Muktadha ni jumla ya vitu, viumbe na hali inayowezesha uwepo wa tukio ama hali fulani mahususi. Mfano, muktadha wa shuleni ni mjumuiko wa majengo, mwanafunzi, Walimu, yanayopaswa kufunzwa, muda n.k. Zingatia kwamba mazingira siyo muktadha bali ni kijisehemu tu kinachoweza kuunda muktadha. Vivyo hivyo muktadha siyo mazingira.