mweyewe). Hakuna Wizara hapa Tz inayoajiri watumishi wenye sifa ya Utoro kazini Never. Lakini jaribu tu bahati yako. (Samahani lakini kama nimekudidimiza au kukukatisha tamaa)
 
Ukirudishwa niite nyau.
Watu wa halmashauri walivyojaa roho mbaya sijui utapitia wapi.
Hapo ungekuwa kada zingine ambazo haziko chini ya TAMISEMI ningekupa mbinu lakini huko local government ni full roho mbaya.
Mkuu, sio roho mbaya ni Kanuni na Taratibu za kazini, Mbona hata huko Central govt. iko hivyo hivyo?
Kuondoka kwenye kituo cha kazi bila kuaga (ama kwa mdomo au maandishi) ni dharau kubwa kwa waliokupangia hapo, ni utovu wa nidhamu, hauiheshimu wala huipendi kazi yako. Ni ishara ya kiburi na majivuno. Umeitelekeza kazi yako. Wateja wako(wanafunzi) uliwaachaje, nani awahudumie? Wakifeli kwako sio hoja. Shauri yao eti! :oops: :oops: Leo kimenuka huko ulikoenda halafu sasa unataka kurudia matapishi yako.:rolleyes:.
Mkuu, kwa Sentensi ya kwanza "Ukirudishwa niite nyau" umemaliza. Short and Clear.
Asiende kusumbua watu na kupita-pita kwenye makorido huko Ofisini eti nataka kurudi kazini.
 
Wadau Samahani Naomba msaada wa namna ya kuandika barua ya kurudi katika Utumishi baada ya kuondoka kazini bila kuaga na kupewa barua ya kufukuzwa kazi.

Nilikua mtumishi katika wizara ya Elimu (Mwalimu). Niliondoka kazini bila kuaga tangu mwaka 2018 na kwenda kufanya mambo binafsi ambayo kidogo yalionesha manufaa kwa wakati ule lakini saivi mambo yameenda vibaya na ninatamani kurudi katika utumishi serikalini.

Naomba msaada sana kwa hilo wadau

Nenda katafute kazi Private school hata ya kufagia ndipo utapata lakini huko serikalini sahau! Hiyo nafasi ilishajazwa tayari na kuna walimu waliomaliza vyuo bsdo hawajapata ajira, nani akurudishe kazini mtu kama wewe na kwa sababu zipi! Zaidi ya hapo nenda kulima!
 
Back
Top Bottom